Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii

DP World wameanza kazi mwezi April! Sina hakika kama wamezalisha kiwango hicho.
Mpaka leo Wastaafu wa TPA hawajapewa mafao yao! Gawio linarudishwaje?
 
..kwa hiyo hilo gawio tumepewa na DP world?

..bila DP world tulikuwa hatuna uwezo wa kupata gawio hilo?
Bandari tangu 2000 nije mjini nasikia inapigiwa kelele,kuanzia wizi wa mizigo ya watu mpaka uzembe kiutendaji,Kuna mkongo kontena la tv akakuta maboksi na nylons,siku zote hizo tija imekosekana,unakuja kuuliza Leo Hilo swali!!?
 
DP World wameanza kazi mwezi April! Sina hakika kama wamezalisha kiwango hicho.
Mpaka leo Wastaafu wa TPA hawajapewa mafao yao! Gawio linarudishwaje?
Inashangaza sana ... Ila ccm inatakiwa isome alama za nyakati. Hizi sio enzi za propaganda na uwongo . Na kama ccm bado inajiamini kwamba wataendelea na mazoea yao ya kuiba kura , 2025 watajua hawajui .
 
Asijifanye hatuelewi tunaosema ameuza. Sisi tunataka usimamizi mzuri wa serikali wa mashirika na taasisi zake kwa tija bila kuwepo ufisadi. Hatuwezi kugawa kila kitu eti kupata hela nyingi wakati tunajua vigogo sasa wanakula na wawekezaji badala ya kula moja kwa moja. Lazima wananchi tuendeshe nchi yetu wenyewe kwa uadilifu. Tufaidi kwa wananchi kupata kazi na nchi kupata yenyewe faida.
 
Ndio maana unaona pesa zinamiminika ndio tafsiri ya ufanisi wa mashirika,huko mlikotoka hakuna kitu mlikuwa mnafanya
 
mbona mzigo unatetewa sana nakumbuka kuna yale magawio ya ttcl ila leo kiko wapi
 
TOKAAAAA MAREHEMH ASEMEE AMEFANYA MABADILIKOK KTK WAKURUGENZI WA MASHIRIKA NA MAKAMPUNI BAADA YA KUSIKIA KUNA BAADHI YA WAKURUGENZJ WANAKOPA BENKI PESA KUBWA KULETA KWENYE GAWIO WAKITESA WAFANYAKAZI KWENYE MALIPO KISA PESA ZA BENKI

SINAHAMUNAZO TENA HIZI GAWIO
 
Bandari tangu 2000 nije mjini nasikia inapigiwa kelele,kuanzia wizi wa mizigo ya watu mpaka uzembe kiutendaji,Kuna mkongo kontena la tv akakuta maboksi na nylons,siku zote hizo tija imekosekana,unakuja kuuliza Leo Hilo swali!!?

Suala hili liwekwe kwa uwazi zaidi.

TPA waripoti mapato yao.

DP world waripoti wanachotupatia.

Adani waripoti wanachotupatia.

Tukiwa na taarifa sahihi za hao watatu tutajua namna bora ya kuendesha bandari zetu.
 
Umeambiwa hawatoripoti?
 
Hakika Mwenyezi Mungu ametushushia Samia, eewe mama yetu ulishushwa na mola wetu mlezi, watu wanakuonea kijicho kwakua u kiumbe mtiifu wa allah. Samia to 2030.
 
DP World walianza kitambo, makabidhiano rasmi ndio yamefanyika mwezi Jana ila toka mwaka Jana DP World wapo kazini, waulize importers.
Mbona sijawahi kuona mabadiriko yoyote kuhusu kuwahi kutoka mizigo bandarini, nina zaidi ya miaka 3 napitisha mizigo yangu pale
 
Kwani Kenya hawajaingia kwenye mkataba nao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…