Wanaofujafuja kama wengi walizaliwa miaka ya 90 ni haki yao kudai mabehewa na treni za kisasa Kama zile zinanozoonekana huko mbele.
Oh ngoja kwanza,... Kwani reli inayojengwa si ya kisasa? Iweje reli ya kisasa itumie mabehewa ya Mundo wa kizamani kwa bei ya sasa? Kuna ubaya gani watoto wa kisasa kuhoji?
Kuwapakazia Waha eti wao wameyapenda mabehewa ya kizamani, kama yupo aliyesifia basi ieleweke tu kuwa tangu ilipoundwa TRC baada ya kuvunjika kwa EAR, mabehewa yaliyokuwa na hali mbaya ndio yaliyopelekwa Kigoma na Mpanda.
Kwa maana hiyo juzi kupanda mabehewa yanayofanana na yale ya Deluxe, ambayo hata hivyo inaenda Kigoma kwa kubahatisha, ni wazi baadhi ya Waha wameiona tofauti..... Lakini siyo kwa kubezwa hivyo!.