Rais Samia, Watanzania kuruhusiwa kufanya kazi Kenya tuepushe na mtego huo

Happy new Year!
Nahisi uko nyuma kwa fikra! Unategemea m-TZ akatafute ardhi Kenya! For what? Kenya ndo wanahangaika kutafuta ardhi TZ. Mbona hamtafuti ardhi Uganda? firstly, Solve your internal problems. Badala ya kutatua matatizo ya Kenya, unatafuta njia ya kupeleka matatizo yako nje, kwa jirani! Rubbish!
Nimeosha mikono!
 
Mwenye akili nyingi aliyeleta ndege zenye hasara ya 60 bil? Sasa hiyo ndio akili nyingi?
Nawe boss, jaribu kukwepa kuzoa kila unachosikia. Umeshindwa hata kutafsiri hiyo 60 billion! sasa unaishikilia kama wimbo wakati sisi tumeshaelewa maana yake!
 
Njoo uchukue dual-citizenship, uone ka hununui ardhi kulingana na uwezo wako. Nyie ndio Mh. Mama Samia anaongelea mbungeni kuwahusu. Mwache hiyo akili.
Frankly, Kenya ina majirani wangapi? Why always Tanzania! Try with Somalia, Ethiopia, South Sudan, or Uganda. Mulijaribu Somalia, nothing! Mulijaribu Ethiopia, nothing! Mukajaribu Uganda, nothing! South Sudan mumewasaidia kuficha pesa za wizi. Politics aside, Kenya is a bad neighbour.
 
Mimi sioni mtego wowote hapo, Kama umeruhusiwa kwenda kufanya kazi kenya bila working permit bado vigezo vitazingatiwa lazima utakuwa na utambulisho wako wa wewe ni Nani? Na sijaona sehemu wakisema ukanunue ardhi huko na wao pia siamini Kama wataruhusiwa kuja kununua ardhi huku, hayo ni mambo ya mahusiano ya kibiashara zaidi Ili kuchangamsha akili zetu na kuondoa uvivu wa watanzania na tunaogopa wasije Ili tuzidi kulala, wewe ukiwa na hela yako kenya ni sehemu ya kwenda kujifunza practical ya utengenezaji wa vitu au kuongeza thamani malighafi tulizonazo sasa hizo working permit huoni zitakukwamisha? Angalia wenye mitaji wanavyo copy bidhaa kenya na kuzitengeneza hapa na sasa hivi tunawaita mamilionea, Sabuni za miche na unga, maziwa, viungo na jinsi ya kupaki, hebu twendeni kenya tukachue ujuzi tumepata hiyo nafasi, hata wao wakija watakuja na hela Kama ni nyumba watalipa kodi kwani watakuja kukaa huku bure? Na vigezo na mashariti vitazingatiwa huwezi kuambiwa ruhusa kufanya kazi wewe ukakimbilia kununua kiwanja.
Jitahidi uwezo wako wa kuona mbali! Tunaozungumza haya tumeishi Kenya na tunaijua Kenya!! Unyang'au Kenya ni sifa ya kujivunia wakati undugu Tanzania ni sifa ya kujivunia! Kwa mentality ya undugu ya Tanzania huwezi kutoboa Kenya! Tumetofautiana sana!! Hakuna fursa za kumfaa mtanzania wa kawaida Kenya! Kwa mfano graduate wa Tanzania hawezi kupambania maisha Kenya kwa kuanza na zero!! Lakini mkenya anaweza kuanza na zero hapa Tz na akafanikiwa! Hatujisifu watanzania kuwa hivyo lakini ndivyo ilivyo!
 
Kuna haja ya kutilia mashaka uwezo wa akili yako. Kumtambua mwenye akili na asiye na akili, kunahitaji kiwango fulani cha akili.

Kwa kipimo chochote kilichosahihi, Tanzania haikuwahi kuwa na kiongozi mbaya wa kiwango cha marehemu. Kwa namna alivyokuwa akitenda, hakustahili kuwa Rais. Mungu amsamehe kwa maovu mengi aliyoyatenda dhidi ya Taifa na dhidi ya watanzania wenzake.
Tafadhali!! You are going too far! Heshima kwa kiongozi yeyote yule ni ya lazima! Napata shida kuamini kama wewe ni mtanzania!
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
Akili fupi hii
 
Mama is too rush, yaani kama watu wanabauguana kwa ukabila ndio wasitubague Watanzania
 
Frankly, Kenya ina majirani wangapi? Why always Tanzania! Try with Somalia, Ethiopia, South Sudan, or Uganda. Mulijaribu Somalia, nothing! Mulijaribu Ethiopia, nothing! Mukajaribu Uganda, nothing! South Sudan mumewasaidia kuficha pesa za wizi. Politics aside, Kenya is a bad neighbour.
Mimi napendekeza wawaalike was wasomali kufanya kazi kenya bila kibali!! Na Waethiopia! Ndio wenye shida ya kutafuta kazi! Wengi wanakimbilia nchi za nje wakati jirani yao Kenya ana ukarimu mkubwa wa kukaribisha majirani wafanye kazi bila vibali!
 
Tatizo kubwa ni sisi watanzani hatutaki kuchangamkia fursa na badala yake tunajijaza hofo.
Binafsi nikimwangalia mtu mmoja mmoja kati ya Mtanzania na Mkenya (Educationally, Financially, civilisation ) hapo nawaona Watanzania wakiongoza.

Fursa kubwa ipo kwa Watanzania. Tatizo la watanzania ni kutokujiamini, wamejengewa hofu, hawapendi kusafiri, na vyote hivyo havipo kwa bahati mbaya bali vimejengwa na wanasiasa ili watanzania wasijielewe, wasiweze kuhoji mambo yao.
Mama Samia ameona sasa ni muda muafaka Kwa watanzani kufunguka kiakili.

Kwama tunawaogopa Wakenya nani tutaweza shindana naye?

Ni nini unachomiliki kwa sasa unahofia Kenyaatakunyang'anya?
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
Mama sijui ana washauri au kaamua liwalo na liwe...
Soon atawaambia wakenya wake chukua ardhi tz kama wana uwezo...
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
Mkuu hongera kwa kuona mbali, usingizi tunaolazimishwa kulala mchana utatutokea puani usiku wa manane, tutakapokosa usingizi, Swali la kujiuliza kwanini Uganda na Kenya waharakishe kukaa mezani na mama Samia.?
 
Tatizo kubwa ni sisi watanzani hatutaki kuchangamkia fursa na badala yake tunajijaza hofo.
Binafsi nikimwangalia mtu mmoja mmoja kati ya Mtanzania na Mkenya (Educationally, Financially, civilisation ) hapo nawaona Watanzania wakiongoza.

Fursa kubwa ipo kwa Watanzania. Tatizo la watanzania ni kutokujiamini, wamejengewa hofu, hawapendi kusafiri, na vyote hivyo havipo kwa bahati mbaya bali vimejengwa na wanasiasa ili watanzania wasijielewe, wasiweze kuhoji mambo yao.
Mama Samia ameona sasa ni muda muafaka Kwa watanzani kufunguka kiakili.

Kwama tunawaogopa Wakenya nani tutaweza shindana naye?

Ni nini unachomiliki kwa sasa unahofia Kenyaatakunyang'anya?
Achana na mawazo kama hayo.
Umewahi kujiuliza watanzania wanavyoonekana ktk nchi zingine jirani zetu? Nenda DRC, Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Mozambique, Uganda na hata comoro. Au vuka hadi Namibia na S. Africa. Kote huko tuna heshima yetu na hata waasi wa DRC hawana shida na TZ. Jiulize mara ya pili, kwa nini Kenya tu ndo inaleta dhalau kwetu wanatafuta nini wanachoshindwa kukipata kwa majirani zao; Somalia, Ethiopia, Uganda na S. Sudan?
 
Frankly, Kenya ina majirani wangapi? Why always Tanzania! Try with Somalia, Ethiopia, South Sudan, or Uganda. Mulijaribu Somalia, nothing! Mulijaribu Ethiopia, nothing! Mukajaribu Uganda, nothing! South Sudan mumewasaidia kuficha pesa za wizi. Politics aside, Kenya is a bad neighbour.
Mh. Samia amenena vizuri kuhusu watu ka nyinyi, wachochezi wa maendeleo, mlio pande zote mbili. Hakuna jambo jema mlionalo, porojo tu zisizo na faida kwa jamii. KE iwe jirani mwema au la, haitakusaidia wewe binafsi. Fanya kazi yako, saidia familia yako na jirani, mambo ya siasa hayataleta unga wa sembe kwako au kwangu. Amani na umoja ndio muhimu kwa pande zote mbili.
 
That is Kenyan style, not TZ style! Sisi tunaangalia zaidi ya familia, bhana! Kenya ni familia. Ndo maana kila siku ni mashindano ya wezi tu.
 
Kuna maamuzi ambayo kihistoria unajua tu huo ni mtego mbaya sana! Hatuhitaji ruhusa kama hiyo ambayo ni nadharia tu! Kenya Mkikuyu hawezi kuajiliwa na Mluo. Mluo naye hawezi kuajiliwa na Mkikuyu. Ni hivyo hivyo kwa makabila mengine. Maana yake, hakuna ajira kwa M-TZ, labda kama ni kuzoa uchafu.

Wakenya wanahofia TZ kiasi kwamba hawataki hata apewe ajira za ofisi za UN ambazo siyo za Serikali yao. Mama Tibaijuka anaelewa alivyokuwa anapigwa vita na Wakenya. Wako tayari nafasi ichukuliwe na mtu wa nje ya EAC kuliko Mtanzania.

Mtego huu uliwahi letwa hapa kwenye suala la ardhi eti waruhusiwe kumiliki ardhi TZ na Watanzania waruhusiwe kumiliki ardhi Kenya. Ilishindikana maana TZ tulijua hakuna uwezekanao wa m-TZ kumiliki ardhi Kenya.

Rais epuka mtego huo usio na faida kwa Tanzania.
Rostam azizi amewapa makavu laivu,2017 aliongea na na Mhe Rais Uhuru Kenyata,kuhusu kuwekeza kwenye mradi wa gas wa dola millioni 190!!akafanyiwa figisu mpaka leo hajapewa jibu.
Na kwa ufupi tu,makampuni Mengi yanayokuja kuwekeza TZ kutokea Kenya,sio makampuni ya wazawa wa kenya,ni kampuni za Ulaya zimeweka Makao makuu kenya zikajitanua na kuja TZ
 
Mama samia akae mbali na kenyata, huyo sio mtu mzuri,

Agenda zote za kuibomoa Afrika Mashariki toka kwa mabeberu zinapitia kwake
 
Kuna haja ya kutilia mashaka uwezo wa akili yako. Kumtambua mwenye akili na asiye na akili, kunahitaji kiwango fulani cha akili.

Kwa kipimo chochote kilichosahihi, Tanzania haikuwahi kuwa na kiongozi mbaya wa kiwango cha marehemu. Kwa namna alivyokuwa akitenda, hakustahili kuwa Rais. Mungu amsamehe kwa maovu mengi aliyoyatenda dhidi ya Taifa na dhidi ya watanzania wenzake.
Wewe ndo huna akili, muda mfupi kanyoosha nchi maendeleo yanaonekana afu wewe unaongea ujinga?

Vyeti feki mnajifariji ila alijuwa kuwanyoosha.kila kichwa hata wazungu walimkubali tho hawawezi kusema. Ile ilikuwa ni chuma ya kweli.

Hakuna kama jpm
 
Achana na mawazo kama hayo.
Umewahi kujiuliza watanzania wanavyoonekana ktk nchi zingine jirani zetu? Nenda DRC, Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Mozambique, Uganda na hata comoro. Au vuka hadi Namibia na S. Africa. Kote huko tuna heshima yetu na hata waasi wa DRC hawana shida na TZ. Jiulize mara ya pili, kwa nini Kenya tu ndo inaleta dhalau kwetu wanatafuta nini wanachoshindwa kukipata kwa majirani zao; Somalia, Ethiopia, Uganda na S. Sudan?
Why Kenya kwetu Tanzania?
Ukweli ni kwamba Kenya haiwezi kuikimbia Tanzania kama inataka kuendelea vivyo hivyo kwa upande wa Tanzania kwa Kenya.

Kwa upande wa Africa Mashariki na kati hizi nchi mbili ndizo zinazomiki Bandari kwa upande wa Bahari ya Hindi, pia Tanzania na Kenya zinashea vitu vingi kama Makabila, Ardhi (Serengeti np) biashara (Mazao na Viwanda) nk. Hizi nchi mbili power yake (Military, economic) hazijaachana sana. Zaidi hizi nchi zinategemeana sana kiuchumi (Tanzania hutegemea sana viwanda vya Kenya, Pia kenya hutegemea sana mazao ya biashara yanayozalishwa toka Tanzania)

Sasa hapo ni mjinga tu anayedhani kuwa kuna yeyote atakayefaidika pale hizi nchi mbili zitakapo tofautiana.
 
Kweli lakini jirani anafanya sabotage nyingi kila wakati awe juu yetu. tukiwa juu yake anaona ni mkosi. Si uliona vurugu alizofanya wakati wa bomba la mafuta ya Hoima? Huyo ni jirani mwema kweli?
 
Upo sahihi na hapo ndipo tunatakiwa kuwa makini. Ukweli ni kwamba hakuna nchi inayotaka kupitwa kimaendeleo na nchi ingine. Ila wahenga walisema "Mchawi mpe mwanao akulelee "

USA na China zinaupinzani Mkali sana kiuchumi lakini USA ndio nchi yenye uwekezaji mkubwa China especially kwenye upande wa viwanda.
Leo hii ukimwambia USA avifunge viwanda vyake china hatokuelewa, pia China ukimwambia aviondoe viwanda vya USA vilivyoko nchini mwake hatokuelewa sababu hapo kuna win win situation, yani kila mmoja anaangalia ni nini anakipata na sio ni nini mwenzake anakipata.

Kuna Shida gani kama ushirikiano wetu na Kenya itaonekana Kenya ndio mfaidika mkubwa japo sisi hatupotezi chochote na pia tunapata faida ya kutosha japo sio ya kufuru kama atakayoipata mshirika mwenzetu?
 
Back
Top Bottom