Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, hakuna hiyo sasa

Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, hakuna hiyo sasa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, kila kitu bure, kila kitu beiwauree, hakuna hiyo sasa. Tulipeni ili miradi tuweze kuitunza. Sawa ndugu zangu!

Pia Rais Samia ameongelea miradi ambapo amesema katika miaka miwili aliyokabidhiwa madaraka hakuna mradi uliosimama ambapo mengine imezinduliwa na mingine inaendelea.

Awali mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo alitoa kilio cha wakazi wa Arusha kulalamikia bili kubwa za maji na kumuomba Rais Samia aiagize wizara ya maji iwapelekee mita kama za LUKU na mtu akitaka maji ya 10,000 anaweka anatumia mpaka iishe.

Arusha

 
Tunalipa tozo, tunalipa kodi unasemaje tumezoea bure? Au ni huduma gani hiyo tunayotaka iwe bure? Hatutaki huduma za bure tunataka huduma ziendanazo na kodi/tozo tunazolipa. Wewe ni miongoni mwa watanzania wa chache mnaopata huduma za Msingi BURE kupitia kodi zetu usidhani iko hivyo kwa kila Mtanzania.
 
Tunalipa tozo, tunalipa kodi unasemaje tumezoea bure? Au ni huduma gani hiyo tunayotaka iwe bure??? Hatutaki huduma za bure tunataka huduma ziendanazo na kodi/tozo tunazolipa. Wewe ni miongoni mwa watanzania wa chache mnaopata huduma za Msingi BURE kupitia kodi zetu usidhani iko hivyo kwa kila mtanzania
Yeye hajui bei ya kitu chochote kila kitu ni bure kama ilivyo kwa wazanzibar wenzake
 
Back
Top Bottom