Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, hakuna hiyo sasa

Mi nadhani wanajisema wao viongozi ombaomba.
Wamezoea burebure hadi wameuza utu wetu kwaajili ya misaada
 
Ipi miradi inayoendelezwa? Miradi gani iliyozinduliwa?. Wanamdanganya au na yeye yumo?. Kitu gani WaTz wamezoea bure? Maana kwenye uongozi wake ndio akina Mwigulu wanatunatoza kila kitu. Wanatamani hata pumzi nayo watoe wao
 
Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, kila kitu bure, kila kitu beiwauree, hakuna hiyo sasa. Tulipeni ili miradi tuweze kuitunza. Sawa ndugu zangu!

Pia Rais Samia ameongelea miradi ambapo amesema katika miaka miwili aliyokabidhiwa madaraka hakuna mradi uliosimama ambapo mengine imezinduliwa na mingine inaendelea.

Awali mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo alitoa kilio cha wakazi wa Arusha kulalamikia bili kubwa za maji na kumuomba Rais Samia aiagize wizara ya maji iwapelekee mita kama za LUKU na mtu akitaka maji ya 10,000 anaweka anatumia mpaka iishe.

Arusha

Kuusu suala la bili ya maji Rais Samia Suluhu amesema serikali inamkakati wa kuondoa tatizo hilo “Tunakuja na suluhu ya kutatua tatizo [maji] tunachotaka ni kwamba mita za maji za kununua, unafungiwa mita yako unanunua maji kwa mita, unacholipa ndiyo huduma utakayopata, pesa yako ikikatika na maji yanakatika. Hiyo itakuwa haina malalamiko.” -Rais Samia Suluhu
 
Ni kipi cha bure ambacho watanzania tulikuwa tukikipata kabla yake yeye?

Yeye Rais ndie anaependa vya bure!
Yeye Rais ndie mtafuta vya Dezo!

Anayetembea Duniani akiombaomba,huku akuacha utajiri wetu wa Raslimali zikiibwa ni nani kama sio yeye?

Kwa hiyo Rais ameamua kutusimanga!

Kwa sababu yeye tayari ameushawekeza vya kutosha kutokana na jiyo mokataba ya Siri?

Kwa sababu yeye tayari anao uhakika wa kiinua mgongo cha mshahara 80% mpaka kufa kwake!

Haya bhanaa!
 
Akawahutubie Wazanzibari wenzake. Hamna lolote huyu mama ananena lenye uzito. Tanesco wanakata umeme kila siku wakiamua na bila taarifa wala sababu.. Ni wazi hawataki tuanze kuhoji. Wanatupotezea kihivyo bila taarifa na sababu ya kukata umeme. Huo umeme tumelipia. Akemee hilo.
 
Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, kila kitu bure, kila kitu beiwauree, hakuna hiyo sasa. Tulipeni ili miradi tuweze kuitunza. Sawa ndugu zangu!

Pia Rais Samia ameongelea miradi ambapo amesema katika miaka miwili aliyokabidhiwa madaraka hakuna mradi uliosimama ambapo mengine imezinduliwa na mingine inaendelea.

Awali mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo alitoa kilio cha wakazi wa Arusha kulalamikia bili kubwa za maji na kumuomba Rais Samia aiagize wizara ya maji iwapelekee mita kama za LUKU na mtu akitaka maji ya 10,000 anaweka anatumia mpaka iishe.

Arusha

Hatari.
 
Ni muda muafaka sasa zenji walipe madeni ya bili ya tanesco kuliko kusubiri msamaha wa raisi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom