Rais Samia kwa sasa anatafuta kuvunja rekodi duniani ya kuzurura na kundi kubwa la watu kwenye mataifa mengine. Safari yake ya India, aliteua watu wa kuzurura nao wapatao 100, wote wakitumia kodi za Watanzania, walio wengi wakiishi kwenye umaskini kiasi hata cha kushindwa kuhudhuria hata baadhi ya misiba ya ndugu zao kwa kukosa nauli. Lakini kodi yao, kiongozi wao hana machungu nayo, anaamua kuitumbua kwa starehe pamoja na wale aliowateua kwa wakati husika. Miongoni mwa wazurulaji ni watoto wake, wasanii, n.k watu ambao haiingii akilini kutumia kodi za masikini kuambatana nao!
Sijui kiongozi kwa kuzurura huko nje na kundi kubwa la watu, anataka kutatua nini. Labda kwa sababu watu wamekuwa wakimlaumu kwa safari zake zisizo na tija, sasa ameamua kwenda na watu wengi, kuzurura nao, kutumbua pesa ya umma, kula vinono na starehe mbalimbali, ili hawa watu baada ya kuonjeshwa starehe zote huko nje, aone kama baada ya kurudi wataendelea kusema kuwa kuzurura nje ni kubaya. Au watasifia kuzurura kwenye mataifa mengine ili waendelee kukumbukwa kwenye starehe hizo za kuzurura kwa gharama ya wananchi.