Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Ahsante raisi kwa kujali.
 
Jpm hakuwa anajali kulipotokea maafa.
Hapana ndugu,
Alijali sana,isipokuwa kuna baadhi ya watu hakumwelewa,walikuwa na usiasa zaidi kuliko uhalisia,hata hivyo, kujali kwake kuliwafanya watendaji wake kuwajibika usiku na mchana, tofauti na awamu hii yenye laana, kiongozi anathubutu kusema hadharani,''sasa ni usiku sana,tusitishe zoezi la uokoaji, tutaendelea tena asubuhi ''bila kujali kuwa sekunde/dakika chache baadae zinaweza kuleta matokeo gani kwa mhanga/wahanga ambao ungeweza kuwaokoa!
Ni fedheha sana.
 
Jitahidi kuficha upuuzi wako na hao ccm wenzako.Unatuonyesha picha na taarifa kuwa hao ccm walienda eneo la tukio,kisha wamekaa na kupiga picha ya pamoja,hebu tuambie uwepo wao ulikuwa na tija gani kwenye zoezi la uokoaji?

Kipindi mz.Lowasa alipokuwa Waziri Mkuu,jengo la chang'ombe village [keko]lilianguka,Mz.Lowasa alisimamia zoezi la uokoaji pamoja na wahusika wa hilo jengo kuwajibishwa, tofauti na hawa jamaa zako walienda kupiga picha ya pamoja ili tuone kuwa walikuwepo hapo,,Hivi hamna aibu hata kidogo?Tuondoleeni upumbavu wenu.
 

Mama unatoa bilioni 100 kwa polisi kununua washawasha za uchaguzi na unatoka milioni 300 mpaka 400 kununua magari ya wakurugenzi wa wilaya wanao engua wagombea. Lakini huwezi kutoa pesa za kununua vifaa vya uokoaji. Hakuna mtu anafukuzwa TZ hata watu wakifa siku hizi. Ripoti unazoomba ni fake kila siku unaomba ripoti fake ambazo hazitoki na hazitatoka. Mnajali chama, ndugu zenu na marafiki . Wananchi mnawajali ili tu wawaweseshe kuendelea kuiba na kujinufaisha nyie na ndugu zenu. Wananchi wamekuwa mbumbumbu hawawezi hata kulalamika tena kama vile wafanyakazi wenu na sio nyie wafanyakazi wao. Hii nchi ni Mungu tu ndiyo anaeeza kuiokoa kwasasa na tukiweka imani atafanya hivyo
 
Inashangaza kidogo rais anahutubua taifa lake akiwa nje ya taifa lake.
Ni kheri angekaa kimya tu au angemwambia dr mpango atoe hiyo taarifa .
Tuna Rais ambaye hajali ila eti anajifanya anajali
 
hebu tuambie uwepo wao ulikuwa na tija gani kwenye zoezi la uokoaji?
Kwa sababu msingi wa hoja zote hizi ni chuki, swali hili hili lingeulizwa pia kama kama angeghairisha safari na kwenda pale. Watu wana agenda zao bwana........
 
Inashangaza kidogo rais anahutubua taifa lake akiwa nje ya taifa lake.
Ni kheri angekaa kimya tu au angemwambia dr mpango atoe hiyo taarifa .
Tuna Rais ambaye hajali ila eti anajifanya anajali
Hivi ndivyo uwezo wa chadema wa kufikiri ulipofikia.
Acha mbowe aendelee tu kujichotea mabilioni ya ruzuku
 
Yaan mama umeeleweka 100% kweli ww ni mfariji mkuu
 
Mama huku nyumbani tumepata msiba mzito! Na wewe umetutelekeza ukijua hatuna baba. Mungu atakulipa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…