bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,794
- 7,551
Ongezeko la bei za bidhaa linatokea dunia nzima siyo hapa kwetu tu. Au huna mitandao umeishiwa bando?Huyu mama akilazimisha kubakia madarakani hiyo 2025, basi mchele utauzwa elfu 6 kwa kilo! Na mafuta ya petrol na dizeli lita itakuwa elfu 6 pia! Vifaa vya ujenzi ndiyo kabisaa!! Vitaendelea kupanda mara dufu.
Nitafurahi kama atakaa pembeni.
Rais kuwa taasisi haina maana azungukwe na wajinga na kupokea ushauri wao, ndio maana alimtaka mwenye exposure licha ya kuwa taasisi.Rais ni taasisi,hasa na idara za usalama wa taifa,kwamba kote huko hakuna mwenye uzoefu na exposure kumzidi mulamula!!!..ushauri si sharti ukubaliwe,na Waziri hapaswi kuwa kinyume na baraza la mawaziri hadharani
Mungu hampiganii mtu yoyote. Unajipigania mwenyewe. Ulishapewa akili na maarifa. Huwezi au kiongozi hawezi kufanya mambo ya kijinga halafu ategemee Mungu kumpigania. Au unafikiri Mungu ni kama sisi tunavyoona viongozi ni kama watu wanaostahili heshima na haki zaidi kuliko binadamu wengine? Kwa Mungu kila mtu yuko sawa.Kwa maombi yetu watanzania Tunaamini Mwenyezi Mungu atamlinda na kumpigania mh Rais wetu mpendwa wakati wote ili aendelee kututumikia watanzania
Urais ni nini? Ni mtu mmoja ama taasisi (Office of the President)?Unataka raisi maamuzi yake yasiheshimiwe?
Hali ya unga wa mahindi kuuzwa 2000 kwa kilo na mchele 3200 kwa mwezi huu wa oktoba sijui Januari bei itakuwaje. Wajanja wameshanunua hayo magunia ya kilo mia kwa 120000 mpaka 140000 wakingojea kutugonga.Iangaliwe namna ya kuthibiti. SIELEWI HALI ITAKUWAJE. Hawa wajanja hata chakula cha akiba kikifunguliwa wanaweza kununua na kupeleka huko nje.Hatogombea, usiumize KICHWA.
Una uhakika sababu ya hilo ongezeko ni la dunia nzima? Ile tozo yenu mliyo ianzisha kwenye mafuta, kwa akili yako unadhani haijachangia kupandisha bei ya bidhaa?Ongezeko la bei za bidhaa linatokea dunia nzima siyo hapa kwetu tu. Au huna mitandao umeishiwa bando?
Kwani sababu kuu ya kumtumbua huyo waziri wake ni ipi hasa? Umeshawahi kuzama majini halafu hujui kuogelea? Kama hujawahi, basi huwezi kunielewa nilicho maanisha.Sasa hii ina uhusiano gani na swala la huyo waziri aliyetumbuliwa!!?
Unamaanisha rais kazungukwa na wajinga!!!?..kwamba wewe huku una jicho la kuona wajinga serikalini!!?..mkishiba mna shida Sana!!Rais kuwa taasisi haina maana azungukwe na wajinga na kupokea ushauri wao, ndio maana alimtaka mwenye exposure licha ya kuwa taasisi.
Tatizo ni Rais kumtaka mwenye exposure na uzoefu asiyetumia huo uzoefu wake kazini, anataka awe mjinga wa kupokea ushauri wa baraza la mawaziri sampuli ya kina Mwigulu, wale wasiojua hata wizara zao zinataka nini..
Alfu kweli kairuki s ilisemakana kabisa jiwe alijimilikisha kihalali kabsa ,Hadi akamtundika ujawepezi [emoji23] Kisha akampanga mbelwa china Kaz za kibalozi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kairuki ndani!
Sukuma gang inazidi kutamba!
Mama anachuki na Mulamula
Raisi hapo anakosea, kwani uamuzi wa huyo waziri utakuwa ni ule wa kulazimishwa yaani watokana na kuwa "coersed".Rais Samia akiwaapisha mawaziri leo, Oktoba 3 amesema waziri hatakiwi kusema hakubaliani na maamuzi ya Serikali au kusema kuwa nimeelekezwa hivi ila sikubaliani. Hatakiwi kujitoa bali kuwa sehemu ya maamuzi.
Sijui ni waziri gani aliyesema haya ni maamuzi ya Serikali sio yangu?
Jiwe nasikia amewahi kumkataa mulamula Kisha mam enu akajidai kumkumbatia Sasa mulamula amemuonesha rangi yake halisiNaona exposure inawaponza wasaidizi wa Rais, Rais anataka kila mteule wake afanye vile anavyotaka yeye hata kama hana ujuzi wa jambo husika, hii sio sawa, anakosea.
Mulamula alikuwa na exposure na mambo ya nje toka enzi za JK, na hiyo exposure yake naamini ndio iliyochangia Rais kumpa kile cheo, leo iweje amuondoe yule aliyegoma kuburuzwa kwenye jambo alilo na experience nalo? lililofanya akaaminiwa na kupewa kazi? Rais hajui anachofanya.
Kuwa na wasaidizi maana yake ni kumsaidia Rais, na sio tu kufanya kazi wanazopangiwa, bali hata kwa ushauri pia, hii kauli aliyoitoa Rais itazidi kuzalisha chawa wengi zaidi, wajinga, majeuri, na viburi.
Matokeo yake kina Mwigulu wanazidi kutuburuza na tozo, huku Makamba na Nape na kauli zao za hovyo kila wakati; yeye anataka jambo lolote wakishakaa na kukubaliana serikalini lisipingwe, vyema atambue hata wajinga huwa wana maamuzi yao na yasipoangaliwa mapema yatatuumiza.
Awaache wenye uzoefu wamsaidie, unaweza kuwa na kundi kubwa la wajinga wasiojua chochote kasoro mmoja wao, na kiongozi mzuri anatakiwa kumtambua huyo mmoja.
Wewe unataka yaheshimiwe hata kama ni ya hovyo?Unataka raisi maamuzi yake yasiheshimiwe?
Hawa ndio walikuwa wanaojifanya tozo haiwahusu,fukuza..Rais Samia akiwaapisha mawaziri leo, Oktoba 3 amesema waziri hatakiwi kusema hakubaliani na maamuzi ya Serikali au kusema kuwa nimeelekezwa hivi ila sikubaliani. Hatakiwi kujitoa bali kuwa sehemu ya maamuzi.
Sijui ni waziri gani aliyesema haya ni maamuzi ya Serikali sio yangu?
Hapo umesema sawa. Katika utawala kuna kitu kinaitwa "collective responsibility" ambayo mkikubaliana huwezi kujitoa kwenye maamuzi hayo. Kama unaona unataka kuendelea na msimamo uliyokataliwa na ewnzako inabidi ujiuzulu na kwenda kwenye "public court" kuutetea huo msimamo. Kama uang'ang'ania uongozi huku uklijitenga na maamuzi ya viongozi wako hii sawa na " you want to have your cake and eat too".Waziri halazimiki kutii kila kitu endapo anaona kuna vitu haviko sawa, alipokosea ni kuendelea kubakia madarakani, alipaswa kujiuzulu baada kuona hakuna muafaka. Kusubiri kuondolewa ni kama kuonesha kiburi.
Kama alioomba kujiuzulu rais lazima angetamka ameomba kujiuzulu, maamna hii inampa kinga yeye kuonekana anafukuza fukuza. Mawaziri au niseme viongozi wetu ni vigumu kuchukuwa maamuzi magumu wanapoona wameharibu au mwelekeo wao na wakubawa zao hauendani. Wanag'ang'ania kuendelea kudfanya kazi na msononeko.Unajuaje aliomba kujiuzulu mwenyewe?
Kama hutaki kuyaheshimu maamuzi ya mkubwa wako wa kazi jiuzulu kwanza ndiyo uanze kumchamba na kumpa mipasho ndogondogo.Wewe unataka yaheshimiwe hata kama ni ya hovyo?
Kwani wewe umezuiliwa na Nani kutunza chakula chako na familia yako, au unasubili kuja kulia Lia humu , au unataka nani akutunzie chakula kwa ajili yako na familia yako? Timiza wajibu wakoHali ya unga wa mahindi kuuzwa 2000 kwa kilo na mchele 3200 kwa mwezi huu wa oktoba sijui Januari bei itakuwaje. Wajanja wameshanunua hayo magunia ya kilo mia kwa 120000 mpaka 140000 wakingojea kutugonga.Iangaliwe namna ya kuthibiti. SIELEWI HALI ITAKUWAJE. Hawa wajanja hata chakula cha akiba kikifunguliwa wanaweza kununua na kupeleka huko nje.
Reference : UK chancellor Kwasi Kwateng on U turn on 45p uk tax akichukua full responsibility .Rais Samia akiwaapisha mawaziri leo, Oktoba 3 amesema waziri hatakiwi kusema hakubaliani na maamuzi ya Serikali au kusema kuwa nimeelekezwa hivi ila sikubaliani. Hatakiwi kujitoa bali kuwa sehemu ya maamuzi.
Sijui ni waziri gani aliyesema haya ni maamuzi ya Serikali sio yangu?