Rais Samia: Wenye akili za kawaida ndiyo wananikosoa kusafiri nje

Na hao marais wenye hayo mapesa huwa wanafanya ziara wapi ili kupata hizo pesa?
Watu wao wanafanya kazi kwa bidii,ndiyo hizo iPhone,movies,jinzi nk..serikali inapata Kodi huko,hizo Kodi wanawakopesha nyie au kuwapa misaada
 
ukweli ni kwamba bila kukopa hii miradi hatuwezi kuimaliza kwa hela za ndani.
Tuache mawazo ya kijinga, tumejipanga hela maarufu kama hela za uviko etI tumejengea matundu ya vyoo, wakati huo huo mumeweka makato ya miamala mka sema ni fedha za matundu ya vyoo akili matope kbs
 
Unashangaa nini wakati 98% ya wanaomuunga mkono ni 'Morons' tupu?
Unahitaji fedha kujenga miundo mbinu,project Kama sgr na mnhp haziwezi kuwa financed na Pato la ndani,hizo pesa zipo nje,rais akikaa ndani inasaidia nini!?...yule jamaa yenu aliyekaa ndani alishusha FDI Hadi chini ya 1b$..Sasa FDI ipo $9b
 
Tuache mawazo ya kijinga, tumejipanga hela maarufu kama hela za uviko etI tumejengea matundu ya vyoo, wakati huo huo mumeweka makato ya miamala mka sema ni fedha za matundu ya vyoo akili matope kbs
Matundu ya vyoo yalihitaji kiasi gani Cha pesa na tozo zimepatikana kiasi gani!?..bila Shaka hujui au hukua ukijua mpaka umegugo...mwerevu huongea kwa takwimu
 
Wewe ndiye uwezo wa kufikiri ni chini ya magoti..kwa post yako hii
 
Kwa nini mama asiishi kwenye ndege ili iwe rahisi kusafiri kwenda ngambo kutuletea wanae ma$$$$
 
Matundu ya vyoo yalihitaji kiasi gani Cha pesa na tozo zimepatikana kiasi gani!?..bila Shaka hujui au hukua ukijua mpaka umegugo...mwerevu huongea kwa takwimu
Mulisema mnakusanya bil 60, kwa mwezi, hivyo vyoo viko wapi?
 
Huu uzi umethibitisha kile alichosema Rais, kweli wewe una uwezo mdogo.
 
Kodi na mirabaha? Kuwa serious aisee, hebu taja hapa tunachukua percent ngapi ya mirabaha kwenye madini
4% kweli kabisa unaweza kusema tunapata chochote?
 
[emoji122]
 
Pascal Mayala njoo huku uokoe banda la kuku kuna mtu anamwaga sumu.
 
Umeandika kwa nongwa nyingi na kisiasa zaidi. Umekuja na tafsiri nyepesi sana kulinganisha na ukubwa wa hoja mezani.

SSH ni mkweli siku zote, hakutaka kuleta simulizi za nchi hii ni tajiri sana inayoweza kuwauzia wazungu mitumba!. Kaamua kuwa mkweli katika uongozi wake. Kwamba miradi inayomdai kuimaliza ni mikubwa mno na huwezi kuifanikisha kwa kutegemea pesa za ndani. Trilioni 16 na kumaliza sehemu moja tu ya treni inayokwenda mpaka Kigoma bado hujaweka pesa ya kujenga treni nyingine ambazo na zenyewe ni muhimu pia kiuchumi.
 
Kodi na mirabaha? Kuwa serious aisee, hebu taja hapa tunachukua percent ngapi ya mirabaha kwenye madini
4% kweli kabisa unaweza kusema tunapata chochote?
Unajua mirabaha inavyokokotolewa ? Mirabaha inakokotolewq kutoka kwenye pato ghafi
Yaani kama umechimba madini yà thamani ya milioni 10 kabla hujatoa gharama za uchimbaji na uendeshaji tayari serikali inachukua 4% yaani laki nne

Ukija kutoa gharama ukabakiwa na faida labda ya milioni 2 serikali inachukua tena 30% yaani laki 6

Madini, mafuta na uchimbaji mwingine haufadishi sana nchi za Afrika sababu wanaochimba, wanaohenjua, wenye mitambo ya kuchimba wote ni raia wa kigeni

So wazawa mnaweza?
 
Huenda huelewi au unafanya makusudi. Hebu soma hii comment yako vizuri tena
 
Wana ka msemo kao kuwa ukiwatoza Kodi MATAJIRI unavuruga Uchumi wa Nchi.

Eti maskini ndo HAKI kulipishwa mikopo iliyokopwa wakapewa MATAJIRI kuinua Uchumi!!!!

Mbona Nchi za MABEBERU matajiri na maskini wanalipa Kodi na wanajivunia kulipa Kodi?

Vituo vya mafuta nw hawatoi tena risiti za EFD.

Ukigusa makontena ya wakubwa bandarini unatumbuliwa.

Hivi sie ni WAJAMAA Uchwara au Mabepari Uchwara?
 
Umeulizwa pale juu huko anakoenda kuchukua pesa... Wao huwa wanazitoa kwa kwenda nchi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…