Rais Samia: Wenye akili za kawaida ndiyo wananikosoa kusafiri nje

Kodi yote anakula silent ocean, halafu mnaanza kukuletea maneno ya kejeli, hiyo barabara ya dar mza imejaa matuta matupu, maroli kilasiku yanatoboa boosters
 
Total misconception !!
 
Unazidi kudhihirisha jinsi ulivyo na akili ndogo kama alivyosema SSH..

Unaweza niambia ni ziara ipi Rais ameifanya ikawa ya hasara? Na Je angebakia anazurura na kudanganya watu mikoani angefikisha investment kubwa kama inayoonekana sasa?

Unajua Tzn ni imesima vyema kuliko Nchi karibu zote za hapa Afrika kwamba licha ya changamoto za uchumi wa Dunia ila tumekuwa na nafuu kwenye Kila kitu?

Nchi za jirani hapo Hali ni mbaya sana Sasa sijui kwamba na wao ni kwa vile wanasafiri sana au hapana..

Mwisho ,laiti kama Jiwe angekuwa hai leo hii,Tanzania tungekuwa kama Zimbabwe au Sri Lanka..Kwa miaka ya Jiwe madarakani bidhaa ya sukari iliwahi adimika mara 3,saruji mara 2 na mafuta ya mitambo mara 2 pia.
 
lakini ulishaanza na umekamilika kwa asilimia kubwa sana kama sioa silimia 90... maana mpaka wanafanya testing. hata ndugai alikuwa anajua hali halisi ya miradi kuwa haiitaji kukopa kopa kila siku

..SGR kipande cha Dar to Moro ndio kimekamilika kwa asilimia 90.

..SGR ni zaidi ya km 1800 na kipande cha Dar Moro ni km 300+.

..Zaidi, SGR imelenga kusafirisha shehena kubwa za nchi majirani.

..Bila reli hiyo kufika mpakani na nchi jirani, au Isaka Dry Port, haitaweza kukidhi malengo iliyowekewa.
 
Kwa akili yako kodi za nchi hii zinalipwa na watu gani? Machinga na mama nitilie? Bodaboda? Au wakulima huko vijijini?
Unajua makampuni kama TBL, Vidacom, Metl, Azam wanalipa kodi kiasi gani?
 
Kama wapi? Utalii hatupati kodi na fedha za kigeni? Madini hatupati kodi na mirabaha, kuwa wanachimba bure? Uvuvi hatupati mapato? Japo ni madogo sababu hakuna uwekezaji..

..tatizo letu ni kwamba tunadharau kilimo, ufugaji, na uvuvi.

..kwa mfano, fedha tulizofuja kununua midege toka kwa mabeberu zingeweza kufanya transformation kubwa kama zingewekezwa kwenye kilimo.

..katika safari zote za Raisi za kutafuta wawekezaji, sijasikia kama amepatikana muwekezaji ktk kilimo, au viwanda, ambaye analeta fedha sawa, au kuzidi, zile tulizowekeza kwenye viwanda vya mabeberu vya kutengeneza ndege.

..Majuzi tulisikia habari za Uganda kutuuzia sukari. Hii ni aibu kwasababu viwanda vya sukari vya Tz vilikuwa operational wakati ambapo viwanda vya Uganda vilikuwa vimekufa. Sasa Uganda wameweza kufufua viwanda vyao na sasa wanaweza hata ku export ktk soko letu.

..Jambo lingine la kusikitisha na kuonyesha uzembe wa miaka mingi wa serikali zetu ni kile kilichoonekana ktk ziara ya Waziri wetu wa Kilimo kwenda Uganda kujifunza kuhusu zao la Chikichi.

..Nchi yetu haiwezi kuendelea bila Watz kuongeza uzalishaji ktk kilimo ambacho kinaajiri asilimia kubwa ya wananchi wetu.
 
Wewe ndio huelewi
Madini inachangia 7% tu ya GDP yetu, Botswana wao madini 35% ya GDP. Alafu sisi tunawazidi Botswana kwa uzalishaji madini.

Ingekua hata 20% au 30%, leo hii GDP yetu ingekua sawa au zaidi ya kenya
 
Madini inachangia 7% tu ya GDP yetu, Botswana wao madini 35% ya GDP. Alafu sisi tunawazidi Botswana kwa uzalishaji madini.

Ingekua hata 20% au 30%, leo hii GDP yetu ingekua sawa au zaidi ya kenya

..Watz tuko milioni 50++.

..Botswana wako milioni 2 [ sina uhakika].

..kutokana na idadi yao ndogo lazima Botswana watafaidi zaidi madini yao kulinganisha na Tz.

..Hata ukiangalia mafuta ya Nigeria vs ya nchi za Kiarabu.

..Ni kweli kuna rushwa na ubadhirifu Nigeria, lakini kwa idadi kubwa ya watu wao sio rahisi kuona manufaa ya mafuta ukilinganisha na Saudia, Kuwait, etc.

..Kwa hapa Tanzania hatuwezi kuwakwepa WAKULIMA kama tunataka kujikwamua kiuchumi.
 
Hii ni justification ya tunachopata tunastahili?
 
Huo uwingi Wenu usio na faida mlilazimishwa mzaane hovyo kama Sungura na Panya wakati mkijua hamna Akili?
 
Hawakutegemea Samia awe rais na hatukuona rais akifariki madarakani tangu uhuru hivyo maneno mengi wanayoongea ni kuchanganyikiwa.

Hawa ni wale waliokuwa wanafaidika na awamu ya JPM hawakuiona leo hii yenye mabadiliko ya uongozi kuanzia juu kabisa pale ikulu.

Kelele na malalamiko yao ni kwa SSH ambaye ni mrithi wa JPM kwa mujibu wa katiba sio kwa kuingizwa na watu fulani. Wanaishi na maumivu ya moyo yasiyoweza kutibika mahospitalini wala kwa waganga wa kienyeji. Pole inawahusu.
 
Madini inachangia 7% tu ya GDP yetu, Botswana wao madini 35% ya GDP. Alafu sisi tunawazidi Botswana kwa uzalishaji madini.

Ingekua hata 20% au 30%, leo hii GDP yetu ingekua sawa au zaidi ya kenya
Mkuu unajua GDP ya Botswana ni ngapi? Ni 15 Bilion USD, Tanzania ni 62 Bilioni USD,
Sijui hicho kipimo cha kuwa madini yanachangia 7% ya gdp umetoa wapi ila mimi takwimu ninazijua madini yanachangia 10% ya gdp, na inaonyesha 35% ya 15 ni ndogo kuliko na 10% ya 62
 
Pesa zitatafutwa sana ila bila kudhibiti matumizi hakuna kitakachobadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…