Rais Samia yupo Afrika Kusini, kapotezea kumbukizi ya Hayati Magufuli?

Rais Samia yupo Afrika Kusini, kapotezea kumbukizi ya Hayati Magufuli?

Kwani kuna ubaya gani kwake kuwepo kwenye maadhimisho ya mara moja kwa mwaka?

Huko Afrika Kusini ameenda kufungua nchi au kuifunga?
Maadhimisho gani hayo mnayozungumzia!!

Tanzania zipo kumbukumbu mbili tunza waasisi wa Taifa hili, Karume na Nyerere!!

Hiyo nyingine ni kimbukumbu ya Wasukuma, siyo ya Taifa, haimhusu Rais wa nchi!!
 
Kesho ni miaka miwili ya kumbukizi ya hayati Magufuli.

Rais Samia yupo nje ya nchi, je amekwepa kwa makusudi au bahati mbaya kwenye kumbukizi ya mtangulizi wake?

Ikumbukwe mwaka jana waliadhimisha Rais Samia pamoja na Kaguta Museveni huko Chato. Mwaka huu kulikoni?
Kesho asubuhi Rais atakuwa amesharudi Tz. Huenda akawepo huko Chato kama kuna shughuli ya kitaifa ya kumbukumbu ya mwendazake.
 
Akae huko huko hata asiporudi poa tu.

Maana hakuna faida ya yeye kuwepo au kutowepo.

Msoto wa maisha uko pale pale.

Nafuu ya maisha ipo kwake , familia yake na chawa wake.
 
Kwani lazima iwe kila mwaka?
Na kumbukumbu ya Mkapa je?mbona hamuulizi??
Ya mkapa inafanyika mkuu tena katika viwangi vikubwa sana nadhani kuliko marais wote kupitia ile BM Foundation in two or three days of discussions.
 
Kakwepeshwa na mshika rimoti. Si unajua ye king'amuzi tu. Hana alijualo zumbukuku ulimwengu upo huku.
Si mlisema sijui system inaandaa RAIS mara sijui CCM Ina succession management kuliko upinzani mara sijui chuo Cha viongozi ni CCM. Sasa kivipi Tena unayemuita zumbukuku amekua Rais? Kumbe hakuna Cha system Wala succession management.

Urais wa Samia umewaumbua wanafiki wote. Yukwapi Polepole aliyesema ana master plan ya CCM kutawala Hadi 2075!! 🤣🤣🤣
 
Kesho Machi 17 ni miaka miwili ya kumbukizi ya hayati Magufuli.

Rais Samia yupo nje ya nchi, je amekwepa kwa makusudi au bahati mbaya kwenye kumbukizi ya mtangulizi wake?

Ikumbukwe mwaka jana waliadhimisha Rais Samia pamoja na Kaguta Museveni huko Chato. Mwaka huu kulikoni?
Magufuli ni nani nchi hii mpaka awe na kumbukizi. Unawashwa?
 
Back
Top Bottom