Itakuwa nimewagusa wahusika wakwapuaji wa hela na michango ya wananchi kichama. na unajua panapo wengi hapakosekani jambo ,na ninayoyajua nyinyi hamuyajui na hata kuelewa mnakuwa wagumu,huenda wengi wenu ni wahusika wa matayarisho a maandamano na mikutano hivyo bajeti mnaielewa.
je mmewahi kuhoji ni hela kiasi gani inatumiwa na viongozi wa Chadema kutayarisha mkutano mmoja tu na kila kiongozi anaehudhuria posho yake ni shilingi ngapi,hela inayotumika kukodi vikundi na vinginetele vya hapa na pale ?
najua ukweli unauma na viongozi wa Chadema ni wafaidika nambari moja na ndio ukaona kila ziku wanazua mikutano.
mfuko ukianza kukauka utawasikia wanaidai serikali mafao ya Chama cha siasa ,ujuwe hapo wameshakwapua na kumaliza hazina ya chama,jamani ukweli usemwe .viongozi wa Chadema mnakifilisi chama kiaina na maandamano yasio kwisha.
Ukiangalia mikutano haina faida zaidi ya uchinganish kwa wananchi na serikali yao ,na kujaza uongo usio na kichwa wala miguu.
Na hili ni kuwa tumezoea kutawaliwa tokea huko mwanzo hata kabla ya ukoloni,tunahitaji mwendo kasi wa Kimagufuli ,fungia fungi mambo yote ya kisiasa mpaka utakapotangazwa uchaguzi na ukimaliza ,kifungo kinaendelea.
Kwani ruhusa na uhuru aliotoa Raisi Samia unatumiwa vibaya tena bila ya heshima wala tahadhari,mipaka inavukwa ,sababu tu tumezoea kutawaliwa na sheria zinazozibwa mianya,tunawaona sasa Chadema hawana adabu kabisa.
Yote wamepewa uhuru na wanashindwa kuutumia kwa heshima na taadhima,bado hatujakuwa watu wa kupewa uhuru kwani hatujui kuutumia.
Ni kheri Serikali inatumia sheria za utawala badala ya uongozi ,asili yetu ni kutawaliwa na si kuongozana tokea enzi za machifu,wao wakitawala na amri kwanza.