Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Pamoja na hayo, sioni Rwanda inaishindaje DRC wakipigana sasa hivi. Nasisitiza endapo hakuna external influence kwa yeyote
Mpaka Sasa Rwanda imeshaishinda Drc, kitendo cha Drc kuwashindwa M23 ni udhaifu tayari.....Rwanda ya Sasa ni imara mno kuliko ya miaka ile na imekuwa na nguvu Sana kwenye hilo eneo.
 
nini lengo kuu la m23?
Wanaikumbusha serikali ya Drc (hasa Tshekedi ) kutopuuza umuhimu wa Rwanda kwenye eneo hilo.

Huo ni mkono wa nchi jirani kujaribu kuishinikiza Drc kutimiza matakwa yao, kitendo cha Drc kuzialika Burundi na Uganda kupambana na waasi wao waliopo huko na kuitenga Rwanda kumechangia hili.

zitto junior JokaKuu Count Capone
 
means hawana lengo la kuitoa serikali ya kinshansa,zaidi ya kuzuia juhudi za fdlr
 
Kijeshi CONGO ina nguvu kuliko rwanda !! lakini kimbinu Rwanda ameizidi DRC mbali sana. So kama ni vita ya ana kwa ana Rwanda haiwezi kufua dafu kwa DRC !! ila kwa vita za siku izi hazipo hivo sikuizi vita zake ni za kuchekeana machoni na kupigana kimya kimya ,kupigana kimifumo na kupandikiziana magaidi na waasi kitu ambacho drc haijabobea!!

rwanda ina marafiki wengi nje kuliko DRC!!
Drc inashindwa hata kujihusisha na nchi marafiki kupata msaada kijeshi na kitechnologia
 
means hawana lengo la kuitoa serikali ya kinshansa,zaidi ya kuzuia juhudi za fdlr
Naweza kukubaliana na wewe kwa sehemu tu, ila unadhani fdlr ina uwezo wowote wa kuiangusha serikali ya Kagame ?...

Huoni kwa Sasa Fdlr inatumika tu kama sababu ya kuhakikisha 'balance of power' kati ya Rwanda na mahasimu wake wa Kikanda yaani Uganda na Burundi inaendelea kuwepo huko Drc.

Unadhani fdlr ikiondoka huko Drc, Rwanda inaweza kuendeleza ushawishi wake huko Drc hata kuipiku Uganda na Burundi ?

Huoni kama ushirikiano kati ya Burundi, Uganda, Kenya, Tz na Drc ni mzuri mno hata wakaruhusiwa kupeleka askari wao huko, huku Rwanda ikizuiwa huoni hilo jambo ni kitisho na hatari kwa Rwanda?
zitto junior JokaKuu
 
Ndio maana nikasema Rwanda apigane na Congo kwenye vita halisi, na kusiwepo third party. Sioni Rwanda anashindaje vita hiyo
 

..eastern congo isipotawalika rwanda nayo haitakuwa salama.

..pia rwanda iache kuchochea na kufadhili makundi ya waasi wa congo.

..lingine ni suala la DEMOKRASIA Rwanda. Kagame atatawala mpaka lini?
 
hao fdr walishaambiwa km wanaweza wakafanye siasa kigali,huko porini hawashindi ht kwa nn

Nami nakubaliana na wewe,ila chaka analoingia felix ni kuanzisha hivyo vikundi km huo mpango anao
 
Sasa mkuu, Marekani imepigana na Taliban miaka 20, ikapiganana na al Qaeda miaka mingi, ikapigana na wanamgambo na magaidi wengine miaka na miaka. Hatuwezi sema Marekani itashindwa vita na Switzerland kwa kuwa hawajawahi teswa na wahuni.

Nigeria hii inateswa na Boko Haram magaidi, achana na zile suicide missions zao za mabomu nasema ile kubwa na vikosi vya mafunzo, kupiga kambi za jeshi, kumiliki Sambisa forest na kuteka maelfu ya watu humo wakiwemo mamia ya wanafunzi. Mtu akitumia kigezo hicho kudai Nigeria inaweza pigwa na Tanzania kisa inashindwa na Boko Haram ujue hajui kitu kwenye majeshi, hajui kitu kabisa.

Kuteswa na waasi sio kipimo cha jeshi kuwa dhaifu. Nchi za Afrika ambayo ilipambana na usumbufu wa hivyo ni the mighty South Africa ya apartheid pekee kupigana na kina SWAPO kule Angola na kupigana na resistance fighters wa Namibia. Hadi leo Misri ina magaidi pale Sinai na Turkey inasumbuliwa na vikundi vya Wakurdi na nchi hizo mbili hata ujumlishe majeshi ya Afrika Mashariki nzima hayawezi ipiga mojawapo
 
..eastern congo isipotawalika rwanda nayo haitakuwa salama.

..pia rwanda iache kuchochea na kufadhili makundi ya waasi wa congo.

..lingine ni suala la DEMOKRASIA Rwanda. Kagame atatawala mpaka lini?
Rwanda ni ticking bomb, muda wowote Kagame akidondoka ujue ni vita ya utawala. Dalili ya kwanza ya kutambua hilo tuulizane ni nani mrithi wa Kagame aliyeandaliwa mpaka sasa?

Maana kawaida ya totalitarian leaders hawapendi kutaja mrithi kuepuka mapinduzi. Unamjua mkubwa ila second in command mmoja wa uhakika hajulikani, unakuta watu kama watatu wenye influence sawasawa. Sasa kati yao kila mmoja akiamua apambane ndio tunarudi kupokea wakimbizi
 
Jambo la kwanza lazima utofautishe vita baina ya nchi na nchi na vita ya waasi,au vikundi vya kigaidi ambao wana kuwa ndani ya nchini vita ngumu sana kwani huwa wanajificha ndani ya jamii humo humo,na mifano ipo mingi,Kenya,msumbiji,Uganda,Burundi na hata Rwanda,zimeshawahi kukutana na hali hii,na viliwasumbua sana.Na vingi hupotea pale milija ya ufadhiri inapokatwa ,hivyo huwa ni ngumu kujua nani hasa ndiye unayegombana naye,lakini vita ya nchi kwa nchi,hiyo ni rahisi sana kwani adui yako unamfahamu,ni nani.Hao M23 nguvu inatoka Kigari tu,na ndio maana siku hizi lile kundi la ADF,lililokuwa likileta vulugu Rwanda,ni kama halipo tena,baada ya Uganda kuamua kulitokomeza ,na kukosa misaada ya kifedha,u lile la LRA la joseph koni.Ninachokiona mbeleni huko KAGAME,atakuja kuanza kuilaumu EAC,kuwa inampendelea DRC,kwani wao wanapeleka majeshi kulinda mipaka ya DRC,na RWANDA,sasa kama kuna michezo inafanywa na Rwanda ndani ya DRC,itafikia mwisho,na majeshi ya EAC,yapo huko under chapter 6,lakini yanataka ikibidi yapewe majukumu ya under chapter 7(hapo yatakuwa na uwezo wa kushambulia sio kulinda tu wananchi)hao M23 baada ya kudhibitiwa huko mashariki mwa congo,vifaa vitakuwa vinapitia wapi kuwafikia.Na kiuchumi DRC,kila mtu ana muhitaji sana kuliko RWANDA.Na rwanda hawezi kukosana na TZ na Kenya kwa wakati mmoja kwani atapata shida sana kiuchumi.
 
Umejitahidi kujifichia kwenye utanzania lakini imeshindikana.Utawajua tu banyamulenge kwa maandishi yao
Haya anza sasa kumsifia mungu wenu PAKA maana ndiyo kazi muiwezayo
Mkuu Nyamizi wanyamulenge ni wakongoman, Paka ni mnyarwanda na mimi mleta mada ni mtanzania. Kwahiyo tuna utofauti wa utaifa.

Usiniaminishe kuwa kila anaeitetea Congo humu ni mkongomani na anaezungumzia tofauti ni mnyarwanda.

Siku zote mtu anaekupenda ni yule anaekwambia ukweli wa hatari iliyopo mbele yako ili uchukue tahadhari mapema kabla hatari hiyo haijakufikia. Ukiona mtu anaficha kukueleza ukweli wa hatari hiyo wakati anaifahamu huwa huyo sio mwema kwako. Sasa kwahiyo hapa nimekuja kutoa tahadhari kwa raisi wa ndugu zetu wakongomani ili wale vijana wake waliopo humu wamfikishie taarifa mapema kabla hajaingia kichwa kichwa vitani na Rwanda.
 
Lengo la M23 ni kuchukua Goma mida hii washachukua miji ya Kiwanja na Rutshiru na wajongelea ndani zaidi.

Tatizo kubwa n kwamba M23 wazungumza kinywarwanda na hiyo ni sababu kubwa inotumiwa (kwa makusudi na malengo maalum) kuendelea kuchochea mgogoro.

Tayari kelele za kuomba msaada wa Russia zimeanza na ni kama zile kelele za kule Mali na Burkina Faso ambako majeshi ya Ufaransa yameondolewa katika nchi hizo.

Hapa ni wazi kuwa mgogoro wa Ukraine unasababisha vita ya rasilimali kati ya mataifa makubwa kugombea sehemu zenye maliasili ya kutosha.

M23 waulizwe mafunzo, silaha na vifaa vyote vya kivita wazitoa wapi na nini gharama zake na nani azilipa?

Tukipata majibu hapo ndipo twaweza kuja na kusimamia hoja kikamilifu kwamba siku za Tshisekedi zahesabika.
 
M23 waulizwe mafunzo, silaha na vifaa vyote vya kivita wazitoa wapi na nini gharama zake na nani azilipa?
Wanadai wao walikuwa sehemu ya jeshi la Congo ila waliondoka jeshini na silaha zao na kuasi baada ya serikali ya Drc kutotimiza makubaliano baina yao.
 
Wanadai wao walikuwa sehemu ya jeshi la Congo ila waliondoka jeshini na silaha zao na kuasi baada ya serikali ya Drc kutotimiza makubaliano baina yao.
Mkuu, fuatilia hii zipo taarifa kuwa kuna "contractor" wa kuaminika kutoka Western Europe atoa mafunzo na kila kitu kwa M23.

KP ana influence kubwa sana katika Commonwealth kwa sasa na hii inampa access kwa mambo mengi.

Kuna masuala mengi sana yapo nyuma ya pazia ila kwa sasa Tshisekedi atumika tu.

Ila Sultani Makenga hawezi kuondoka jeshini (Congolese Army) na vifaa vyote yakiwemo "armour vehicles" ambayo mida hii yafagia kule Eastern Congo DRC.
 
Mkuu

Proved


Usishangae yapo mambo mengi sana ya kijasusi yaendelea kwa sasa duniani ni mazito sana.
Inawezekana mkuu, ushindi wanaoendelea kuupata M23 dhidi ya jeshi la Drc unashangaza Sana, huenda kuna mkono mzito nyuma yao.
 
Hii ni fedheha kwa nchi kubwa kwa idadi ya watu, raslimali na eneo kama DRC kudharauliwa na ka nchi kadogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…