Rais Uhuru Kenyatta: Wakenya hawapaswi kujilinganisha na mataifa yanayoficha taarifa za COVID-19

Kenyata unaona utaaaaaaamu kutangaza covid19 eh ?

Nashukuru ndugu,jamaa na marafiki zangu wote 100% hakuna aliyeugua wala kufa na covid19 👏

Kama wewe ni muhanga wa covid19 nikupe pole nyingi sana sana
 
Kikubwa nikushinda vita! Taarifa bila kushinda vita ni kazi bure, tafuta namna kumaliza tatizo.
 
Nyie wenye hamuwezi kupata corona endeleeni kujivinjari.
 
We jamaa hata mara moja uwe unakubali kushindwa ndo uungwana sio kila kitu unashupaa, hauonekani mjanja.

Sasa hapa issue ya Lissu inaingiaje kwenye mambo ya kupambana na corona! Ila pia watu kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi wao bila barakoa wala sanitizer haikupi picha kwamba corona haipo Tanzania?

Acha mambo yako bana, stick kwenye mada mkuu kuhamisha gori kila unapotaka kufungwa sio sifa ya kiume
 
Endeleeni kuficha kichwa kwenye mchanga kama mbuni. Wote wanaokufa kuna ripoti ya daktari inayoelezea chanzo cha kifo kwa wahusika so endeleeni kuamini mnachoamini kwetu haina athari.
 
Uliona wamevaa mibarakoa?

Je, hapo Kenya mkiruhusiwa muandamane kama vile si lolisi watamaliza risasi?
 
Lazima aendelee kupima pima tu. Kwa maana mabeberu mwishoni watahitaji retirements ya hizo fedha. Uhuru anapaswa kujua ya kuwa:-

1. Elimu ya namna ya kujikinga na tiba ndiyo jambo kuu. Wawafundishe wananchi jinsi ya kujikinga na lililo la muhimu zaidi ni jinsi ya kufanya kinga yako iimarike. Tanzania walijitahidi kufanya mambo yanayoimarisha kinga na kubadirisha mitindo ya maisha ambayo ni hatarishi. Ndiyo maana wagonjwa ni wachache sana katika mahospitali (considering cases vs serious cases).

2. Kuondoa hofu kwa wananchi ni jambo la msingi katika vita dhidi ya korona.

3. Kupima kwa mtu ambaye hana dalili hata moja ya ugonjwa au kumkamata na kumpima mtu anayetembea zake barabarani kuelekea kwenye shughuli hakuta punguza korona, wala si njia ya kupambana na ugonjwa bali ni kupotea rasilimali tu.

4. Kama unataka kupima kweli hali ya korona kwa watu, ni kupima ni weekly or semi-month basis. Hiyo ni kwa maana hali (status) ya ugonjwa kwa mtu hubadirika daima. Ukinipima leo sina maambuki, lakini baada ya majuma mawili ukinipima utanikuta na maambukizi. Au leo umenipima nina maambukizi, lakini baada ya juma moja au mawili utanikuta SINA MAAMBUKIZI. Hivyo status yake hubadirika daima. Tofauti na ukimwi ukipimwa unao, basi baada ya miezi mitatu wakikupima tena watakuta unao.

Kwa sisi ambao tumetumia muda mwingi kuusoma na kuufuatilia ugonjwa huu. Kupima kama kenya inavyofanya hakutoi picha halisi ya maambuizi ya ugonjwa.

5. Kuna mambo mawili katika ugonjwa huu. Mosi ni maambuki (cases) na pili ugonjwa au kuumwa sana (sevior cases). Mafanikio katika ugonjwa huu ni kutotishwa na idadi ya maambukizi, bali shughulika kikamilifu na wagonjwa ambao wanaumwa.

Hili ni jambo la msingi sana, maana kuna nchi nyingi ambazo cases zinaongezeka, lakini serious cases, yaani wagnjwa hospitalini wanapungua sana. Mfano mmoja wapo ni nchi ya Sweden.

Huo ndiyo ukweli kuhusu huu ugonjwa wa kovidi.
 
Kenyan,
Lakini walajirushwa na mafisadi wanaoimaliza kenya mbona wanafichwa.na hawatangazwi poleni Mimi ni mgeni napita tu.
 

Ni aibu sana watu mnaopenda kujiita wataalam na nyie pia mlishaingizwa kwenye hayo mawazo ya kujichokea, mpaka mnatumia nguvu nyingi kujaribu kueleza zero points, tafuta mtu akutafsirie nini maana ya "asymptomatic carriers of COVID-19" ambayo inasababisha watu wajitokeze kupimwa hata kama hawaumwi ili kuwalinda walio na magonjwa mengine kama kisukari.

Hiyo mnayopenda kujipa mfano nayo leo hii wanapukutika kushinda maelezo, uzuri wao hawafichi.
 
Uhuru anajaribu kuzuia mafuriko kwa mikono. Ajiulize kwa nini mwanzoni raia wake walikuwa wanatuponda huku ila kwa sasa mashambulizi yanaelekezwa kwake. Jamaa kafeli pakubwa kwenye hili janga hata yeye analitambua vema hilo. Anaona kuihusisha Tz inaweza kumpunguzia lawama. Aibu sana!

Hajui raia washaamka sasa hivi kasoro haya maroboti ya JF yaliyo mahututi majumbani yamejifungia.
 

Wakati mwingine kuna mambo hutakiwi kuwaambia wananchi maana yanazidi kuhatarisha maisha yao. Kuna wakati unaweza ukawa umelalia nyoka bila kujua na ukaamka ukaondoka na nyoka asikuguse, lakini mtu anaweza kukuambia umelelia nyoka ukazimia ukafa, na saa ingine hata huyo nyoka pengine hayupo.

Kwahiyi MK254 si vizur kutangaza tangaza kiholela inachangia kuumiza watu pia na sio sifa ama democrasia! [emoji114][emoji114]
 

Uwe unakuwa makini sana kutumia neno kabla ya kulijua. Siyo kwa kuwa umesikia watu wakiongea, basi na wewe unadandia kulitumia hata pasipo stahili.
 
Kutokana na kauli ya Kenyetta ghafla ndege ya serikali ya Kenya ,iliyo kua imewaleta Wajumbe toka Serikali ya Kenya kwa ajili ya ibada ya mazishi ya mh Mkapa, imeshindwa kutua JKN Inter Airport.

Ujumbe wa viongozi wa Kenya waliokuja kuhudhuria mazishi ya Rais mstaafu Benjamen Mkapa umeshindwa kutua uwanja wa ndege wa JNIA, Dar na hivyo kulazimika kurudi Nairobi.

Serikali ya Tanzania imesema ndege hiyo imeshindwa kutua kutokana na sabbu za kiufundi lakini Mhariri wa Radio Africa Group ya mjini Nairobi, Oliver Mathenge amesema kuwa ndege hiyo imezuiwa kutua na mamlaka za Tanzania.

Mathenge amedai msafara huo umefurushwa kutokana na mgogoro wa kidiplomasia baina ya Kenya na Tanzania uliosababishwa na janga la corona. Taarifa za Mathenge hazijathibishwa na serikali ya Kenya.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Kenya, Macharia Kamau amesema serikali itatoa taarifa kuhusiana na tukio hilo hapo baadae!
 

Hili ni janga la kisayansi linapaswa kushughulkiw kisayansi sio hayo matamko yasiyokua na mantiki na mifano sijui ya nyoka wala nini.
 
Uwe unakuwa makini sana kutumia neno kabla ya kulijua. Siyo kwa kuwa umesikia watu wakiongea, basi na wewe unadandia kulitumia hata pasipo stahili.

Ukipata mtu akutafsirie maana yake nahisi utatia akili, ila kwa sasa nyote sijui mumeingiwa na pepo gani hata wale huwa mnajinadi wataalam, hakuna anayeonekana kushirikisha ubongo, mnatumia nguvu nyingi kuandika insha zenye zero points.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…