Mocumentary
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 806
- 2,049
Tulishaambiwa tutaishi na corona kama tunavyoishi na mahonjwa mengi hata maralia inaua, magonjwa ya moyo yanaua piaMwenyewe nimejifungia; sihitaji ruhusa yake maana najua fika kuwa korona ipo!
Ndugu zako wameshakufa wangapi?Si afadhali Kenya wanajitahidi, sisi tumekaa tu tukijidai hakuna korona kumbe watu wanakufa kila leo, tunaficha ukweli!
Mitaa gani mbona kila kitu kipo shwari huwezi kuficha vifo kwa sababu kila MTU ana smartphone siku hizi.#truth.
Isiwe kama Tanzania wanaodai coronavirus imeisha kumbe inaua mitaani.
Ukipata mtu akutafsirie maana yake nahisi utatia akili, ila kwa sasa nyote sijui mumeingiwa na pepo gani hata wale huwa mnajinadi wataalam, hakuna anayeonekana kushirikisha ubongo, mnatumia nguvu nyingi kuandika insha zenye zero points.
Ukweli toka kwa nani? Mbona hao waliokuwa wakisema Corona inaua watu na kukataa kuingia bungeni ndio waliofanya maandamano ya kumpokea Lisu bila kujali sheria za kujikinga?Hicho ndicho kinachoendelea. Tumeshadanganywa kwamba COVID19 haipo Tanzania lakini ukweli ni kwamba bado vifo vinatokea na kudaiwa wamekufa kwa ugonjwa wa kubana mbavu kumbe ni COVID19.
Hicho ndicho kinachoendelea. Tumeshadanganywa kwamba COVID19 haipo Tanzania lakini ukweli ni kwamba bado vifo vinatokea na kudaiwa wamekufa kwa ugonjwa wa kubana mbavu kumbe ni COVID19.
Hicho unachosema cha kuwa korona haipo ni wewe ndiye unayesema. Mimi naangalia kila siku TV za nyumbani, elimu na tahadhari inatolewa kila siku. Ugonjwa usingekuwepo hayo yasingefanywa. Ukweli ni kuwa madhara ya ugonjwa huu Tanzania na Afrika kwa ujumla siyo makubwa kama maeneo mengine. Tumependelewa. Mwisho namaliza kwa kusema ugonjwa bado upo tuchukue tahadhari kama wajuvi wa afya wanavyosema.
Hebu soma kwa kituo Mkuu ili uelewe nilichoandika.
Mbona hata Chadema awachukui tahadhari dhidi ya korona maana mnasema serikali ya Tanzania inaficha sasa kwanini wewe na wapinzani amjikingi kwa barakoa na kujifungia ndani au magu kawa shikieni bunduki msivae barakoa.#truth.
Isiwe kama Tanzania wanaodai coronavirus imeisha kumbe inaua mitaani.
Mbona ukuwashutumu chadema kwa kupuuza korona maana wanakutanika bila kujali korona?Mwenyewe nimejifungia; sihitaji ruhusa yake maana najua fika kuwa korona ipo!
Najaribu kuwaza hapa, serikali yetu ingefanya mnachokifanya huko yaani hakungekalika, Wakenya huwa tuna muamko tofauti sana, ila naona Wabongo wameanza kuamka amka, kwa namna walivyojitokeza kumlaki Tundu Lissu licha ya mikwara mliyokua mumewatolea inadhihirisha kiaina wana kamuamko fulani.
Kenyatta anapaswa kudili na corona kwa njia anazojua yeye mwenyewe. Aache kulalamika. Wananchi wake wanamacho, wanaakili, wanaona na wanasikia kila kitu kilichopo Tanzania. Huku tz hakuna corona hata chembe, huo ndio ukweli na wakenya msijaribu kutuletea corona yenu hapa.
Hongera sana mzee kenyatta, mficha maradhi kifoo humuuumbuaa,[emoji23] waswahili wanaendelea kuzika wabunge, mawaziri hata na maraisi wastaaafu!! huku wakijidanganyaaa no koronaaaaa![emoji23]
Endelea pia kuwabana kabisa kuleee mipakanii na nyanya zaooo hukoo!!
Kwenye nchi "ile" ya Bwana "yule" hata alipoambiwa gonjwa la ZIKA limeingia nchini mwake akamfukuza kazi mkurugenzi, sembuse Covid-19!!!!Safi sana rais, endelea kutupea takwimu zote hamna haja kuogopa au kujichokea, isemwe kama ilivyo, mwanzo mwanzoni tulikua na uwoga ila kwa sasa watu wamekua na ujasiri wa kupambana maana hamna kinachofichwa, tunaambiwa kama ilivyo bila kumumunya.
Hili suala la Corona hunikumbusha ilivyokua mara yangu ya kwanza kupima UKIMWI, yaani kabla kupata ujasiri wa kwenda kupima nilihangaika sana kwa uwoga, siku nyingi niliishi kwa kujiaminisha sina UKIMWI, ni gonjwa la mabeberu na haliniathiri, lipo kwa ajili ya wengine, mimi mzima, mimi kidume, nikawa najiaminisha pumba ila kila nikikohoa kidogo tu baasi naamini ndio hapo limenikuta, ila hatimaye nilipiga moyo konde na kupima na tangu kipindi hicho baada ya kupima sijawahi kusita kupima tena na tena, ukweli uliniweka huru John 8:32
Bila kuujua ukweli, mtateseka sana kimawazo maana kila kifo cha mtu yeyote mnajikuta mkishuku na kueneza uvumi na tetesi kwmba kafa kwa Corona.
YOU CAN'T HANDLE THE TRUTH
Na huyo aliyekwambia ni daktari mtaalamu siyo? Kalaga bao!Tulishaambiwa tutaishi na corona kama tunavyoishi na mahonjwa mengi hata maralia inaua, magonjwa ya moyo yanaua pia
Rip uncle ben
Una ndugu yako hata 1 kafa kwa corona? Au hata jirani? Au hata rafiki wa jirani yako? Au hata rafiki wa rafiki yako?Hicho ndicho kinachoendelea. Tumeshadanganywa kwamba COVID19 haipo Tanzania lakini ukweli ni kwamba bado vifo vinatokea na kudaiwa wamekufa kwa ugonjwa wa kubana mbavu kumbe ni COVID19.
Basi endelea kukifungia hadi wagonjwa wabaki 0 dunia nzimaMwenyewe nimejifungia; sihitaji ruhusa yake maana najua fika kuwa korona ipo!