Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

Katiba mpya ni madai ya CDM vyama vingine wanafuata mkumbo ili siku mtu akitaka kwenda CDM apokelewa sababu katiba iliyopo haina ubaya kama unaosemwa kikubwa vyama pinzani wanaona kupata nafasi zingine ubunge ushakuwa kazi sana kutokana na kuwa na ushawishi mdogo kwa wananchi fikiria kama Mwenyekiti wa CDM amekosa jimbo sasa wanachofanya ni kutanua wigo wa kupata nafasi zingine kama u DC u kuu wa mkoa, ukurugenzi na nafasi ya katibu tawala pia wanataka nafasi ya u waziri kwamba Mh. Asiteue hao watu wapigiwe kura sasa wananchi tutakuwa tunafanya shughuli gani kila siku ni uchaguzi. Madai ya katiba mpya ni tamaa za madaraka za wapinzani wanaona CCM kama wanafaidi kumbe hata wakipigiwa kura kwenye hizo nafasi bado watakosa tu mfano mdogo tu kama udiwani ndani ya kata tu mnashindwa kushawishi wananchi ndio mtaweza wilaya au mkoa mnacheza nyie. Wananchi hawana shida na katiba iliyopo kama marekebisho ni madogo madogo sana tusisemee watu maneno ambayo hawajasema kama mnataka ukuu wa mkoa na wilaya nendeni mkaombe sio kushinikiza Serikali iliyopo madarakani mambo yenu binafsi.
 

Acha upotoshaji, katiba mpya sio ya wanasiasa pekee, wanasiasa au CHADEMA, wanaonekana mbele kwasababu Katiba inaanza na political process. Ila katiba inajumuisha makundi yafuatayo.

1. Wakulima
2. Wafanyakzi
3. Wafanyabiashara
4. Walemavu.
5. Wanafunzi.
6. Wanasiasa.
7. Wazee.
8. Wanawawake
9. Watoto.
10. Wasiojiweza.
11. Wanamichezo.
12. Wasanii.
13. Wanataaluma.

Pia, katiba mpya sio kwaajili ya udc au ubunge Bali inajumuisha mambo mengi. Kama.

1. Muuondo wa muungano.
2. Haki za binadamu.
3. Maadili ya taifa.
4. Uchumi.
5. Ushirikiano wa kimataifa.
6. Kodi na mapato ya taifa.
7. Rasilimali za nchi.
8. Wajibu wa kila Raia.
9. Wajibu wa serikali.
10. Mahakama
11. Bunge.
12. Mamlaka ya nchi.
13. Vyombo vya ulinzi na usalama.
14. Tume ya uchaguzi. Nk.

Kwa hivyo chadema Kama wanasiasa wait Wana haki ya kujadili mambo yanayo wahusu kwenye katiba na wengine wataingilia Kati.
 

Acha kujificha kwenye mgongo wa wananchi. Mwaka 1977 Tanzania iliandika katiba mpya, je wananchi waliamdamana kuishinikiza katiba mpya?. Tusiwatumie wananchi Kama mgongo wa kakimbia majukumu.
 

Unajipinga mwenyewe. Unataka Katiba ifanyiwe marekebisho ila hutaki katiba mpya kisa wanatume watalipwa pesa?. Huo ni wivu tu. Mbona miaka michache iliyopita watu waliunga juhudi na Uchaguzi ulikuwa unafanyika kila siku?. Mbona hukuhoji Hilo?

Mbona katiba iliandikwa mwaka 1977 hamkulalamika? Ikaja kufanyiwa marekebisho makubwa 1984 hamkulalamika? Imefanyika marekebisho mpaka 2005. Sasa kwanini tufanye marekebisho baadla ya kuandika mpya. Mnataka nchi iende kibabe kwa maslahi ya Nani?.
 
Mkuu Mganguzi kwanza nikupongeze kwa kuwa na maoni tofauti na lazima tuheshimu kwa kuwa Kila mtanzania anauhuru wa kutoa maoni yake.

Ila napata mashaka kwamba hata hii katiba ya Sasa Bado hauijui na ndio maana huwezi kuona mapungufu yake, kwa upana wa katiba hii lakini wewe umeona jambo moja tu AMANI. Ni kweli AMANI ni jambo muhimu lakini hii katiba ya Sasa inamengi sana yanayokandamiza hiyo AMANI unayoizungumzia.

Ushauri; Kabla hatujaanza kujibizana kwa hoja tumia muda kwanza kupitia katiba ya Sasa ya nchi halafu Rudi ulete neno.

Alamsik.
 

Wanaotaka katiba mpya wamejitokeza hadharani na kuidai, na wanafahamika waziwazi. Je nyie msiotaka katiba mpya kwanini hamjitokezi muipinge hadharani?
 
Wengi wape
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…