Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

 
Rais haleti katiba mpya, anawezesha tu mchakato wa maamuzi wa hiyo katiba.

Kwa hiyo katiba mpya itapendekezwa, kura zitapigwa. Nyie msioitaka hiyo mpya mtapiga kura za maoni na wale wanaoitaka hiyo mpya watapiga kura zao. Upande utakaopata kura nyingi ndio utakuwa mshindi.

Kwa hiyo kwa sasa hata nyie msioitaka katiba mpya, mnatakiwa pia muungane kudai wananchi kupewa uwezo wa kujiamulia aina ya katiba wanayoitaka karne hii.
 
Kwa nini utake kuzuia mchakato wa watu kujiamulia mfumo wao wa kujiendesha??
Ni sawa wewe kutotaka katiba mpya, ila ni wendawazimu kutaka kuzuia mchakato wa kidemokrasia wa raia wengi kuamua wajitawalaje.
Niko tayari kukosolewa na nimejiandaa kwenda kuzuia huu mchakato mahakamani
 
Kama unafahamu uhuru wa maoni kwa nini unataka kuzuia huo huru wa wananchi wengi kufikia hatua ya kupiga kura ya maoni kujiamulia mfumo wao wa uendeshaji nchi yao?? Kuna nati zitakuwa hazijakaza vizuri kichwani kwako.
Juha ni wewe usiejua maana ya uhuru wa maoni wewe ni mpumbavu
 
Hayo ya sasa hivi Kenya ni maandamano tu yanayoruhusiwa na Katiba, mwaka 2007 wakati wanachinjana katika vurugu baada ya uchaguzi wakiwa na katiba chakavu ya zamani itakuwa bado ulikuwa unanyonya na kutawazwa.
Walisifia nchi jirani wakati wa uchaguzi eti katiba mpya sasa kinachotokea huko siyo katiba mpya bali kitabu kipya
 
We nani aweza kukuamini na huu upotoshaji wako. Galileo hakuuawa alifungwa na kanisa. Halafu we umeonja wapi hiyo katiba mpya ambayo haipo. Umeandika porojo tupu
 
Naunga mkono Hoja kwa asilimia 100 .Watanzania hatuna haja ya Katiba Mpya .Katiba ya Mwaka 1977 ni Msingi Imara wa Taifa letu. Mambo yote ambayo tumeyafanikisha kama Taifa au Watu binafsi yametokana na Katiba hii.

Wanatokea baadhi ya Watanzania wenzetu kwa maslai ambayo hayako wazi , ovu,potofu na hatarishi wanataka Katiba hii ibadishwe.Kumbukeni mkibadirisha Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 huo ndio utakuwa Mwisho wa utambulisho wa Mtanzania.

Acheni kufanya majaribio kwenye eneo lisilohitaji majaribio hata kidogo.

Matatizo mlio nayo au matatizo tuliyonayo kama Nchi kisiasa,kiuchumi,kiteknojia,kibailojia, kiutamaduni,kitibabu etc hayawezi kutatuliwa kwa kubadilisha Katiba.

Mkifanikisha hili mtakuja na hoja ya kubadilisha VITABU VYA DINI ili kuendana na matakwa yenu.

Yangu Maoni ni hayo kwa ajili ya rejea mbeleni.

ARTICLE.
 
Andamaneni basi

Na siku hiyo hiyo mkisema muandamane lazima mcheze kichapo

Ova
 
Subiria kura ya maoni ndio tutajua wangapi wanataka na wangapi hawataki katiba mpya.
Hata wakati wa kurudisha vyama vingi inasemakana wengi karibia 80% walijifanya hawataki vyama vingi kupitia Tume ya Nyalali ila mwaka 1995 kwenye uchaguzi wa vyama vingi Mrema alipata 40% ya kura. Hiyo janja janja yenu itaamuliwa kwa kura.

Kuhusu vitabu vyako vya dini hakuna anayejali , hayo ni mambo yenu na waumini wenzako huko kwenye nyumba zenu za ibada. Mkiamua kuvibadilisha, kuvichoma au kuachana navyo kabisa ni juu yenu. Hili taifa halina dini, haliwezi kuingilia mambo yenu kama hamvunji amani ya nchi.
 
Katiba ndio Dini yetu Kama Taifa.Unaposema wewe ni Mtanzania rejea ya utanzania inakuwa inaanzia kwenye Katiba na si penginepo popote.
 
Kama hiyo katiba mpya haitawekwa sheria ya kunyonga mafisadi hata Mimi pia sitaki maana itakuwa hakuna jipya
 
Tatizo la wanasiasa haswa vyama vya upinzani wanadhani kuwepo kwa katiba mpya kutawawezesha washike dola!!!!!
Mimi nasema fikra hizo ni za kipuuzi!

Mfano angalia nchi JIRANI ya Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya nzuri lakini kila Uchaguzi Raila analia hakubali matokeo na hakubali maamuzi ya mahakama!!!!

Kwa maana hiyo ni wazi kuwa katiba mpya sio "mwarobaini"

Kwa mtizamo wangu, maadili/uadilifu ndio jambo la msingi ambao hauletwi na katiba mpya bali unajengwa kwa kizazi na kizazi.

Uadilifu na maadili mazuri ya viongozi wetu wote walio pita kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa awamu ya sita ni kutokana na uadilifu wa viongozi wetu, wamejengwa na kulelewa kwenye misingi ya maadili na uadilifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…