Rais umewasikiliza wanaotaka katiba mpya! Je, sisi tusiotaka katiba mpya utatusikiliza lini? Tuna hoja!

..........pole mkuu naona unapopolewa mawe na wadau Kwa kuwa na mtazamo tofauti na wao.......hii ndo jf inayodaiwa kuwa ni free to talk openly lakini kumbe nyuma ya pazia watu wanataka uzungumze wanachokipenda wao, ubaguzi na kutotendeana haki kunaanzia humu hata kabla ya wenye mamlaka tunaowalalamikia kila siku........ ........humu ukitaka uonekane una akili unatakiwa uikosoe serikali kila siku, uipende chadema tu, udai katiba au umkashifu hayati Magu......
 
Katiba sio dini yetu kama Taifa, uliwahi kuona wapi dini inafanyiwa marekebisho??
Hii katiba ya 1977 ni ya nne tangu Tanganyika na Tanzania kuwepo. Tunahitaji mpya ya tano sasa.
Katiba ndio Dini yetu Kama Taifa.Unaposema wewe ni Mtanzania rejea ya utanzania inakuwa inaanzia kwenye Katiba na si penginepo popote.
 
NI MJINGA TU NDIO HATAKI KATIBA MPYA
 
Tofautisha maandamano na ubora wa katiba. Kenya kesi ya u haguzi wa Rais ilichukua siku tano, ila bongo kesi ya ubunge wa akina Halima Mdee itachukua miaka mitano.
Kwa hiyo mnataka kwa ajili ya akina mdee
 
Duuh hivi ni amani au utulivu??
Unaogopa migogoro au unapenda kukandamizwaa??
 
Kwamba Rais naye apoteze muda kusikiliza maoni ya vichaa wakati maoni yenu nyinyi Wapumbavu yatachukuliwa kutoka kwa Madaktari wenu wao ndio wanaweza kutafsiri ujinga wenu.
Mnajaribu kumuweka mfukoni lakini hamtaweza
 
Wanaotaka katiba mpya wamejitokeza hadharani na kuidai, na wanafahamika waziwazi. Je nyie msiotaka katiba mpya kwanini hamjitokezi muipinge hadharani?
Ndio tumeanza Sasa tunaratibu Mikutano tutatembea nchi kuwaambia wananchi katiba mpya haifai
 
Wewe umeongea pointi na kiutu uzima, bila Shaka utakuwa Mzee mwenzangu Asante kwa maoni mazuri sana
 
Mmmh ! Waendelee kupongezana tu wa upande ule ? Au iwepo serikali ya mseto ??!
 
Katiba iliyopo mpaka hatujaona madhara yake Bali amani yetu imekuwa tunu katiba hii Ingekuwa mbaya tusingefika hapa
 
Watu wanataka wapate vyeo kwa sababu ajira Yao ni siasa
 
Katiba hii ambayo DPP mficha pesa china anateuliwa kuwa jaji au katiba ipi hiyo? Ambayo spika akitoa mawazo yake anatumbuliwa? Katiba ambayo inaruhusu serikali kukopa bila kikomo? Be serious.
Hakuna nchi isiyokopa
 
Hakuna kinachopiganiwa hapo zaidi ya maslahi ya wanasiasa
Lakini wote wa pande tofauti ni watanzania na wanahaki ya kutawala !! Lakini wanaona hii katiba ndio kikwazo inawapendelea walioko madarakani! Je hiyo ni sawa kwako ??!
 
HUyu sio mjinga anatoa maoni yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…