Rais wa Afghanistan kakimbia nchi!

Rais wa Afghanistan kakimbia nchi!

Nimeangalia live watelaban wakiingia Kabul nimegundua mambo kadhaa:kwanza hawa jamaa wananidhamu ya juu mno,sikuona wakipora vitu au mali,hawana wenge la ushindi kushangilia au kuimba au kupiga risasi juu kufurahia ushindi.
Wanahabari wapo na wanachukua habari bila bugdha.
Nimegundua pia US wamebariki kila kilichotokea,US wamemsaliti kiaina Rais wa Afghan na serikali yake ili Taleban wachukue mamlaka.
Nimegundua pia US siku za usoni atakuwa mpole kwa Taleban na wataanza upya mahusiano ya kidiplomasia pamoja na misaada,kwa.kifupi US anabadili mbinu za kupambana na Taleban.
hapo usa lazima awe mpole sababu walikubaliana kwa sababu wamarekani wakizingua kidogo wamarekani wanaotoroka kabul watachijwa wote hawa jamaa sheria zao sidhani kama zitaendana na marekani
 
Marekani na NATO wamechoka kupigana Vita,hua Ni wachumba Sana kwny Vita vya Muda mrefu.Miaka 20 wavaa makobasi wako wanapigana tu hawapoi,hawaboi.

Vietnam ilionyesha mfano,na Sasa Afghanistan imeandika historia Tena.

Tusubiri utawala wa sharia uanze hapo Afghanistan,wezi Kupigwa mawe,wazinzi kukatwa mikono,wanawake hakuna kutoka nje peke yao,lazima wavae hijabu, takbiir.
Hii kweli kabisa,nchi nyingi hasiwezi vita vya muda mrefu
 
jeshi mpaka USA aamue. Hiyo kitu USA kaipika. ninahisi tayari washasaliti hiyo serikali. USA hanaga rafiki
Raia wa USA ambao ndugu jamaa na marafiki zao wameuawa kwenye hiyo vita wamesha anza kuipiga pressure White house ili ieleze lengo la hiyo vita lilikua ni nini hasa?

Hii ngoma ndio kwanza inaanza,tutajua mengi.
 
Sasa hii Vita si ilikuwa ya Bush? Kwa hiyo Biden aelezee nini hapo?
Kimsingi Biden amesema asingependa kumrithisha rais ajaye Vita.
 
Unawajua vizuri hao wanajeshi?
Hakuna wanajeshi bana,wanajeshi gani lege lege hivyo? Hakuna hata ndege za jeshi? Hakuna vifaru? Hatusikii wakipigana zaidi ya kukimbia uwanja wa vita? Kuna wanajeshi au mgambo?
 
Hakuna wanajeshi bana,wanajeshi gani lege lege hivyo? Hakuna hata ndege za jeshi? Hakuna vifaru? Hatusikii wakipigana zaidi ya kukimbia uwanja wa vita? Kuna wanajeshi au mgambo?
Migambo wamechukua nchi sasa
 
Kwanza nalaumu sana vyombo vya habari vya kiswahili sababu siku zote vimekuwa vya mwisho kwenye kuripoti habari kwa uharaka.

Talebani wako ndani ya ikulu ya Kabul wakikagua kagua.

[emoji327]source: Aljazeera English
IMG-20210816-WA0022.jpg
 
Kuna watu wanaona CIA wamekimbia, na huu ni ushindi kwa Taliban. Binafsi siwaamini CIA, huenda hii kitu imepangwa. Tayari kuna jambo lao wanataka litokee hapo. Fikiria wale wenyeji wa Afghanistan waliofanya kazi na CIA walikwea pipa na kupelekwa USA muda mfupi baada ya CIA kutimua. Na walisema wazi kabisa lengo ni kuwanusuru wasipate kichapo cha ulipizaji kisasi toka kwa Wataliban. Tuhesabu siku , tuone yajayo.

"Parliamentary governments were barred or overthrown, with US support and sometimes direct intervention, in Iran in 1953, in Guatemala in 1954 (and in 1963, when Kennedy backed a military coup to prevent the threat of a return to democracy), in the Dominican Republic in 1963 and 1965, in Brazil in 1964, in Chile in 1973 and often elsewhere. Our policies have been very much the same in El Salvador and in many other places across the globe" (Noam Chomsky- How the world works, p.18)
Kuna watu wanaona CIA wamekimbia, na huu ni ushindi kwa Taliban. Binafsi siwaamini CIA, huenda hii kitu imepangwa. Tayari kuna jambo lao wanataka litokee hapo. Fikiria wale wenyeji wa Afghanistan waliofanya kazi na CIA walikwea pipa na kupelekwa USA muda mfupi baada ya CIA kutimua. Na walisema wazi kabisa lengo ni kuwanusuru wasipate kichapo cha ulipizaji kisasi toka kwa Wataliban. Tuhesabu siku , tuone yajayo.[emoji1752][emoji1548]
 
🤔 Mh! Hapa ndio nazinduka hata mimi
 
Us and its huge doublestand they must turnabout with a new strategies against that territory
 
Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amekimbilia Tajikistan, kwa mujibu wa Al Jazeera!

Taliban wameshinda!

Taliban wamechukua nchi!

Mwezi mmoja uliopita, Rais wa Marekani alisema bila kumung’unya maneno kuwa Taliban kuchukua nchi hakuwezekani kwa sababu jeshi la Afghanistan liko imara.

Hahahaa. Well, tayari Taliban wameshachukua nchi na Rais wa Afghanistan kala kona.

==============

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia nchi yake leo jioni baada ya wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul.

Maafisa wawili wa serikali ambao hawakutaka majina yao kutajwa wameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Ghani ameondoka Afghanistan na inaarifiwa amekimbilia taifa jirani la Tajikistan.

Mkuu wa Baraza la Maridhiano ya Taifa nchini Afghanistan Abdullah Abdullah pia amethibitisha habari hizo kupitia mkanda wa video.

Kuondoka kwa Ghani kunatoa taswira halisi ya uwezekano wa kundi la Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan wakati wowote kuanzia sasa.

Wapiganaji wa kundi hilo waliingia kwenye viunga vya pembezoni mwa mji mkuu wa Kabul leo Alfajiri baada ya kupata mafanikio makubwa katika siku za karibuni kwa kuikamata miji mingi nchini humo.
Mkuu, huwa nashangaa akili ya US na siwaelewi kabisa. Wametumia gharama kubwa (about USD 6 Trillion + several deaths of army pesonnel) kwenye vita nchini Afghanistan ambayo finally Taleban wameshinda. US wamepata faida gani?
 
Sasa hii Vita si ilikuwa ya Bush? Kwa hiyo Biden aelezee nini hapo?
Kimsingi Biden amesema asingependa kumrithisha rais ajaye Vita.
Vita ni ya USA na USA ni nchi ya watu sio ya raisi aliyeko madarakani au rais mstaafu,

Kwahiyo raia wasiulize kisa serikali iliyoanzisha hiyo vita haipo madarakani?
 
Mkuu, huwa nashangaa akili ya US na siwaelewi kabisa. Wametumia gharama kubwa (about USD 6 Trillion + several deaths of army pesonnel) kwenye vita nchini Afghanistan ambayo finally Taleban wameshinda. US wamepata faida gani?
US hapo wamepata mara 100 ya hizo dola walizotumia!

Ndio mana mimi nikionaga wapinzani wanawashobokea hawa weupe napata hasira sana!

Ni kweli tawlaa zetu hasa waafrika zina shida, ila nikiona watu kama Lisu wameenda kwa hawa beberu kutafuta sapoti huwa nawadharau sana.
 
Back
Top Bottom