Jaribio la mapinduzi linaendelea nchini Guinea, mpaka muda huu vikosi maalum vilivyoasi tayari viko ndani ya Ikulu ya Rais na vimeondoka na raisi wa nchi hiyo kuelekea naye pasipo fahamika.
View attachment 1925208
Hizi ni picha ambazo baada ya vikosi hivyo kuongia ikulu walipiga naye picha na kupiga naye picha na Rais anaonekana kukamatwa, askari wakimpiga picha.
Picha ya juu ni Rais wa Guinea Alpha Condé aliyekamatwa na jeshi alionekana kwenye mitandao ya kijamii.
View attachment 1925209
Picha ya video ikimuonyesha rais huyo akiwa kakaa na vikosi hivyo vya waasi vikipiga naye picha kabla ya kuondoka naye.
Wananchi katika mji mkuu wa nchi hiyo Conakry wameonekana wakishangilia mapinduzi hayo wakati wanajeshi walipokuwa wakipita barabarani.
View attachment 1925246
Kamanda anayeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi nchini humo inasemekana ni Luteni Mamady Doumbouya ambaye alikuwa mtu karibu kwa upande wa rais wa nchi hiyo.
View attachment 1925272
☝🏾Luteni Mamady Doumbouya
Mzizi wa fitina uko hapa:
"Wananchi katika mji mkuu wa nchi hiyo Conakry wameonekana wakishangilia mapinduzi hayo wakati wanajeshi walipokuwa wakipita barabarani."
Huwa hawajifunzi kutambua demokrasia ni kutawala kwa kuwajibika kwa watu.
Wanasherehekea vipi basi?