Rais wa miaka 10 wa watu milioni 60, siku yake kubwa kuliko zote maishani ilikuwa kukutana na Michael Jackson na Rihanna!

Rais wa miaka 10 wa watu milioni 60, siku yake kubwa kuliko zote maishani ilikuwa kukutana na Michael Jackson na Rihanna!

Hivi ikitoa mtu mmoja katika watu million sitini wanabaki million 59? Hesabu hii sijuwi umepiga kwa kutumia fomula ya wapi? Hapa imefanya na hoja yako isitiliwe maanani

Itakuwa kafanya hivi 60-1=59

Hahahah
 
Ndio maana alienda hijja........kumbe ilikuwa na maana kubwa kwake......tuombe mwisho mwema ....maana shetani kaamua kutoa connection ya waganga njaaa kiringeni
Hija haimpi mbingu ni kunidanganya tu
 
Kuna mambo ya hovyo sana Dunia hii.
Kuanza kupangiana ya kuongea.

Kuwa kiongozi wa Nchi hakukufanyi usiwe na mapenzi binafsi na mambo yako.
Kwahiyo ni dhambi hata akisema yeye anashabikia timu fulani ya mpira kwa kuwa ni kiongozi au tena akihudhuria mechi hiyo ng'ambo?

Vitu vyote ulivyosema anatumia bure ni dhihaka hiyo.
Tarartibu za nchi zimewekwa hivyo.
Kwahiyo ni halali na stahiki kwake.
Na wewe ukitaki pigana uje uzipate hizo hudma.

Lawama nyingine naona ni chuki tu una rogho mbaya,
unaona mwenzako anafaidiiiii
 



Mzee, hujatutendea haki, hujarudisha heshima tuliyokupa.

The biggest day of your life haiwezi kuwa siku uliyokutana na Rihanna na Michael Jackson... Jamani!

Kwa miaka kumi ukiingia bafuni Mikocheni sisi tunaanza kusimamishwa Kiwalani kujiandaa kukupisha unaenda Airport, ukija msibani na harusini tunasimamisha kusali, kulia, kula, kuongea, mpaka we ukasaini kitabu ukakae chini, umestaafu unatumia jumba la serikali bure, petroli bure, vocha ya simu bure, mlinzi bure, mpishi, karani, dereva, shamba boy, and so forth and so forth and so forth.... Kijana wako na mke wako tumewapa ubunge na uwaziri si kwa lolote la kiuongozi walilofanya kabla ya hapo bali kwa heshima yako wewe.....


Lakini the greatest day of your life ni kukutana na Rihanna!

Hukumbuki hata siku moja uliyolala na amani kwa kupata majawabu ya tatizo moja la Mtanzania? Tanzania tuna shida milioni 60, kila mtu ana msongo, jana umetangazwa mgao wa umeme D'Salaam, kwa hiyo hata kwa Mo Dewji nako wamelala na mikelele ya genereta. Walobaki milioni 59 wamelala na mlo mmoja. Hukumbuki hata siku ulioapishwa Rais wetu? Basi ungevunga kwa kutaja siku uliyomuoa Salma, manake nae kakufumbia macho kwa makandokando kibao! Unampaisha Rihanna and your wife is sitting right next to you!


Halafu huna noma unasema ulikutana na Michael Jackson hotelini Spain ukiwa Waziri wa Madini. Hoteli pendwa ya Michael Jackson akiwa Spain ilikuwa ni WESTIN PALACE MADRID, jina lake lingine ni "the icon of luxury!"

Waziri na Rais wa nchi ambayo wasafiri tunasimamishwa vichakani "kuchimba dawa" kwa saab hatuna rest areas zenye vyoo njiani, unatumia viji tozo vyetu kukodi hoteli anayofikia Michael Jackson! Jamani! Na sijui kampuni gani la Spain ulilileta lije kutupiga makinikia..... Msalie Mtume!

Waafrika, nani atatuokoa????



View attachment 2381816

Haya wai chato kafagilie kaburi
 
Kuna mambo ya hovyo sana Dunia hii.
Kuanza kupangiana ya kuongea.

Kuwa kiongozi wa Nchi hakukufanyi usiwe na mapenzi binafsi na mambo yako.
Kwahiyo ni dhambi hata akisema yeye anashabikia timu fulani ya mpira kwa kuwa ni kiongozi au tena akihudhuria mechi hiyo ng'ambo?

Vitu vyote ulivyosema anatumia bure ni dhihaka hiyo.
Tarartibu za nchi zimewekwa hivyo.
Kwahiyo ni halali na stahiki kwake.
Na wewe ukitaki pigana uje uzipate hizo hudma.

Lawama nyingine naona ni chuki tu una rogho mbaya,
unaona mwenzako anafaidiiiii
Achana na hayo matahila ya dikteta
 
thank-you-for-being-you-grateful.gif
 
Back
Top Bottom