Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kuna vitu vyepesi (cheap) vya kutembea navyo na kuna vitu vigumu kama Umeme, maji, mfumuko wa bei, miundo mbinu n.k ambavyo havipaswi kuongelewa kwa sababu ni vikubwa kwa msemaji.Kuna vitu vya ajabu sana, uamuzi wa kutibu majeruhi waliotokana na ajali nao lazima autoe Rais.
Moshi ni kijiji kilichopoa, among them wametapakaa ukanda wetu wa ziwa, pwani n.k.Watu wengi bado hawajui kama hakuna mkoa unaitwa Moshi
Sasa kama kaamu kutoa bonus kuna tatizo gani? Au wewe unajua huduma za afya ni bure yaani huo ndio uboreshaji?Huu upuuzi ndo hufanya tuanze kurumbana bila sababu....kama ameboresha SASA anahangaikia nini. Huduma za afya ni mbovu Sana.
Msilete siasa Kwa kuwa mnamegewa keki
Kila kitu kwa mqagizo mpaka lini? Ikitokea sunami, wakaumia watu laki tano watatibiwa wore bure?Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza majeruhi wote waliotokana na ajali iliyoua watu 25 mkoani Arusha watibiwe bure
Dkt Godwin Mollel amesema hayo leo Februari, 25, 2024 alipowajulia hali majeruhi wa ajali hiyo iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, Mkoani Arusha waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru.
Dkt. Mollel amesema majeruhi wote wanaendelea vizuri na mmoja ndo kapewa Rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC Mkoani Moshi.
"Rais Samia Suluhu Hassan ametuelekeza majeruhi wote wa ajali hii kupatiwa matibabu bila kulipa gharama zozote"
Dkt. Mollel ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu wakati wakiendelea kuwatibia majeruhi na kwa wale waliopoteza ndugu zao utaratibu wakupatiwa miili unaandaliwa na wataalamu.
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 25 na majeruhi 21.
Credit - EastAfricaTV
Ulitaka aagize maiti ziitibiwe bure?, punguza kuishi na maumivu ya moyo.Kuna vitu vya ajabu sana, uamuzi wa kutibu majeruhi waliotokana na ajali nao lazima autoe Rais.
Wewe wacha njaa..Taja rais aliyeboresha huduma za afya kwa muda mfupi sana kumzidi Samia nikuwekee ushahidi hapa.