Rais wa Ukraine awaambia NATO: 'Hii yaweza kuwa mara yenu ya mwisho kuniona nikiwa hai!'

Rais wa Ukraine awaambia NATO: 'Hii yaweza kuwa mara yenu ya mwisho kuniona nikiwa hai!'

Siku zote vuta inaanza kwa sababu ndogo sana, ambazo kukuzwa na kuwa kubwa.

Kushindwa vita ni sehemu ya vita, ukrain isidhanie itaishinda urusi, wakubali tu mapema kwamba wameshindwa kunusuru wasio na hatia kuwa hatiani.
 
Sababu ya kijinga? Haitakaa itokee kamwe taifa kubwa kama Russia kumruhusu NATO na Marekani wawe na access na mipaka yao kupitia nchi iliyopakana nae, sababu kwa kufanya hivyo atakua kajiweka hatarini kiusalama. Marekani ni mnafiki, unadhani angekubali Russia awe na ushirika na nchi kama Mexico na kuwa na uwezo wa kupeleka majeshi yake? Hakuna anaependa vita, ila Putin hakua na chaguo jingine. Hakuna namna yoyote angeweza kuruhusu Ukraine ajiunge NATO, never. Siku chache zijazo rais wa Ukraine atapinduliwa, kisha Putin ataweka mtu anaemmudu kama yule aliekuwepo kabla ya huyu wa sasa, na biashara itaishia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ni mawili,
1. Hujui unachoandika hapa.
AU
2. Unajitoa ufahamu kwa kutokujishughulisha hata kusomasoma japo.

Russia na USA ni majirani kabisa. Tena wa kugawana mpaka.(huko Alaska)
 
Jamaa anafanya proganda kwa kiasi flani, kwani Ukraine ndiyo nchi pekee jirani na Rusia ambaye akitaka kujiunga na NATO?

RUSIA amekosea sana kumvamia Ukraine kwa ukweli, wakija kufanya analysisi wanaitangazia dunia kua walikosea sana.
wewe muandika hii koment ndio umekosea sio RUSSIA
 
He is just greedy for power….Baada ya hapa atawatafuta wengine anaopakana nao wanyonge arudishe tena U.S.S.R .Kwaio China naye Aivamie Taiwan akitoa sababu kwamba Marekani atajiattach .Au Marekani naye amvamie Mexico kwasababu kama za putin?
kila mmoja anavamia kwasababu zake usitake sababu zifanane MKUU
 
Hakuna namna. Wewe jirani yangu unajua NATO na Marekani ni adui zangu namba moja unawakaribisha uishi nao. Pia unajua ni wanafiki. Unataka nifanye nini zaidi ya kukuwahi kabla haujaenda mbali.

Hii vita imesababishwa na NATO na Marekani kwani wao ni watu wa maslahi tu. Angalia wameharibu Irak, Libya, Syria. Korea Kaskazin tu ndio hawajaweza lakini bado hawachoki kuichokonoa japo Korea alishawawahi kwa kuwa na silaha kali kama zao zikielekezwa kwa watoto wa Marekani.
 
hawa wayahudi wanajua wanachoiamulia dunia hii, russia atachapwa tu.
 
Huyu jamaa ukute anasema kupumbaza watu ukute wanataka kumsuprise mrusi hpo Mungu aepushe isije leta machafuko duniani
 
Nimesoma historia..sijawai kusoma popote Vita iliyopiganwa kwasababu za kijinga Kama hii..Russia Ni watu wa hovyo Sana
Hivi wanagombania nini mpaka leo sjapata kusoma sababu ya hiyo vita, nisadie kujua mkuu.
 
Rais wa Ukraine Zelensky amewaonya marais na viongozi wa Ulaya katika video call (conference call) kuwa huwenda wasimuone hai tena milele kufuatia jeshi la Urusi linavyozidi kujikusanya na ktk viunga vya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, alimo rais huyo. Ambapo yeye ni taget namba 1.

Ktk conference call hiyo amewashukuru viongozi hao wa Ulaya lakini pia akawalaumu kwa kushindwa kwao kumzuia Rais Putin asiendelee kuingia zaidi Kyiv.

"NANI YUKO TAYARI KUPIGANA PAMOJA NASI DHIDI YA PUTIN?...KWA KWELI SIMUONI HATA MMOJA"

Kwa kweli mie binafsi (Sikirimimimasikini) nimemuonea huruma sana rais huyu, bora Putin angekubali kuzungumza nae tu na wala asimuue.
======


Ukraine’s President Volodymyr Zelensky warned European leaders in a conference call that they may never see him alive again as Russia’s army masses outside the Ukrainian capital Kyiv.

Zelensky issued the warning during a discussion with several other European leaders on Friday. A day earlier, the Ukrainian president warned that Russian “sabotage teams” had entered Kyiv in search of him and his family. On the call, Zelensky thanked them for their support but chastised them for their failure to do more to stop Russian President Vladimir Putin’s advance.

“Who is ready to fight with us? Honestly, I don’t see anyone .. .I’m asking them, are you with us?” Zelensky said, according to the Financial Times.
Mbona vifo vya wasomali, wairaq na sadam wao, walibya na ghadaf, waafghan na mulla wao havikukuumiza?
 
Mambo ni mawili,
1. Hujui unachoandika hapa.
AU
2. Unajitoa ufahamu kwa kutokujishughulisha hata kusomasoma japo.

Russia na USA ni majirani kabisa. Tena wa kugawana mpaka.(huko Alaska)
Anaejitoa ufahamu hapa ni wewe, kama ulijishughulisha kusoma basi hujui ulichosoma. Nani asiejua kuwa Alaska ilikua sehemu ya Urusi, na Marekani akauziwa 1867? Nani asiejua pia kuwa Estonia na Latvia zimepakana moja kwa moja na Urusi, zilikua sehemu ya Soviet Union na walishajiunga na NATO, na Urusi haku-react kama alivyofanya sasa kwa Ukraine? Kama Urusi ingekua ndio Tanzania unadhani mipaka ipi ni muhimu zaidi kwake kiusalama kati ya ile ya Kenya & Uganda versus ile ya Rwanda na Burundi? Ni wazi Ukraine na Belarus wakijiunga NATO, na Marekani wakapeleka majeshi yake hapo Urusi itakua imezungukwa na maadui karibu upande wote wa Magharibi ya Urusi, na kuweka rehani usalama wa taifa lake, ndio maana Putin hataki NATO iendelee kujitanua tena kuelekea Mashariki, ambayo ndio Magharibi ya Urusi. Nimekuwekea na ramani hapo ujaribu kujifunza kitu, pengine utaelewa sababu ya Putin. Siungi mkono vita, ila naelewa sababu ya Putin kuamua kuingia vitani

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 2131519
 
Nimesoma historia..sijawai kusoma popote Vita iliyopiganwa kwasababu za kijinga Kama hii..Russia Ni watu wa hovyo Sana

Zipo nyingi tena za kishenzi kabisa na tamaa ya mali kama mafuta
Kuna Blair na Bush umewasahau wale wapumbavu waliouwa watu 3m bila sababu za maana na walikuwa hawana njaa hivyo

Urusi kuweka kambi Cuba je?
Akisogea nchi karibu na USA unaona wanavyohaha
Sasa NATO wanataka waweke manowari zao na subs na kambi zao kwenye mipaka yake kwanini asi mind?
 
Back
Top Bottom