DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Kawaida, kiongozi wa taasisi au hata wa nchi inapotokea kuna mgogoro mkubwa unaohitaji uangalizi wako wa karibu na haraka, unaacha unachofanya unarudi kuokoa jahazi. Tumeshuhudia marais hata wa Marekani wanasitisha ziara zao na kurudi kusimamia jambo la dharura hadi litakapokaa sawa.
Cha kushangaza, Yanga hivi sasa ipo kwenye mgogoro mkubwa na vyombo karibia vyote vya michezo nchini ila Rais wake Hersi Said yupo huko anajivinjari. Hii ina tafsiri gani? Ni mbinafsi? Amesahau majukumu yake ya msingi? Ni dharau kwa mamlaka za nchi? Bila Yanga hata huko CAF asingepata na hawezi kubaki na hizo nafasi.
Hersi alipoanza pale Yanga na alipokuwa anatafuta kuaminiwa, alikuwa anaingia front mwenyewe na hilo ndiyo lilimjengea sifa kwa mashabiki wa timu yake. Nakumbuka story ya kutekwa kwa Kibu, alihusika moja kwa moja.
Leo hii, Yanga iko katika hatari ya kushuka daraja, huku mitandaoni wanarushiana barua na shutuma na mamlaka za nchi, halafu yeye amejificha kwenye mwamvuli wa "kamati ya utendaji". Klabu ameachiwa msemaji anayebwabwaja lolote linalomjia kichwani.
Najua mashabiki wa Yanga wanamuona huyu bwana kama masihi wao na hawadiriki kumsema kwa lolote baya ila najua wakikaa chini wenyewe wanawaza makosa na madhaifu yake na yanawaumiza sana kimoyomoyo.