Rais wa Yanga Hersi Said aitelekeza timu yake katikati ya mgogoro mkubwa

Rais wa Yanga Hersi Said aitelekeza timu yake katikati ya mgogoro mkubwa

Hawa ndio wanaojielewa?
Tatizo ni kwamba hayo mafanikio mkijivunia yanga mnajiona mko timamu ila wakijivunia simba ndio hawajielewi, ninyi msimu huu hadi sasa si ndio mnajivunia ngao ya jamii na kombe la muungano au siyo ninyi, mlipofika fainali cafcc mkaanza kujivunia medali mlipoona msimu huu simba naye anaenda kuvaa medali mkayaita mashindano ya umiseta sijui na upuuzi gani
 
Hivi wewe kweli akili zimo? Fainali ya CAF ipi ambayo Yanga haijafika?
Tatizo siyo kufika tu fainali tatizo mmecheza fainali mkiwa na kikosi mlichookita bora na kimekamilika, mna striker kama mayele na bado mkashindwa kubeba lile kombe mbele ya usm alger, ambao hawakuwahi kubeba lile kombe hapo kabla ndio wakalibebea kwenu kwa mara ya kwanza na wala hawakuwa wagumu

Lakini simba imecheza fainali ikiwa inajenga timu zaidi ya nusu ya kikosi kikiwa na wachezaji wageni na wasio na uzoefu na michuano ya kimataifa, na wameshindwa kubeba kombe mbele ya berkane ambaye ni mzoefu wa hiyo michuano hili likiwa kombe lake la tatu kulibeba, na huku akiwa bingwa wa ligi ya morocco ambayo ni ligi ya pili kwa ubora barani africa

Kifupi yanga imetuonesha kwamba hata ikiwa bora na imekamilika vipi ila bado haiwezi kuchukua kombe la africa hata mbele ya timu za kawaida tu, ila simba imetuonesha kwamba hata ikiwa dhaifu inaweza kucheza na timu ngumu na ikavuka kuenda hatua inayofuata kwahiyo katika hizi timu mbili simba ndio ambayo ni promising na inaonesha dalili kwamba ikiendelea kuboreshwa, ina uwezo wa kufanya makubwa zaidi ya haya tofauti na yanga ambayo inaonesha hata iboreshwe vipi ndipo uwezo wake ulipoishia kwa sasa na yote ni sababu ya mashabiki wake kuwa na hulka na kuridhika na mafanikio madogo madogo yasiyo na tija
 
Watu mmetoka mapouvvvvv wakati wenyewe hataa

Haitushtui!!💛💚🖤🖤🖤💪!


Cc Smart911
Hersi aache kujificha kwenye sketi ya Mahondaw. Ameitelekeza timu wakati iko kwenye hatari ya kushuka daraja. Klabu inamfia katika mikono yake, yeye yupo huko anakula pizza na Hamisa Mobetto.
 
Nilisikia Ki alimuolea on behalf!!

Sa itakuaje 🤔????

Anyways time will tell

Cc Smart911
Labda ndo maana kina AliKamwe ghafla wamecharuka kudai pesa za CRDB. Inaonyesha kuna malimbikizo ya madeni huko kwa Trump, boss anatapanya pesa za klabu anawaahidi atamleta Messi.
 
Mlichangishwa michnango kujenga uwanja wa bunju mmefikia wapi? Mliahidiwa msimu huu unaoenda ukingoni mngetumia uwanja wa bunju kama uwanja wa nyumbani je ni mechi ngapi mmecheza na ni nani amehoji
Na hili nalo ni moja ya matatizo ya mashabiki wa yanga nilisahau kuliainisha hapo hili suala la kuona kama kila mchango unaochangishwa na timu yako basi unaibiwa au kuliwa na watu wachache, kama mashabiki wa simba wenyewe hawajalalamikia hiyo michango unajuaje kama wameumia au hawajafurahia kuchanga maana inaonekana ninyi kuchangia timu yenu ni suala la anasa kiasi kwamba mnataka kila senti mnayotoa mjue imetumika vipi hata kama maendeleo ya timu mnayaona, niliona hata ile ishu ya mashabiki wa simba kukatishwa tiketi za kwa mkapa huku fainali ilitakiwa ichezwe zanzibar mashabiki wa yanga ndio mlilishikia bango na kujifanya wasemaji wa mashabiki wa simba ilihali wenyewe sijawasikia wakilalamikia hiyo michango yao maana yake walitoa kwa hiyari na pesa ndogo kama hizo kwao siyo tatizo ili mradi waone timu inapiga hatua mahali
 
Tatizo ni kwamba hayo mafanikio mkijivunia yanga mnajiona mko timamu ila wakijivunia simba ndio hawajielewi, ninyi msimu huu hadi sasa si ndio mnajivunia ngao ya jamii na kombe la muungano au siyo ninyi, mlipofika fainali cafcc mkaanza kujivunia medali mlipoona msimu huu simba naye anaenda kuvaa medali mkayaita mashindano ya umiseta sijui na upuuzi gani
So far 5imba ana trophy gani msimu huu?
 
1749624328000.jpg
 
Kawaida, kiongozi wa taasisi au hata wa nchi inapotokea kuna mgogoro mkubwa unaohitaji uangalizi wako wa karibu na haraka, unaacha unachofanya unarudi kuokoa jahazi. Tumeshuhudia marais hata wa Marekani wanasitisha ziara zao na kurudi kusimamia jambo la dharura hadi litakapokaa sawa.

Cha kushangaza, Yanga hivi sasa ipo kwenye mgogoro mkubwa na vyombo karibia vyote vya michezo nchini ila Rais wake Hersi Said yupo huko anajivinjari. Hii ina tafsiri gani? Ni mbinafsi? Amesahau majukumu yake ya msingi? Ni dharau kwa mamlaka za nchi? Bila Yanga hata huko CAF asingepata na hawezi kubaki na hizo nafasi.

Hersi alipoanza pale Yanga na alipokuwa anatafuta kuaminiwa, alikuwa anaingia front mwenyewe na hilo ndiyo lilimjengea sifa kwa mashabiki wa timu yake. Nakumbuka story ya kutekwa kwa Kibu, alihusika moja kwa moja.

Leo hii, Yanga iko katika hatari ya kushuka daraja, huku mitandaoni wanarushiana barua na shutuma na mamlaka za nchi, halafu yeye amejificha kwenye mwamvuli wa "kamati ya utendaji". Klabu ameachiwa msemaji anayebwabwaja lolote linalomjia kichwani.

Najua mashabiki wa Yanga wanamuona huyu bwana kama masihi wao na hawadiriki kumsema kwa lolote baya ila najua wakikaa chini wenyewe wanawaza makosa na madhaifu yake na yanawaumiza sana kimoyomoyo.
huyo huyo ALI KAMWE anawatosha INJINIA watamuwezea wapi
 
huyo huyo ALI KAMWE anawatosha INJINIA watamuwezea wapi
Mlikuwa mnampamba, watu mwaka huu wakaamua kumuonyesha mjini walikuja kabla yake, akaamua kula kona na kumuachia timu Mzambia na yule roporopo. Timu inazama nyie mnashangilia, ngoja mjikute playoff.
 
Mlikuwa mnampamba, watu mwaka huu wakaamua kumuonyesha mjini walikuja kabla yake, akaamua kula kona na kumuachia timu Mzambia na yule roporopo. Timu inazama nyie mnashangilia, ngoja mjikute playoff.
yani YANGA inazama!!!
nimecheka sana,kama timu inayozama ni YANGA basi timu zingine ikiwemo simba zipo kwenye hali mbaya sana
 
yani YANGA inazama!!!
nimecheka sana,kama timu inayozama ni YANGA basi timu zingine ikiwemo simba zipo kwenye hali mbaya sana
Msipokuja Jpili mnadhani mtakuwa kwenye hali gani? Kinachowapa kiburi ni kwa sababu mna uhakika wa kuwafunga Singida kwenye fainali. Najua nia yenu muelekee CAF shirikisho, hizi zote mnazofanya ni zuga tu.
 
So far 5imba ana trophy gani msimu huu?
Hilo swali ulipaswa uulize baada ya ligi kuisha, ni kama madrid sasa hivi ndio mtu anaweza akawauliza kwamba wana trophy gani msimu huu, vinginevyo mtakuwa mnajitekenya wenyewe na kujichekesha
Sisi tuna kombe la Toyota international tournament nyie mna kombe gani?
Ndio yale yale uliyotoka kuwasema simba hapa kwamba wanajivunia mafanikio madogo, sasa hilo kombe lina hadhi gani hadi useme ni kombe la kujivunia na kumtambia mpinzani wako, hilo kombe lina hadhi gani huko caf kuliko list ya timu zilizopo top five kwenye caf ranking kama timu bora africa
 
Hilo swali ulipaswa uulize baada ya ligi kuisha, ni kama madrid sasa hivi ndio mtu anaweza akawauliza kwamba wana trophy gani msimu huu, vinginevyo mtakuwa mnajitekenya wenyewe na kujichekesha

Ndio yale yale uliyotoka kuwasema simba hapa kwamba wanajivunia mafanikio madogo, sasa hilo kombe lina hadhi gani hadi useme ni kombe la kujivunia na kumtambia mpinzani wako, hilo kombe lina hadhi gani huko caf kuliko list ya timu zilizopo top five kwenye caf ranking kama timu bora africa
Leta hata hilo kombe lisilo na thamani tulione
 
Back
Top Bottom