Rais wangu Samia, 'Tanzania Mainland' ni nchi gani?

Rais wangu Samia, 'Tanzania Mainland' ni nchi gani?

Tanganyika imejivika koti la muungano na kuipokonya znz haki zake zote
 
Rais wa Zanzibar,anatoka Tanzania bara
Rais wa Tanzania anatoka Makunduchi,Zanzibar.
Kuna vitu kuvielewa inabidi usome Ilani ya CCM.hasa pale ambapo Mtanganyika anaweza kuwa Rais wa Zanzibar.
 
Leo wakati Rais Samia akitoa hotuba katika hafla ya utiaji saini mikataba mitatu ya kusaidia bajeti kuu ya Serikali kutoka umoja wa Ulaya wakati wa kutambulisha mawaziri wake amewaita mawaziri wa Tanzania bara, nauliza kuna mawaziri wa Tanzania bara?

Kuna Serikali ngapi ndani ya nchi hii? Na mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wepi?

Kuna kitu kinamsuta huyo mkuu.., kama vp kabla ya 2025 turudishe Tanganyika yetu na tuanze kupambana tujuavyo, na si huu mkanganyiko., na tukisema sana hawachelewi kusema tunabagua, tunachochea na tunapotosha.
 
Tukio hili na mkataba wa bandari limefunua siri ya umuhimu wa Serikali TATU. Kungekuwa na serikali ya Tanganyika serikali ya Muungano ingekemewa na Tanganyika. Kumbukeni ile issue ya ugunduzi wa mafuta kule Zanzibar jinsi wazanzibar walivyokomaa.
 
Nyie ndo mlioyuambia Watanzania wanaingia kote kote pale tulipowauliza Kwa nini Mbarawa anaongoza wizara isiyo ya Muungano. Sasa hapa unajizima data kutudanganya kwamba na nyie mnatambua kuwepo Kwa wizara zisizo za Muungano? Mbarawa na Katibu Mkuu wake wanafanya nini pale uchukuzi?
Yupo pale kama Mtanzania maana yeye ni Mzanzibari lakini pia ni Mtanzania !!
 
Rais wa Zanzibar,anatoka Tanzania bara
Rais wa Tanzania anatoka Makunduchi,Zanzibar.
Kuna vitu kuvielewa inabidi usome Ilani ya CCM.hasa pale ambapo Mtanganyika anaweza kuwa Rais wa Zanzibar.
Hapo sasa ndio patamu !
 
Watu wakiambiwa rasimu ya warioba iwekwe mezani iwe katiba mpya, wanaingia uvunguni kujificha......matokeo yake wazanzibari watatu wamejitwalia mamlaka ya kuuza bandari za Tanganyika, twende tu hadi akili zitukae sawa.​
 
Back
Top Bottom