Rais wangu, Vita ni kubwa, vijicho ni vingi, kaza moyo twende mbele!

Naona uvivu kujibu haya mashudu
 
Tuache kumdanganya Mama yetu, ukweli kwa umuri wake na jinsi yake hadi 2025 hataweza hekaheka za siasa za wakati huo. Ushauri mzuri kwake ni kufanya maandalizi ya kukabithi kijiti na kupumzika na atakumbukwa daima kwa busara hiyo. Hata Mwl Nyerere alifanya hivyo pamoja na watu kuonyesha kumpenda na kumtaka aendelee.
 
Watanzania bado tuna mpenda rais wetu, Mambo na maendeleo tunayaona waziwazi!
 
Watanzania bado tuna mpenda rais wetu, Mambo na maendeleo tunayaona waziwazi!
Wapo wachache wanaoshinda humu jukwaani na kudhani hapa walipo ndio sawa na ukubwa wa Tanzania.

Hii nchi ina hekari za mraba laki tisa, ni kubwa na Samia anagusa kila eneo lake kwa umahiri.

Sasa hivi hakuna kinachokatiza huko angani bila rada zetu nne kuweza kukitambua na mtu wa kawaida hawezi kuona hayo maendeleo ya kutoka kuwa na rada inayoishia kutazama pale Ngerengere Morogoro mpaka kuwa nazo nne zenye kuangaza nchi nzima.

Umeme unawaka nchi nzima. Kuna mechi za ligi kuu zinazochezwa usiku kule Ruangwa Lindi, miaka 20 iliyopita ilikuwa ni kama muujiza kwa umeme kuwaka tena kiwanjani katika mkoa mmoja wa kusini.

Anayeshinda humu JF na kuanzisha uzi wa matusi na kejeli kila kukicha hana picha halisi ya kinachoendelea kufanyika katika kila kona ya Tanzania.
 
Akifanikiwa kumaliza shida ilioko ndani ya chama kila kitu kwake itakuwa ni kuserereka...
 
Kushindwa kwake unakuumba wewe kichwani mwako. Mwalimu Nyerere aliiongoza Tanzania yenye watu milioni 25 tu leo Samia anaiongoza yenye watu milioni 64 na ni ulimwengu wa sayansi ya hali ya juu na teknolojia zilizopiga hatua.

Samia ni mjanja anajizungushia wasaidizi ambao ni vichwa kweli kweli wenye kuijua kazi yao na hivyo wanampunguzia kazi akiwa pale ikulu.

Umri sio hoja kama bado anayo afya na hanywi pombe wala kuvuta sigara na anayo hulka binafsi ya kufanya mazoezi. Kitu kilichomuweka hai RIP Mwinyi mpaka akaweza kufika miaka 98.
 
Kiongozi anayejiita Chura Kiziwi yeye mwenyewe ndiye adui wake wa kwanza.

Kabla ya kulaumu maadui wa Samia, muangalieni Samia mwenyewe anavyojihujumu kwa ujinga wake.
 
Ukweli rais wa kurithi(yaani aliyepata urais wa mbeleko) Huwa ni hatari sana Kwa ustawi wa taifa.Huyu kaharibu Kila kitu
 
Labda niwe mkweli na muwazi, hasa kwenye kutengeneza zanzibar airways hapo pana makosa makubwa sana, aidha sijui watundu wa mitandao wameprint ile nembo kwenye ndege au la!, Endapo kama Ikatokea zanzibar airways tayari tunakuwa tumetengemeza mpasuko, maana yake itatokea Tanganyika airways, badala ya mama yetu Tanzania airways!, Ushauri wangu hata kama zanzibar imenunua ndege basi isome "" Air tanznania - zanzibar! ""
 
Kiongozi anayejiita Chura Kiziwi yeye mwenyewe ndiye adui wake wa kwanza.

Kabla ya kulaumu maadui wa Samia, muangalieni Samia mwenyewe anavyojihujumu kwa ujinga wake.
Remember she is a worker bee!, maneno mengi huweza kumtoa katika Uwajibikaji na hatimaye ufanisi ukapungua, katika kulijenga taifa, nyie wa maneno mengi ongozaneni na kina mbowe na Lissu, kwani hizo ndizo nyumba za maneno!
 
Remember she is a worker bee!, maneno mengi huweza kumtoa katika Uwajibikaji na hatimaye ufanisi ukapungua, katika kulijenga taifa, nyie wa maneno mengi ongozaneni na kina mbowe na Lissu, kwani hizo ndizo nyumba za maneno!
Uwajibikaji upi?

Rais anawajibika kusikiliza wananchi.

Anaweza kukataa hoja baada ya kuisikiliza, lakini hatakiwi kukataa kusikiliza wananchi.

Sasa ukisema kusikiliza wananchi kutamtoa katika uwajibikaji unaji contradict.

Ni kama vile unasema kuwajibika kutamtoa katika uwajibikaji.
 
Ndugu yetu Mbowe akikuonea kijicho ujua una kazi, maana ana uwezo wa kuona nyuzi 360
 
Ndugu yetu Mbowe akikuonea kijicho ujua una kazi, maana ana uwezo wa kuona nyuzi 360
Uwa najiuliza sana mbona wakati wa magufuli hakuna tutusa lilokuwa likisema chochote!, au kuandamana kipumbavu, ipo misingi, Rais inamlazimisha airudie njia ile ile ya Hayati, maana naona amekuwa labda VERY SOFT.
 
[emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…