Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Umeona nilichokiona Mimi...yaani natamani nkupe likekm mia hivi!Maza anajishtukia sana mpk anaudhi yaani ye ndo rais sasa sijui bado hajiamini na nini!akanyage twende!
 
Sioni aibu kwa matendo ya mtu mwingine. Aibu ni zake mkuu
Ikiwa hivyo basi ni mtu asiyekuhusu. Ni mtu usiyempenda. Unayempenda ukiona anafanya matendo ya aibu, inauma na inatia aibu rohoni/moyoni.
 
Anajiangusha na kujidharaulisha. Yupo too defensive. Hakuna anaedharau mwanamke ...
Kuna tatizo la asili yake. Alianzia kwenye NGO. Watu wa NGO huwa ni kama wapambanaji badala ya watoa huduma. Huyu kwa nafasi hii ya urais wa urithi, anajiona kama malengo ya upambanaji wa NGO yamefanikiwa, nimekuwa strong, nimekuwa kama wanaume, wanawake tunaweza, ...... bhla! bhla! kibao!

Ole wake avurunde! Atakuwa amewaharibia wanwake wenzake kama yule Joyce Banda aliyeingia na mkwara na kuruhusu ushoga akiamini kwa kupendwa na Westerners, basi Malawi itapata misaada. Akashindwa na kutupwa nje.
 
SSH anatakiwa awe mkomavu!
I hope baada ya 30th April akipewa u-top wa ccm atabadilika. Otherwise wakimzoea watamfanya shamba la bibi...
 
Awe mwanamke au mwanaume inabaki palepale ni Rais, hata mimi sioni haja ya kuzungumzia ibaki tu usiponiheshimu utaheshimu kiti changu
 
hata mimi nashangaa, kwa hiyo akizishiwa msagaji ataanza kujitetea? Issue zingine ni za kijinga azipuuze vitendo vitasema.
 
Ikiwa hivyo basi ni mtu asiyekuhusu. Ni mtu usiyempenda. Unayempenda ukiona anafanya matendo ya aibu, inauma na inatia aibu rohoni/moyoni.
Mama Samia hanihusu, sio ndugu yangu. Sijawahi hata kumuona live
 
Kuna wanasiasa walijua hayati angewapa wao nafasi ya umakamu, lazima mioyo iwaume. Na ndio hao wanaombagaza chini kwa chini.

Atulie tu na kuchapa kazi. Anapopaniki na kuonyesha hadharani ndio wanapochukua pointi na kuona kama wamefanikisha malengo yao.
 
Anasema vile ili wale ambao wameathirika na mfumo dume waweze kuelewa!
 
Hii iwe ni "Never and never again" kusema tena "mimi mwanamke, najiamini, naweza" etc. Tunataka vitendo sasa. Hata wale anaowapelekea message wataacha kumdharau. Ni vizuri akaelewa kuwa yeye ni rais kwanza na huo uanamke unakuja baadaye kama second..
 
ni asili ya mwanamke kutokujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake tunajiamini sana, tatizo ni kuwa tuko katika dunia ambayo mwanamke haruhusiwi kujiamini, Mwanamke ukijiamini utaitwa majina, utapewa majina, na inafika muda utaanza kuyaamini majina hayo ndiyo majina yako. Bado tuna changamoto kubwa, na battle letu ni kubwa sana.

Mama hajayasema hayo kwa bahati mbaya, kuna chokochoko kubwa kutoka dunia ya kiume.

Ameshapata nafasi, atafanya vizuri. Ambao hawajaridhika watulie tu.
 
Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni (official visit) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa Rais kwanza mwanamke.

Kina Queen Elizabeth wametawala dunia miaka na miaka. Majukumu mazito kuliko aliyonayo.
Amepigiwa Uganda na mseven

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom