Sawa mkuu Kiranga. Wanatumie dini kuwatawala ki vipi?
Ina maanisha dini inadumaza akili za watu.
Dini ndiyo zinawafundiaha watu utii wa kikondoo, zinawaambia watu watii mamlaka, zinawaambia mamlaka yote ya kisiasa yanatoka kwa Mungu.
Ukifuatilia historia ya dini kubwa zote zimeanzia sehemu zenye falme kubwa, ili kuwaweka sawa watu watawalike kirahisi, wasiwe na maswali mengi, na wakiwa na maswali mengi waridhike kwa majibu mepesi kwamba haya matatizo yote tunayopitia duniani ni mipango ya Mungu tu.
Kumbe kuna mengi ni mipango ya wanasiasa wanafaidika kwa ujinga wa watu.
Sasa katika ulimwengu huo ambao wanasiasa wanafaidika kwa ujinga unaoenezwa kwa imani za dini, unategemea mwanasiasa Ruto hata akijua Mungu hayupo, aseme hilo?
Unategemea Ruto aseme nini wakati habari za kuwepo Mungu zinamfaidisha yeye kisiasa hata akishindwa kazi kizembe tu, badala ya kujieleza kwa wananchi kwa nini kashindwa aweze kutoa jibu jepesi tu "ni mipango ya Mungu"?
Ruto kasema hata kama Wakenya wasipompigia kura, Malaika watampigia. Maana yake anaweza kuiba kura na kutumia imani ya dini kuzihalalisha kura kwamba Malaika wamempigia kura.
Huoni kuwa imani ya Mungu kuwepo inamfaidisha Ruto kutawala watu kwa urahisi, na kwa hiyo, ni lazima aitetee tu?