Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote nawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.
.....
We have indeed revealed this (Message) in the Night of Power:
And what will explain to thee what the night of power is?
The Night of Power is better than a thousand months. (laylatu al-qadri khayrun min alfi shahrin)
Therein come down the angels and the Spirit by Allah's permission, on every errand:
Peace!...This until the rise of dawn!

— Sura 97 (Al-Qadr), āyāt 1-5[19]
 
Kufunga sio lazima, kama sjakosea unaruhusiwa kutofunga ukiwa safarini kama safari ni ndefu, ila pia unapokuwa safari hakuna excuse ya kutoswali, kuna swala za safari unaswali ukiwa hapo kwenye kiti chako, kama ni adhuhuri unachanganya na Alasiri.
Inshaalla.safali yangu ni kianzia alfajir mpaka sita usiku nipo kwenye kipando,na umesema naweza swalia kwenye siti inakuwaje nikiwa nimekaa siti moja na ndugu zetu wakike iyo swala inakuwaje apo,huenda sina maji ,mchanga hamna ntafanyaje ili niweze kupata udhu nipate kuswali
 
Assalamualaik,
Kuna aya ktk Surat Al baqrah inaeleza juu ya watu walioko ktk Safari na wagonjwa, kwamba wao watafunga ktk cku zitazofuata.
Ktk suala la swala unatakiwa kuswali swala ya safari, kwani swala haina excuse hata kwa wagonjwa inawapasa kuswali.
Wallah aalam.
Samahan kidogo katika kuswali safali naweza kuinganisha na alfaji
 
Hapana, Alfajiri inatakiwa kuswaliwa pekee rakaa mbl, addhuhur na laasir unachanganya, unaunganisha rakaa mbl kila moja zinakua rakaa nne, magharibi na ishaa unaswali rakaa tano, tatu za magharibi na mbl za ishaa. Khalas, wallah aalam!!
 
Inshaallah nashulu kwa hilo
 
Inshaalla.safali yangu ni kianzia alfajir mpaka sita usiku nipo kwenye kipando,na umesema naweza swalia kwenye siti inakuwaje nikiwa nimekaa siti moja na ndugu zetu wakike iyo swala inakuwaje apo,huenda sina maji ,mchanga hamna ntafanyaje ili niweze kupata udhu nipate kuswali
kuhusu kukaa na mwanamke hyo sio tatizo hayo mambo mengine tunamuachia mungu ye ndo mjuaji cha umuhimu we swali tekeleza wajibu wala usimfikirie uliyekaa nae.
Kuhusu udhu hapo kuna vitu nimesahau watu wengine wataongezea ila nachokumbuka wakati nasoma pale same tukiwa tunarudi likizo nyumbani, waalimu walikuwa wanatuelekeza pale kwenye kiti cha mbele yako unafanya kupagusa kwa mikono miwili halafu unafanya kama unatawadha. Like kama unashika kile kiti pale kichwa chako kinapoangalaia halafu halafu unajipaka kuanzia mikono then utagusa tena kwa mikono miwili utaenda kwenye uso mpka umalize viungo vya lazima kutia udhu. Kama nitakuwa nimekosea watu wanirekebishe
 
Inaitwa kutayamamu kama sijakosea,na inakuwaje kuipata kibra yangu maana kuswali ni mpaka niipate kibra sasa katika usafili naipataje au sio lazima kibra,samahani lakin kwa maswali nataka kuelewa
 
Kujuzu Kutoelekea Qibla
Inajuzu kutoelekea qibla katika hali mbili:

Kwanza, wakati wa khofu kubwa na kuwemo vitani; katika hali hii watu husali wakiwa wako kwenye kipando au wanakwenda kwa miguu, husali wakielekea qibla au bila ya kuelekea qibla; yote hutegemea hali ya vita ilivyo. Hivi ni kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. .........". (Al Baqara : 239).

Ruhusa hii imetolewa kwa Sala ya fardhi pia, sio ya sunna tu; kwa sababu huweza kutokea hali ambazo zitafanya mtu asiweze kuelekea qibla, kama wakati wa vita. Katika hali kama hizo hailazim kuelekea qibla hata katika kuhirimia (kufunga) Sala, bali atahirimia na huku anakwenda, ama kawa miguu au kwenye kipando na bila ya kuelekea qibla; wala haitakuwa juu yake kulipa Sala atakazozisali katika hali hii. Muhim ni kwamba haitakiwi kuakhirisha kusali, ni muhim kusali katika wakati wake; hivi ni kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"…. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu". ( Annisaai : 103 ).
 
Inshaalla.safali yangu ni kianzia alfajir mpaka sita usiku nipo kwenye kipando,na umesema naweza swalia kwenye siti inakuwaje nikiwa nimekaa siti moja na ndugu zetu wakike iyo swala inakuwaje apo,huenda sina maji ,mchanga hamna ntafanyaje ili niweze kupata udhu nipate kuswali
Udhu ni kinga kwa muumin kwa mambo mengi. Jaribu uwe nao kila nyakati. In case umekuponyoka na uko ktk safari za mabasi yetu haya, jaribu unapofika ktk vituo vyao ambavyo hutumika kwa ajili ya kuchimba dawa na msosi uwe unapata udhu. Ama ktk ndege toilets zenye maji zipo.
 
Tupa macho waangalie watu unavyotoka, hutuona isipokuwa fakiri anateseka na ufakiri wake, au tajiri amebadilisha neema ya Mungu kuwa ni kufuru, au bakhili ameutumia ubakhili kujikusanyia mali, au mtu muovu ambae kama kwenye masikio yake ameeka vizibo hasikii mawaidha, wako wapi watu wema na waliohuru wote wamepotea. ( Imam Ally a.s katika Nahjulbalagh hutba no 129)
 
Kufunga sio lazima, kama sjakosea unaruhusiwa kutofunga ukiwa safarini kama safari ni ndefu, ila pia unapokuwa safari hakuna excuse ya kutoswali, kuna swala za safari unaswali ukiwa hapo kwenye kiti chako, kama ni adhuhuri unachanganya na Alasiri.
Udhu ni kinga kwa muumin kwa mambo mengi. Jaribu uwe nao kila nyakati. In case umekuponyoka na uko ktk safari za mabasi yetu haya, jaribu unapofika ktk vituo vyao ambavyo hutumika kwa ajili ya kuchimba dawa na msosi uwe unapata udhu. Ama ktk ndege toilets zenye maji zipo.
Wakuu hivi ukiwa katika safari ya umbali wa kiasi gani unaruhusiwa kuacha kufunga?
 
Tupa macho waangalie watu unavyotoka, hutuona isipokuwa fakiri anateseka na ufakiri wake, au tajiri amebadilisha neema ya Mungu kuwa ni kufuru, au bakhili ameutumia ubakhili kujikusanyia mali, au mtu muovu ambae kama kwenye masikio yake ameeka vizibo hasikii mawaidha, wako wapi watu wema na waliohuru wote wamepotea. ( Imam Ally a.s katika Nahjulbalagh hutba no 129)
Ndugu yangu sory naomba nieleweshe zaidi hii hadithi nimeisoma sijaielewa
 
IMG-20170606-WA0005.jpg
samahani wakuu kidogo nimetoka nje ya mada
 
Kujuzu Kutoelekea Qibla
Inajuzu kutoelekea qibla katika hali mbili:

Kwanza, wakati wa khofu kubwa na kuwemo vitani; katika hali hii watu husali wakiwa wako kwenye kipando au wanakwenda kwa miguu, husali wakielekea qibla au bila ya kuelekea qibla; yote hutegemea hali ya vita ilivyo. Hivi ni kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. .........". (Al Baqara : 239).

Ruhusa hii imetolewa kwa Sala ya fardhi pia, sio ya sunna tu; kwa sababu huweza kutokea hali ambazo zitafanya mtu asiweze kuelekea qibla, kama wakati wa vita. Katika hali kama hizo hailazim kuelekea qibla hata katika kuhirimia (kufunga) Sala, bali atahirimia na huku anakwenda, ama kawa miguu au kwenye kipando na bila ya kuelekea qibla; wala haitakuwa juu yake kulipa Sala atakazozisali katika hali hii. Muhim ni kwamba haitakiwi kuakhirisha kusali, ni muhim kusali katika wakati wake; hivi ni kwa Qauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"…. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu". ( Annisaai : 103 ).
Nashukulu sana kwakuweza kunifunulia nilichokua namashaka nacho inshaallah
 
Udhu ni kinga kwa muumin kwa mambo mengi. Jaribu uwe nao kila nyakati. In case umekuponyoka na uko ktk safari za mabasi yetu haya, jaribu unapofika ktk vituo vyao ambavyo hutumika kwa ajili ya kuchimba dawa na msosi uwe unapata udhu. Ama ktk ndege toilets zenye maji zipo.
Nashukulu mkuu
 
Back
Top Bottom