Ramadhani na Kwaresma kugongana je is it a coincidence? The evidence says No!!!

Hujasomeka
Hoja zako za kitoto hamn kipya zilikuwepo tangu hujazaliwa ,the same wewe hauna unacopy somewhere.

Kingine wewe uko kwenye kundi( dini nyingine) ambalo unaleta chuki zile zile kwa imani nyingine..Jiangalie sana utakuwa mtu mkubwa halafu mpumbavu..
Bora uje na logics kuliko kunakili kutoka kwa watu ni chuki za kurithi.
 
Africa walikuwa na tamaduni gani ? Kabila langu nimesoma wanaamini maisha baada ya kifo niambie lako ?
 
Hembu wewe tuambie inakuaje Kwaresma, Ramadhani, Naw-Ruz na Holi ziangukie mwezi mmoja??
Ramadhani Imeanza Kulingana Siku hizi tu na Mwezi wa Kwa Rezima Ila Zamani haikuwa Hivyo..

Hiyo ni simple tu inatokana Na Tarehe Kufanana na Ikumbukwe Tarehe za Kiislmu Yaani Hijriya Zinaenda Tifauti na Tarehe za Dunia au Za Roma au Miladiya..

kwanza Nikukumbushe Kwamba Ramadhani Ni mwezi wa 9 Wa Calendar ya Hijriya Na Calendar ya hijiriya Ina Siku 30 kwa Kila Mwezi na Siku zake Hutegemea na Mwezi..

Kwa Kuanza Hii ndo miezi ya Kiislamu au Miezi ya Hijriya..

1. Muharram (المحرّم)
2. Safar (صفر)
3. Rabi' al-Awwal (ربيع الأول)
4. Rabi' al-Thani (ربيع الآخر)
5. Jumada al-Awwal (جمادى الأول)
6. Jumada al-Thani (جمادى الآخر)
7. Rajab (رجب)
8. Sha'ban (شعبان)
9. Ramadhan (رمضان)
10. Shawwal (شوّال)
11. Dhul-Qa'dah (ذو القعدة)
12. Dhul-Hijjah (ذو الحجة)

Na Hii ndo Miezi ya Kimiladiya..

1. Januari (January)
2. Februari (February)
3. Machi (March)
4. Aprili (April)
5. Mei (May)
6. Juni (June)
7. Julai (July)
8. Agosti (August)
9. Septemba (September)
10. Oktoba (October)
11. Novemba (November)
12. Desemba (December)

Na Kwakujibu Swali lako Nitarudi Miaka Kumi Nyuma Kuprove Theory Zote mlizotoa Ni just Conspire tu na Haina Uhalisia..

Mwaka 2015, Ramadhani ilianza tarehe 18 Juni, na Kwaresima ilianza tarehe 18 Februari.

Mwaka 2016, Ramadhani ilianza tarehe 6 Juni, na Kwaresima ilianza tarehe 10 Februari.

Mwaka 2017, Ramadhani ilianza tarehe 27 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 1 Machi.

Mwaka 2018, Ramadhani ilianza tarehe 16 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 14 Februari.

Mwaka 2019, Ramadhani ilianza tarehe 6 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 6 Machi.

Mwaka 2020, Ramadhani ilianza tarehe 24 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 26 Februari.

Mwaka 2021, Ramadhani ilianza tarehe 13 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 17 Februari.

Mwaka 2022, Ramadhani ilianza tarehe 2 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 2 Machi.

Mwaka 2023, Ramadhani ilianza tarehe 23 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 22 Februari.

Mwaka 2024, Ramadhani ilianza tarehe 11 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 14 Februari.

Mwaka 2025, inakadiriwa kuwa Ramadhani itaanza tarehe 1 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 5 Machi...

Sasa hiyo Hapo Juu Inaprove nini Inaprove kwamba Calendar Baina ya Miladiya na Hijriya hazina Static Formation na Haziwezi kuwa..
Ramadhani Imewahi Kuwa Mpaka Mwezi wa Kumi na Moja na Mwezi wa Kumi na Mbili ila KWARESMA haijawahi na Itakuja Kuwahi kuwa..

Na Mwaka 2033 Tunategemea Idd El fitri Itaangukia Tarehe 25/12 siku ya Xmass Najua Pia itakuwa Story nyingine kwa Watu wa Kuconspire
 
Unanikosea sana kuniita mtu wa dini. Kuwa na dini ni ukichaa...

Niambie kwanini unaenda kanisani au msikitini?
 
Hii ya Uislamu kuwa toka enzi za Adamu ni uongo wa wazi kabisa. Kwanza quran na hadithi zinasema muislam wa kwanza na shehe Muhammad. Pili ili uwe muislam unatakiwa ufuate nguzo tano za Uislamu ikiwemo kushahadia.

Je wapi Adam na Mitume kabla ya Muhammad walishahadia? Kwa hili mmefanganywa na kudanganyika mkuu.

Kuhusu ibada ya Sanamu, ni kweli Wakatoliki kuna masanamu mengi.sana ila ni kweli nanyi mnaabudu lile jiwe pale Macca. Pia unasema kuwa sio kila msikiti una lile.Jiwe, ni kweli usemacho ila ushawahi jiulize bro kwanini kila mahali msikiti unaelekea QIBRA ambako ndiko Macca alipo Mungu wenu(Allah pale Kaaba)?
 
Unanikosea sana kuniita mtu wa dini. Kuwa na dini ni ukichaa...

Niambie kwanini unaenda kanisani au msikitini?
Una dini hauwezi kujidanganya hata wanyama wana dini ni vile hujitambui ...Si rahisi kama hujitambui wewe binafsi hlafu halafu unataka kuleta hoja ambazo hujui kitu
 
Hivi Mungu na yeye anafungwa na mambo ya tarehe?
 
Hoja ya majina ni ya kijinga sana, Chukulia hapa hapa Tanzania angalia majina ya Kiswahili mengi utakuta Asili yake ni kwa Waisilamu.

Jumanne, Majaliwa, Tatu, Zawadi, Maua, kilua, mosi, pili, waridi, Balozi na Majina mengi tu, Uisilamu upo very clear kwenye issue ya majina, umpe tu mtu jina zuri,
 
Kimsingi bro umenena vyema kuhusu kuangukia wakati mmoja hii hata kwangu sio big deal.

Binafsi natambua na kuthamini uwezo wako bro juu ya issue za kidini. Kuna hoja umeiruka hapo ambayo natamani ungeweka neno mkuu.

Uislam kuanzishwa na Wakatoliki. Hii imekaaje? Sema Neno mkuu kwa uzoefu wako.
 
Una dini hauwezi kujidanganya hata wanyama wana dini ni vile hujitambui ...Si rahisi kama hujitambui wewe binafsi hlafu halafu unataka kuleta hoja ambazo hujui kitu

Sina dini mkuu. Intake radhi. Sihitaji dini kumjua na kumuabudu Mungu
 
Kilua ni jina la ki Swahili? Au umemaanisha kulwa?
 
that is how islam is created by them, halafu kijana mbongo wa madongokuinama mchambawima, temeke mikoroshini choo paspoti saizi ugali dona bamia anashupaza shingo hawataki kuambiwa ukweli kuwa wanapumbazwa akili
Ukweli gani wewe!!.. wakristu na wayahudi ndiyo walikua wakifanya mijadala kumpinga mtume akihubiri,kwa hiyo mapadre wakaandika Quran inayosema 'wamekufuru wanaosema hakika ni Mungu masihi mwana wa maryam?..hawakumuua wala kumsulubu..sasa waanzishe uislam dini contrary to christianity Ili iweje?..
 
Sina dini mkuu. Intake radhi. Sihitaji dini kumjua na kumuabudu Mungu
Unayo usianze kulia hapa ni vile hujielewi ,unaabudu mizimu ndiyo dini yako so take care of your iman usilete porojo kwingine inaonekana kama hujiamini kabisa.
Kaa na imani yako usisambaze stori hazina ukweli kwa kunakili.
 
Ni kweli hizi ni hoja mfu kama zile hoja zenu za baadhi ya mashehe wasiojitambua kuwa eti Yesu alivaa kanzu hivyo alikiwa muislam au Yesu alizikwa kwa Sanda hivyo ni muislam. 😀😀😀😀😀
 
Unayo usianze kulia hapa ni vile hujielewi ,unaabudu mizimu ndiyo dini yako so take care of your iman usilete porojo kwingine inaonekana kama hujiamini kabisa.
Kaa na imani yako usisambaze stori hazina ukweli kwa kunakili.
Siabudu mizimu. Natumia akili aliyo nipa Mungu kuishi..
 
Kwamba wakristo waliandika quran na kusema Yesu hakusukubiwa. Kuna vitu vinachekesha sana.
 
Jesuit ni jina tu lakini walikuwepo hata kabla ya Yesu.
Uwongo unakusaidia nini!?


Wakati Yesu anahubiri Yudea ilikiwa chini ya utawala wa Rumi.

Nchini Ureno kitongoji kinacho itwa Fatima kilipewa jina hilo specifically kwa heshima ya Fatima Bint Muhammad
 

Attachments

  • Screenshot_2025-03-13-12-15-36-979.jpg
    254.4 KB · Views: 1
NOMA SANA MKUU
 
Kwanza Kabisa Unaonekana Hata Historia Huifahamu Vizuri (Nisamehe kusema Hivyo)..

Kijiji Cha Fatima au Fateema Kiliitwa Hivyo Si Kutokana Na Mtoto wa Mtume hapana..

Kwanza Nikukumbushe kwanza Kuwa Hispania Na Ureno na Nchi zingine zilikuwa chini Ya Utawala wa Kiislmu Au Islamic Empire Tangu mwaka 711 Mpaka 1249..

Kama Unakumbuka..

Mwaka huo wa 711 nilioutja, Waislamu kutoka kaskazini mwa Afrika, chini ya kiongozi wao anayeitwa Tariq ibn Ziyad, walivamia na kuiteka sehemu kubwa ya Peninsula ya Iberia, yote Ikiwemo Ureno na ikiwa ni pamoja na sehemu ya leo ya Ureno na Hispania.

Katika kipindi chote cha utawala wa Waislamu, Peninsula ya Iberia ilikuwa sehemu ya himaya kubwa zaidi inayoitwa Al-Andalus.Ila baada ya kuingia Karne ya 11 Waidlamu walianza Kuzidiwa Nguvu, Maarifa, na kipindi kinaitwa Reconquista kilianza, ambapo Wakristo walijitahidi kurejesha maeneo yaliyokuwa chini ya Waislamu..Naiamani Unaijua Hii Historia Kama Huijui Kaisome sitaki Kuihadithia Sana..

Turudi kwa Fatima au Fateema..
Kipindi cha Vita ya Waislam na Wakristo kwenye Kuikomboa Ureno Kuna Mwislamu Mwanamke Ambaye yeye alijitoa Kuisaidia Ukristo ipate ushindi na Baadaye aliolewa na Kamanda wa Kikristo aliyeitwa Gonçalo Hermigues..

Mwanamke Huyo alikuwa akitoa Siri Za Waislamu na Kuzipelekwa kwa Kamanda Huyo Na baada ya ushindi Mwanamke huyo aliyekuwa Akitwa Fatima Alibatizwa na Kuwa Mkristo na Sehemu ya Kijiji Ilipewa Jina lake kumuenzi Yeye na Aliolewa na Kiongozi wa Vita..

Na Sio Kama Ulivyoelezea Wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…