Nawasalimu na kwa Jina la JMT,
Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wake wa mambo ya ndani Mhe George Simbachawane wameamua kumaliza utata wa kijadi wa mchezaji wa zamani wa Geita Gold, Mbeya City na Sasa Simba SC Kibu Denis Prosper kwa kutekeleza ombi la Tanzania Football Federation ( TFF),Waziri kwa mamlaka anayopewa na Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002) amemtunuku Uraia kijana huyu machachari na mzalendo wa kweli kwa Taifa lake baada ya Uraia wake kuingia utata wa kishabiki,
Rais Samia kwa kutambua kuwa michezo ni kazi Kama zilivyo kazi nyingine, Michezo ni ajira amepunguza kodi kwenye zawadi ya Ushindi ( Gamming Tax on Winnings ) toka 20% hadi 15% ,Tanzania imetoa vijana zaidi ya 54 kwenda kucheza nje ya nchi huku 32 kati yao wakiwa ni wachezaji Wa mpira wa miguu yaani ( football ),
Mtakumbuka, Michezo ndio sekta inayokuwa kwa kasi zaidi Tanzania mfano mwaka 2017|18 iliongoza kwani ilikuwa kwa 13.7% haya ndio yanamfanya Rais Samia Suluhu Hassan kuitazama michezo|sanaa kama sekta itakayomsadia kukuza utali,Uwekezaji na kutoa Ajira vijana kwani Ilani ya CCM iliahidi kutengeneza ajira 8m ifikapo mwaka 2025,
#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
=====================================
Soma Habari Mbali Mbali za Udaku, Michezo, Siasa, Mapenzi na Mengine Mengi Kutoka Tanzania
Tanzania yampa uraia Denis Kibu, rasmi Simba
Udaku SpecialOctober 03, 2021
Chibu Denis (kushoto) akiwa katika kikosi cha Taifa Stars. Kulia ni John Bocco
WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, amehitimisha sakata la uraia wa Kibu Denis Prosper kwa kutangaza kumpa uraia mchezaji huyo wa Simba. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).
Simbachawene ametumia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), kumpa uraia Kibu.
Uamuzi huo umetangazwa usiku wa Jumamosi tarehe 2 Oktoba 2021 kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo uliyoweka picha ya Kibu na maneno yaliyosomeka;
“Mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa URAIA wa Tanzania Mchezaji wa Mpira wa Miguu, Kibu Denis Prosper, Sept. 30, 2021.”
Waziri Simbachawene ametangaza uamuzi huo ikiwa imepita siku moja tangu, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuibuka na kumtaka, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo akidai linatia aibu Taifa.
Mbali na Majaliwa, Zitto aliwatupia mzigo Waziri Simbachawene na Innocent Bashungwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema, wakiamua wanaweza kuhitimisha suala hilo ndani ya siku moja.
Zitto aliibuka kuzungumzia suala hilo alipofanya mahojiano maalumu na MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online akishangazwa na uamuzi wa Serikali kushikilia hati ya kusafiria ya Kibu ambaye amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mbeya City.
Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) alisema, ilikuwaje Kibu akacheza Mbeya City, timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars “hakuulizwa uraia, ila amesajiliwa tu Simba anaulizwa uraia.”
Kibu anayevalia jezi namba 38 aliyopewa baada ya kusajiliwa Simba, aliicheza Taifa Stars kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi, tarehe 13 Julai 2021, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Stars kuibuka na ushindi wa 2-0.
George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani
Kwenye mchezo huo, Kibu anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alionesha kiwango kinachoridhisha na kuwezesha ushindi huo na baadaye akizungumza na waandishi wa habari alisema “nashukuru sana kwa mara ya kwanza kuichezea timu yangu ya Stars. Wazidi kunipa moyo kwani safari bado ndefu.”
Baada ya uamuzi huo wa Serikali, Zitto ameandika kwenye Instagram yake akipongeza uamuzi huo akisema “nazishukuru na kuzipongeza mamlaka za uraia.”
VIVA TANZANIAN VIVA ||VIVA SAMIA VIVA