Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Rasmi: Kibu Dennis ni Mtanzania

Hakukuwa na haja ya kueleza hayo yote, uhamiaji wangejitokeza kusema jamaa ni mbongo hayo mengine yangebaki kwa watu afu maisha yakaendelea.

Mtu amecheza hadi mechi ya timu ya taifa afu leo ndio unakuja kutangaza kumpa uraia 😂😂
 
Kwani ilikuwa lazima achezee Yanga? Kisa kakataa kusajiliwa Utopoloni mkataka kumkomoa.Utopolo acheni roho mbaya.
Kwa hiyo waliomzuia kucheza ni Yanga, au uhamiaji? Je, ukweli ni upi, amesingiziwa au ni kweli alikua ni mhamiaji haram?
 
Kwa hiyo waliomzuia kucheza ni Yanga, au uhamiaji? Je, ukweli ni upi, amesingiziwa au ni kweli alikua ni mhamiaji haram?
Uhamiaji walikuwa wanafanyia kazi malalamiko ya Yanga yaliyoletwa kwao kupitia TFF
 
Kwa hiyo sasa hivi ni Raia wa kujiandikisha October 2021!
 
Uhamiaji walikuwa wanafanyia kazi malalamiko ya Yanga yaliyoletwa kwao kupitia TFF
Je, hayo malalamiko yalikua yana ukweli, au yalikua ni ya uongo?

Tuachane na ile sababu isiyo na mashiko ya kwamba eti wamekalamika baada ya huyo mchezaji kukataa kusajiliwa na Yanga.
 
Tunajitia Aibu Sana Hili Taifa. Ni bora wasinge Tangaza Chochote na Wangemuonya Kibu Denis kutokusema Chochote. Wangempa Uraia Kimyakimya Kumpa Uraia kwa Matangazo hivi wanaiabisha sanaaa hii nchi Yetu...
Ndo maana Hadi Leo shule ya mwaka 1974 wanafunzi wanasomea chini ya mti viongozi ndo hao wanakaza shingo kwenye mambo ya Simba SC hawajui walifanyalo kufuatilia mambo ya msingi na yenye mashiko KB siyo mtanzania kisa kaja Simba
 
Taarifa aliyoitoa Waziri Anazidi Kujichanganya Tuuu.

Anasema Kibu Denisi Wazazi Wake Walikuwa ni Wacongo waliingia nchini kwa kukimbia Mapigano CONGO wakati Kibu Denis Akiwa na Umri Wa Miaka 6...
Hii nchi hatari taarifa zenyewe hazina majibu toshelez
 
Una uhakika huyo mchezaji amezuiliwa na Yanga, au uhamiaji, tena baada ya kugundua siyo raia wa halali wa Tanzania?
Yani wewe hata ueleweki,, wewe ndo umesema ya kuwa tunatakiwa kuwashukuru yanga na tff kwa kumbaini muhamiaji haramu so ndo maana mimi nikakujibu.

Hao yanga walikuwa wapi siku zote alizocheza geita gold na mbeya city mpaka leo yupo simba ndio mnahoji uraia wake!

Wewe tena unaniuliza una uhakika gani kama huyo mchezaji kazuiliwa na yanga! Yani zilongwa mbali zitendwa mbali..... nyie watu wa yanga mbona mnapenda kujitoa ufaham
 
Je, hayo malalamiko yalikua yana ukweli, au yalikua ni ya uongo?

Tuachane na ile sababu isiyo na mashiko ya kwamba eti wamekalamika baada ya huyo mchezaji kukataa kusajiliwa na Yanga.

Hilo swall waulizwe waliomjumuisha kwenye Kikosi cha Taifa Stars,maana nijuavyo wachezaji wa Taifa Stars ni Raia wa Tanzania na si vinginevyo.
 
Basi sawa. Wasalimie sana Moo na Barbra.

IMG-20211003-WA0001.jpg


IMG-20211003-WA0002.jpg
 
Tunajitia Aibu Sana Hili Taifa. Ni bora wasinge Tangaza Chochote na Wangemuonya Kibu Denis kutokusema Chochote. Wangempa Uraia Kimyakimya Kumpa Uraia kwa Matangazo hivi wanaiabisha sanaaa hii nchi Yetu...
Hizi ndo comment za GREAT THINKERS Msomi wa JF[emoji106]
 
Nawasalimu na kwa Jina la JMT,


Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wake wa mambo ya ndani Mhe George Simbachawane wameamua kumaliza utata wa kijadi wa mchezaji wa zamani wa Geita Gold, Mbeya City na Sasa Simba SC Kibu Denis Prosper kwa kutekeleza ombi la Tanzania Football Federation ( TFF),Waziri kwa mamlaka anayopewa na Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002) amemtunuku Uraia kijana huyu machachari na mzalendo wa kweli kwa Taifa lake baada ya Uraia wake kuingia utata wa kishabiki,

Rais Samia kwa kutambua kuwa michezo ni kazi Kama zilivyo kazi nyingine, Michezo ni ajira amepunguza kodi kwenye zawadi ya Ushindi ( Gamming Tax on Winnings ) toka 20% hadi 15% ,Tanzania imetoa vijana zaidi ya 54 kwenda kucheza nje ya nchi huku 32 kati yao wakiwa ni wachezaji Wa mpira wa miguu yaani ( football ),

Mtakumbuka, Michezo ndio sekta inayokuwa kwa kasi zaidi Tanzania mfano mwaka 2017|18 iliongoza kwani ilikuwa kwa 13.7% haya ndio yanamfanya Rais Samia Suluhu Hassan kuitazama michezo|sanaa kama sekta itakayomsadia kukuza utali,Uwekezaji na kutoa Ajira vijana kwani Ilani ya CCM iliahidi kutengeneza ajira 8m ifikapo mwaka 2025,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI

=====================================


Tanzania yampa uraia Denis Kibu, rasmi Simba
Udaku SpecialOctober 03, 2021

Chibu Denis (kushoto) akiwa katika kikosi cha Taifa Stars. Kulia ni John Bocco

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, amehitimisha sakata la uraia wa Kibu Denis Prosper kwa kutangaza kumpa uraia mchezaji huyo wa Simba. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).

Simbachawene ametumia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), kumpa uraia Kibu.

Uamuzi huo umetangazwa usiku wa Jumamosi tarehe 2 Oktoba 2021 kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo uliyoweka picha ya Kibu na maneno yaliyosomeka;

“Mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa URAIA wa Tanzania Mchezaji wa Mpira wa Miguu, Kibu Denis Prosper, Sept. 30, 2021.”

Waziri Simbachawene ametangaza uamuzi huo ikiwa imepita siku moja tangu, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuibuka na kumtaka, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo akidai linatia aibu Taifa.

Mbali na Majaliwa, Zitto aliwatupia mzigo Waziri Simbachawene na Innocent Bashungwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema, wakiamua wanaweza kuhitimisha suala hilo ndani ya siku moja.

Zitto aliibuka kuzungumzia suala hilo alipofanya mahojiano maalumu na MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online akishangazwa na uamuzi wa Serikali kushikilia hati ya kusafiria ya Kibu ambaye amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mbeya City.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) alisema, ilikuwaje Kibu akacheza Mbeya City, timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars “hakuulizwa uraia, ila amesajiliwa tu Simba anaulizwa uraia.”

Kibu anayevalia jezi namba 38 aliyopewa baada ya kusajiliwa Simba, aliicheza Taifa Stars kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi, tarehe 13 Julai 2021, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Stars kuibuka na ushindi wa 2-0.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani
Kwenye mchezo huo, Kibu anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alionesha kiwango kinachoridhisha na kuwezesha ushindi huo na baadaye akizungumza na waandishi wa habari alisema “nashukuru sana kwa mara ya kwanza kuichezea timu yangu ya Stars. Wazidi kunipa moyo kwani safari bado ndefu.”

Baada ya uamuzi huo wa Serikali, Zitto ameandika kwenye Instagram yake akipongeza uamuzi huo akisema “nazishukuru na kuzipongeza mamlaka za uraia.”

VIVA TANZANIAN VIVA ||VIVA SAMIA VIVA

Screenshot_20211004-153733.png
 

Rais Samia ampa Uraia Kibu Denis Prosper mchezaji machachari wa Taifa Stars na Simba | Hakika hii ndio Serikali rafiki wa michezo na wanamichezo wote​


Screenshot_20211004-091224.png
 
Back
Top Bottom