PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Shughuli zote zinasimamishwa kivipi?
Uamuzi huo ni jaribio lingine la kuidhibiti Chadema. Chama kinaadhibiwa na wenye mamlaka.

Ushauri wangu: Chadema lazima mjue mamlaka mmeishika pabaya, na kuna watu wenu mliokuwa nao wameshachukua vipande vya fedha. Kuweni makini hasa kwenye mashauri, yule mama halali juu yenu kwa hiyo msifikiri mpo salama.
Wasilisheni pingamizi maamuzi ya Jaji, na pelekeni motion ya kutokuwa na imani na Jaji huyu ni kitengo.
 
Chama Cha Ma..🤔
Nimesahau kumalizia
Hicho hicho unachowaza malizia
 
Waislamu sikuzote utumika kipumbavu .....😁😁 ni hatari nchi kuongozwa na waislamu hakuna tofauti kubwa baina ya muislamu na mwanamke kwenye mambo ya uongozi ....siku zote wanawake na waislamu huwa awana uzalendo
Kakojoe ukalale wewe unamjua aliyeleta uhuru nchi hii?

Tafuta kumi Bora waliyoleta uhuru nchi hii alafu niambie wakristo walikuwa wangapi?

Kwa Sasa nyinyi CHADEMA kinachokusumbueni ni udini na ukabila na uchu wa madaraka ndio maana sisi tumekaa tunakuangalieni tu
 
Ni mwanadamu kujaribu kusema hapana kwenye jambo la Mungu kitu ambacho ni kuandika sifuri na kufuta oo wakati huo huo useme nimeandika sifuri sasa
 
Hii mbinu ilitarajiwa, na muda wake umefika.
Je ahueni kwa CCM itapatikana baada ya mpinzani kutokuwepo uwanjani?
 
Ukisikia wanasema ccm imejificha nyuma ya serikali ndio kama hivyo. Tundu Lissu wamemfanyia hujuma kumuweka mahabusu ili tu wasipate upinzani wakaona haitoshi wameamua kuifungia CDM. Swali la msingi ni kwanini wanafanya hivyo katika kipindi ambacho kunatarajiwa kufanyika uchaguzi mkuu ambao CDM wameukataa?

Ccm kwa kushirikiana na serikali na mibimili yake inachochea uvunjifu wa amani kwa sababu tu ya maslahi ya watu wachache wanaoona wana haki ya kuongoza Tanzania peke yao.
 

NO REFORMS, NO ELECTION!
 
Mbona joto kubwa sana kwa watawala? Usikute hii nchi haijawahi kuwa na upinzani wa kweli kama ambavyo ilivyo hivi sasa?😅😅

Ni nini hasa kinachowaogopesha? Kama mmekua madarakani kwa miaka 30 tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ufanyike ambayo ni sawa na round sita, na katika round zote hizo mlishinda inakuaje sasa hivi ni kama kuna kauoga fulani hivi kasiko ka moja kwa moja mnakaonesha?

Huwezi kuwa mashindi wa kweli ukaogopa mabadiliko madogo kama hayo ambayo watu wanayataka ili wajiridhishe ya kwamba ni kweli kura zao huwa zinapata thamani ile ile ambayo wao wanaitarajia au laa.

Nchi yetu ni nchi iliyojaliwa wazee wenye busara nadhani ni muda sasa na wao wakajitokeza ili waweze kusema jambo juu ya mambo haya, kwa maana hivi sasa ni kama tunajiendea endea tu, na maamuzi mengi ukiyafikiria sana unaona mbona kama huu uamuzi umefanyika kimihemko zaidi ya busara.

Tunajua kuna wazee wetu wamepata heshima ya udokta kutokana na busara zao za kusuluhisha migogoro kadha wa kadha katika maeneo mbalimbali sasa nadhani ndio muda wa kuonesha uwezo wao na kutuprove kwamba heshima hizo ambazo walitunukiwa hazikua kwa bahati mbaya bali ni kweli wanao huo uwezo.
 
Hatimaye shetani azidi kukita mizizi,kwa hofu kuudhidi ya Chadema.Na juu ya hofu ya madai ya haki na usawa kwenye taifa letu.Mbeleko ni zilezile za kishetani zikisaidiana na waliotakiwa kuwa walinzi wa haki amani na umoja wa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…