Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

kaka unatumia nguvu kubwa sana kusoma script za maigizo ya watu.

nimeziita script kwasabb ni mambo ya kutungwa tu
Hujathibitisha kuwa ni mambo ya kutungwa tu.

Naweza kukwambia kuwa wewe kusema haya ni mambo ya kutungwa tu ndiyo jambo la kutungwa tu.

Kwa sababu hujathibitisha kuwa haya ni mambo ya kutungwa tu.

Yani si tu hujathibitisha kuwa haya ni mambo ya kutungwa tu, hujathibitisha hata kama umeyasoma, achikia mbali kimuyaelewa.

Unaongelea vitu ambavyo huvielewi, hujavisoma, huwezi kuvichambua kimantiki.

Pengine huna hata uwezo wa kuvichambua kimantiki.
 
Tunasema hivi;
AMINI MUNGU YUPO, HATA UKIFANIKIWA KWENDA MBINGUNI NA UKAMKUTA ISIKUGHARIMU, KULIKO KUAMINI HAYUPO ALAFU UKAMUONA NDIYE HUYU HAPA!.
Mbingu haipo.

Huyo Mungu kama yupo kwa nini anajificha halafu anataka kuaminiwa yupo akiwa mafichoni?

Huyo Mungu akijitokeza hadharani akajulikana yupo na kutambulika yupo, itamcost nini?

Au huyo Mungu anacheza kombolela
na binadamu?

Kwamba anajificha mafichoni, Halafu anataka sisi tuzinge kumtafuta..😆
 
Haya uliyoyasema hapo ndio nataka uyathibishe
Nikuthibitishie kupitia nini?

Kwani wewe jua hulijui?

Kwani wewe hujawahi kuliona jua?

Sasa unataka uthibitisho gani kwamba jua lipo?

Kama jua lipo si kwamba lilikuwepo ndio maana umeweza kulikuta lipo?

Kama jua lisingekuwepo, ungelikuta lipo?

Si ungekuta halipo?

Jua lilikuwepo ndio maana umelikuta lipo.

Sasa unataka nini zaidi?
Nani aliyekuambia kuwa jua lilikuwepo milele na litaendelea kuwepo milele?
Logic.
Kwani useme na kuamini vitu ambavyo hauwezi kukithibisha?
Unataka uthibitisho wa kitu gani?

Jua tayari lipo.

Sasa unataka nini zaidi?
Au na wewe upo katika kundi la viumbe ambavyo Kuna vitu hawawezi kukithibisha?
Kila kitu kilichopo except man-made things ni uthibitisho tosha kwamba kilikuwepo.

Kama kisingekuwepo, Usingeweza kukuta kipo.
 
Kwa hiyo mimi nimekufa?

Kama siishi nafanyaje?

Hebu eleza hapa.

Pia ni kichaa pekee ndio ataamini Mungu alitokea from Nothing.
Inawezekana nachat na AI, wewe unaweza kuthibitisha vipi kama Mimi sasa hivi ninaishi? Una uhakka gani kama huoti? Niambie umejuaje kama Mimi ni mtu Niko hai na siyo AI
 
Inawezekana nachat na AI, wewe unaweza kuthibitisha vipi kama Mimi sasa hivi ninaishi? Una uhakka gani kama huoti? Niambie umejuaje kama Mimi ni mtu Niko hai na siyo AI
Basi umekufa.

I rest my case.
 
Atheists wanasumbuka Sana.

Hawana utulivu wa nafsi, muda wote wanapeleleza kuona kwamba kwenye dini Kuna Jambo la miujiza wa wazi unaoweza kurudisha imani zao zilizopotezwa lkn wanakuta hakuna. Wala hawachoki kupeleleza na wataendelea hivyo maisha yao yote. Poleni bandugu!
 
Theists ndio mnasumbuka sana.

Kila mara mnakazana sana kuelezea habari za huyo Mungu, mara Allah, mara Yesu n.k

Kila mara nyuzi za mabishano kuhusu Allah, Yesu, Mudi, Biblia na Quran haziishii hapa JF.

Kwa hiyo ninyi waamini Mungu (Theists) ndio hamtulii. Mnapata utata kila mara na hizo imani zenu.

Ndio maana mnakuwa na mabishano yasioisha.
 
Mungu ndiye kaumba viumbe vyote ukiwemo na wewe...

Mpe heshima yake aliyekuumba
Ni wewe tu unafosi na kulazimisha iwe hivyo. Lakini Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Hata wewe hukuumbwa na huyo Mungu, Umezaliwa kutoka kwa wazazi wako.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Waafrika mnahangaika kweli na dini za wakoloni, yaani uende mbinguni kwa dini za wakoloni? Ambazo wamezileta kwa maslahi yao , Huo ulokole wenu Ina maana dini zingine amboko ukristo na uislamu haupo hawaendi mbinguni, dini ya Tao , Hindu, Shinto , Buddha, Shaman hawa wote hawaendi mpaka waingie kwenye dini zenu na hawa ni wengi kuliko nyinyi kwa Mungu wenu atawapeleka motoni wote? So ndio walokole ?
 
Nikuthibitishie kupitia nini?

Kwani wewe jua hulijui?

Kwani wewe hujawahi kuliona jua?

Sasa unataka uthibitisho gani kwamba jua lipo?

Kama jua lipo si kwamba lilikuwepo ndio maana umeweza kulikuta lipo?

Kama jua lisingekuwepo, ungelikuta lipo?

Si ungekuta halipo?

Jua lilikuwepo ndio maana umelikuta lipo.

Sasa unataka nini zaidi?

Logic.

Unataka uthibitisho wa kitu gani?

Jua tayari lipo.

Sasa unataka nini zaidi?

Kila kitu kilichopo except man-made things ni uthibitisho tosha kwamba kilikuwepo.

Kama kisingekuwepo, Usingeweza kukuta kipo.
Kwa haya majibu yako tayari umeshajijua kuwa wewe ni kiraza

Kwa kuwa wewe ni kiraza hata ukisema hakuna Mungu sawa tu
 
Theists ndio mnasumbuka sana.

Kila mara mnakazana sana kuelezea habari za huyo Mungu, mara Allah, mara Yesu n.k

Kila mara nyuzi za mabishano kuhusu Allah, Yesu, Mudi, Biblia na Quran haziishii hapa JF.

Kwa hiyo ninyi waamini Mungu (Theists) ndio hamtulii. Mnapata utata kila mara na hizo imani zenu.

Ndio maana mnakuwa na mabishano yasioisha.
Hakuna utata zaidi yakukusikitikia ulivyo mbali na ukweli. Mungu anawapenda japo mnamtoa kasoro kibao mkitamani angefanya mnavyopenda. Hata hivyo kimoyomoyo mnakubali kazi na kutaka aonekane ili mumpe maua yake.

Lkn hawezi kuonekana Mr. Utachosha akili yako.
 
Hahaha ikitokea Mungu akaonekana sijui mtasujudu, au mtaendelea kukaza tu kwamba hatukumtaka wa hivi.

Acheni ulevi.
 
Ila bange 🤣🤣🤣🤣, Mtu umepiga paf zako 10 akili inakuambia andika verse moja ya kuwaaminisha watu Mungu hayupo.

Yaani hii verse yako moja ndo unataka ishinde hoja zote zilizo katika maandiko yote na imani za watu.

Ni kush gani hiyo?
 
Ni wewe tu unafosi na kulazimisha iwe hivyo. Lakini Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.

Hata wewe hukuumbwa na huyo Mungu, Umezaliwa kutoka kwa wazazi wako.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
Kama hicho kisimu chako cha kichina ki creator mtu aliye kiunda kina systems kadhaa ambazo ni simple systems kama chaji,sauti na mifumo mingine vipi kuhusu wewe usiwe na creator ambaye ni zaidi ya genius ambaye katengeneza jinsi ulivo bora na unamifumo ming na very complicated na akakupa na mifumo had ya ufahamu ila umeamua kuwa kilaza inasikitisha sana🥹
 
It's biblical teachings that I apply in my daily life activities
How can you apply something you don't believe? It's called blind faith. So ukubali wewe ni mtumwa wa kufuata kitu usicho kijua.
Namfahamu kwa mambo mengi
Si ndo hayo ya kwenye bible ambayo ni religious dogma?
Kama sivyo elezea dhana nyingine ya Mungu unayosema unaijua..
 
Kuwa atheist akili inakataa kwani yapo mambo mengi ambayo ulimwengu xa phenomena hauwezi kujustify.Lakini noumena(ulimwengu usiomekana) inatoa majibu.Ninapoungana na mleta mada ni namna ya mimi kulink na noumenic world kwani inatia shaka na kujiuliza:Kabla ya ukoloni Mwafrika hakuwa akiabudu?Kama alikuwa akiabudu alitumia mfumo huu wa miungu ya kigeni?Kusudi hasa la kuabudu lilikuwa ni nini?Kwa fikira pevu twamuona Mwafrika kapotea kiimani na hajui anachokiabudu.
 
Kuna watu ni wajinga wanaamini kabisa kwamba Kuna mungu utakuta mtu amefanyiwa ubaya na binadamu mwenzie eti namuachia mungu halafu Kwa mujibu wa dini huyo huyo mtu alienda kutubu anasamehewa aisee zindukeni dini na neno mungu limetungwa na matapeli Ili waweze kuitawala dunia ikiwemo kuanzisha dini zao uchwara na kweli wajinga ambao ni masikini wanaendelea kuteswa Kwa vitisho vya kuchomwz moto ilihali wanaona kabisa wakifa wanazikwa ardhini.
Kila mtu ashinde mechi zake 😁😁
 
Mungu ni mwanga. Unapokataa mwanga, unakuwa umejiingiza gizani. Utembeapo gizani utajikwaa na kuumia.
 
Back
Top Bottom