Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

Pole sana.
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?

Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba kuna watu watakuja kutokumwamini Awadhibiti na kuwazuia mapema wasiwepo duniani?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote na wakati wote?

Mungu anayedaiwa kwamba ni mkamilifu, Kwa nini aliumba binadamu wasio mwamini na wenye uwezo wa kumkufuru?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
"Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu". Kusema moyoni mwako hakuna gharama yoyote unaweza sema vyovyote unavyosikia ni takwa la kikatiba kabisa.
Mtoa mada Jibu hili swali, unaweza kwenda katikati ya mji ukakuta gari lime park ukasema umeliokota?. Unaweza kusema umeokota nyumba?. Ikiwa ni hapana basi hakuna kisicho na mmiliki hata wewe kuna nguvu iliyo na NENO la mwisho kwako ikisema ufe hakuna daktari, pesa, uwezo, elimu ya kidunia inayoweza kupinga na huyo ni Mungu.
 
Tukirudishwa nyuma watu wote yaani kwenye matumbo ya mama zetu na viunoni mwa baba zetu,huoni kuwa kuna chanzo au asili ya mwanadamu?.
Hapo ndo kuna chanzo cha dini pia.
 
Acha nipumbazwe,hivi wewe kutoamini uwepo wa mungu kunakusaidiaje,zipi faida wapata!!?,,na mi unadhani hasara gani napata kwa kuamini uwepo wa mungu?
Uamini Mungu, Usiamini Mungu vyote ni sawa. Hakuna faida wala hasara yeyote inayo patikana. Kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Kama ni kufa wote tutakufa, Haijalishi unamwamini Mungu au haumwamini.

Kama ni shida, matatizo na majanga. Vyote vinawapata waamini Mungu na wasio waamini Mungu.

Hivyo huyo Mungu aaminiwe, asiaminiwe hana effect yeyote.
 
Kuna kinyozi alikuwa akimnyoa mteja akasema Mungu hayupo kama yupo kwa nini watu wanakufa, wanaugua, maskini, n.k yule mteja akawa kimnya tu
Gafla akatokea kichaa nywele ndefu, chafu, ndevu kama zote, kucha ndio kabisa.

Yule mteja akasema hivi kuna vinyozi kweli?. Hakuna vinyozi hebu angalia Yule kichaa alivyo na minywele yote ile na mindevu kweli hakuna vinyozi. Yule kinyozi akawaka akasema vinyozi tupo si nipo hapa akamuuliza mbona Yule Ana nywele ndefu?. Akasema ni kwa sababu hajaja kwangu aje nitamnyoa.
Yule mtu akasema Mungu yupo kuhusu uweza wake wa kuponya, kutajilisha n. K ni kwa sababu watu hawamuamini ili awaponye na kuwainua. Hivyo asiyeamini Mungu ni kama kichaa Yule aliyepungukiwa akili asiyaamini maji kumsafisha, kinyozi kumnyoa, na wembe kuondoa kucha. Asante
 
 
"Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu".
Mpumbavu amesema moyoni mwake, Kuna Mungu.
Kusema moyoni mwako hakuna gharama yoyote unaweza sema vyovyote unavyosikia ni takwa la kikatiba kabisa.
Hata wewe kusema kwamba kuna Mungu ni uhuru wako wa kikatiba kufanya hivyo.

Ila ukianza kudai kwamba hiyo imani yako ya uwepo wa Mungu ina ukweli lazima uthibitishe hilo.
Kama hakuna kisicho na mmiliki, Mmiliki wa huyo Mungu ni nani?

Kwa nini unafosi kila kitu kilichopo lazima kiwe na mmiliki, Halafu una mu exclude huyo Mungu kwenye kuwa na mmiliki?

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mmiliki, Hata huyo Mungu lazima awe na mmiliki.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mmiliki, Hata Dunia na vyote vilivyomo except man-made things, Havina mmiliki.
 
Hizi ni stori uchwara zisizo na uthibitisho wowote ule.

Mnatunga vistori uchwara kutetea uwepo wa Mungu ambaye hayupo kujitetea mwenyewe.

Huyo Mungu kama yupo, Ajitokeze hadharani yeye mwenyewe ajidhihirishe yupo, Kama ana huo uwezo.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumtetea huyo Mungu aonekane yupo kumbe hayupo.

Huyo Mungu kama yupo, Anacho jifichia huko alipo ni nini?

The fact that an almighty God and all powerful God needs humans to speak for him and defend him kinda proves his non-existence.
 
Mazombi hakuns kitu wanaelewa, vunga tu ndugu yangu wajinga ni mtaji ishi nao vizuri uendelee kuwapiga vibunda.
 
Mimi mtu akiweza tu kunijibu yeye Mungu alitoka wapi, na kwanini anapenda sifa nitamsikiliza.
Afu kwanini atuchonganisje na Shetani?
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 
Swali, wewe hutaki kua na afya bora muda wote, kua na amani na utajiri?
Umeenda kwa Mungu vipi amekupa Shi ngapi mpaka sasa ambazo sisi hatuna?
 
Hizo alinacha zako ndiyo proof yako kuwa huyo Mungu wako exists? So pathetic.
 
Tofautisha dini na kuamini Mungu, Kuamini uwepo wa Mungu ni imani inayokaa ndani ya mtu kwa asili. Sio lazima uwe na dini maalum ili uamini uwepo wa Mungu.

Isaac Newton, Albert Einstein and many other great scientists believed in the existence of God. Halafu unakuja na blah blah za facts mara logic sijui reasoning...
 
I could feel that mkuu πŸ˜….

Ulichosema ni sahihi, Atheism inahitaji knowledge na sio kuendeshwa na mihemko.

Atheism inahitaji Knowledge gani ?

Sababu wakana Mungu wote wanafikiri kitoto sana, na ni wadhaifu sana kwenye kujenga hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…