Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

Rasmi nimeligundua hili, Mungu na Shetani hawapo: Dini ni utapeli

Kama ametupa uhuru wa kuchagua mema na mabaya, Kwa nini sasa anakasirika akitendewa mabaya.

Kama huyo Mungu hapendi mabaya, kwa nini akupe uhuru na uwezo wa kutenda mabaya?

Huyo Mungu Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote?

Kama huyo Mungu "He couldn't create us righteous" basi hana uwezo wa vyote.

Na kama huyo Mungu alitupa freedom yakuchagua right and evil path, Basi hapaswi kuingilia freedom ya watu watakaochagua evil path.

Pia huyo Mungu akae kwa kutulia asikasirike akiona watu wanatenda evils.

Maana yeye mwenyewe ndio kaweka uhuru wa kuchagua njia yeyote, Evil au right.

Kwa nini huyo Mungu aliumba binadamu ignorant?

Kama huyo Mungu alitaka sisi tuwe purely free, Basi akae kwa kutulia akufuriwe vya kutosha.

Maana si aliyataka mwenyewe.

Kama alikuwa hataki binadamu wafanye mabaya, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote na wakati wote?
Infropreneur I'm being Open minded and respectfuul kuheshimu mawazo Yako and trying to understand why you don't believe if God exits na kumkufuru...
What did he do to offend you?!
Usisahau na mazuri aliyokufanyia
Since nobody has ever asked you this before allow me to know
 
Kuna watu ni wajinga wanaamini kabisa kwamba Kuna mungu utakuta mtu amefanyiwa ubaya na binadamu mwenzie eti namuachia mungu halafu Kwa mujibu wa dini huyo huyo mtu alienda kutubu anasamehewa aisee zinduke I dini na neno mungu limetungwa na matapeli Ili waweze kuitawala dunia ikiwemo kuanzisha dini zao uchwara na kweli wajinga ambao ni masikini wanaendelea kuteswa Kwa vitisho vya kuchomwz moto ilihali wanaona kabisa wakifa wanazikwa ardhini
Umechelewa sana.
 
Infropreneur I'm being Open minded and respectfuul kuheshimu mawazo Yako and trying to understand why you don't believe if God exits na kumkufuru...
What did he do to offend you?!
Usisahau na mazuri aliyokufanyia
Since nobody has ever asked you this before allow me to know
Mungu anayedaiwa kwamba ni mwema sana, mpole na mwenye upendo na huruma.

Ameshindwa kabisa kuwasaidia maelfu ya watoto na wanawake waliokufa na wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa, umaskini na majanga mbalimbali ya asili kama vile ukame, vimbunga, mafuriko, matetemeko ya ardhi, Radi n.k

Licha ya wanawake hawa na watoto kusali sana, kuomba sana, kufunga sana na kumlilia sana huyo Mungu kumuomba awasaidie. Lakini Holaaaa!!! Huyo Mungu hajawahi kuonekana kusaidia chochote. Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wameangamia.
JamiiForums1832832046.jpeg
FB_IMG_1722976782305.jpg
JamiiForums-890530179.jpeg
JamiiForums907565714.jpeg

Sasa huyo Mungu ana wema gani?

Huyo Mungu ana msaada gani?

Huyo Mungu ana huruma gani?

Huyo Mungu kwa nini aumbe viumbe vije viteseke kwanza duniani, Halafu eti baadae ndio aje kuwapa raha huko mbinguni?

Huyo Mungu kwa nini anaacha viumbe vikiteseka duniani, Halafu yeye anakula bata huko mbinguni?
Halafu akiombwa aje atoe msaada japo kidogo hapa duniani, Hatokei na haonekani?????????

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?

Huyo Mungu kama yupo, Basi ni Mungu mkatili, muuaji, muovu, bandidu, sadist, nunda, dikteta na hana hata chembe ya huruma.

Mungu huyo hafai kabisa anastahili kufurushwa huko alipo.
FB_IMG_1710533066467.jpg
 
Kua hai na kuishi ni haki yako ya msingi, ulevi ni ujinga wako.
Mambo ya kuketi na wakuu ni hustle zako na jinsi unavyobehave.
Mambo mengi yamekaa kibinadamu sana lakini Watu wa Iman mnayakuza na kuyafanya kama Magic kiasi cha kuyatolea sadaka ndo utumwa wenyewe huo.
Kumbuka taifa la Israel lilikuwa si kitu baba Yao Yakobo alikuwa mtoto wa mama na nduguye Esau alikuwa mchakalikaji kama usemavyo Ila kwa kumtegemea Mungu alimpita kaka yake na Leo hakuna taifa kama Israel
 
Kama ubongo ndio ufao kwa nini msiukarabati kama injini ya pikipiki ukarudie uhai tena.
Mtu akifa viungo vyake vya mwili huacha kufanya kazi.

Ubongo 🧠 na moyo huacha kufanya kazi. Hivyo viungo vingine vyote vya mwili huacha kufanya kazi.

Hakuna roho hapo.

Ni ubongo 🧠 umeacha kufanya kazi.
 
Bado teknolojia hiyo haijafanikiwa.

Huenda kwa siku za mbeleni ikawezekana kufanya hivyo.

Hatujui tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua Kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.
Ndio ujue yuko Mungu yako mengi msiyoyajua wala hamtoyajua kamwe.
 
Mungu yupo na shetani yupo,siku zaja ambazo kila ulimi utakili kwamba,Hakika hukumu zako na Sheria zako ni za Haki Eeh Mwenyezi Mungu!
 
Ndio ujue yuko Mungu yako mengi msiyoyajua wala hamtoyajua kamwe.
Ulijuaje huyo Mungu yupo?

Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Sio kufosi imani yako uliyoaminishwa na kupumbazwa.
 
Kuthibitisha ni uhai wako!
Uhai unathibitisha vipi uwepo wa Mungu?

Mthibitishe huyo Mungu, yeye kama yeye.

Au huyo Mungu kama ana uwezo ajitokeze mwenyewe hadharani ajidhihirishe na kujitetea.

Sio ninyi mnahangaika kumwelezea na kumtetea hapa.

Huyo Mungu aje mwenyewe ajitetee kama ana huo uwezo.
 
Mungu yupo na shetani yupo,siku zaja ambazo kila ulimi utakili kwamba,Hakika hukumu zako na Sheria zako ni za Haki Eeh Mwenyezi Mungu!
Mungu hayupo.

Shetani hayupo.

Mungu na Shetani mmewatunga vichwani mwenu tu. Ndio maana hamuwezi kuthibitisha uwepo wao.

Kama Mungu na Shetani wapo, Wajitokeze hadharani wenyewe wajiongelee na kujitetea.

Sio ninyi mnahangaika kuwatetea na kuwaelezea.

Kwani wao hawana uwezo wa kujitetea wenyewe?
 
Kuna ongezeko la nyuzi za kukufuru, vijana mkishiba halafu hakuna sehemu ya mwili inauma unajihisi unaweza Kila kitu. Ila ipo ile siku inakuja, unajua kwanini hospitalini wanakuwa na namba za simu za viongozi wa dini?? Tena zinabandikwa kwenye ubao pale kwa nesi wa zamu
 
Mungu anayedaiwa kwamba ni mwema sana, mpole na mwenye upendo na huruma.

Ameshindwa kabisa kuwasaidia maelfu ya watoto na wanawake waliokufa na wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa, umaskini na majanga mbalimbali ya asili kama vile ukame, vimbunga, mafuriko, matetemeko ya ardhi, Radi n.k

Licha ya wanawake hawa na watoto kusali sana, kuomba sana, kufunga sana na kumlilia sana huyo Mungu kumuomba awasaidie. Lakini Holaaaa!!! Huyo Mungu hajawahi kuonekana kusaidia chochote. Maelfu ya watu hasa wanawake na watoto wameangamia.
View attachment 3206933View attachment 3206934View attachment 3206936View attachment 3206937

Sasa huyo Mungu ana wema gani?

Huyo Mungu ana msaada gani?

Huyo Mungu ana huruma gani?

Huyo Mungu kwa nini aumbe viumbe vije viteseke kwanza duniani, Halafu eti baadae ndio aje kuwapa raha huko mbinguni?

Huyo Mungu kwa nini anaacha viumbe vikiteseka duniani, Halafu yeye anakula bata huko mbinguni?
Halafu akiombwa aje atoe msaada japo kidogo hapa duniani, Hatokei na haonekani?????????

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?

Huyo Mungu kama yupo, Basi ni Mungu mkatili, muuaji, muovu, bandidu, sadist, nunda, dikteta na hana hata chembe ya huruma.

Mungu huyo hafai kabisa anastahili kufurushwa huko alipo.
View attachment 3206938
Mungu atusaidie
 
Kuna ongezeko la nyuzi za kukufuru, vijana mkishiba halafu hakuna sehemu ya mwili inauma unajihisi unaweza Kila kitu. Ila ipo ile siku inakuja, unajua kwanini hospitalini wanakuwa na namba za simu za viongozi wa dini?? Tena zinabandikwa kwenye ubao pale kwa nesi wa zamu
Infropreneur umeshiba eh ndo maana unapata ujasiri wa kumkana Mungu
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?

Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba kuna watu watakuja kutokumwamini Awadhibiti na kuwazuia mapema wasiwepo duniani?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote na wakati wote?

Mungu anayedaiwa kwamba ni mkamilifu, Kwa nini aliumba binadamu wasio mwamini na wenye uwezo wa kumkufuru?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Mbana maswali yako rahisi sana Kwa sisi watu tunayemjua Mungu na kumuamini?

1) Mungu ameumba malaika hawajui kumuasi Mungu Wala kukumkuru Mungu hivyo ndivyo alivyo waumba
Malaika hawana option ya kutenda maovu

2) Akaumba binadamu na majini akawapa option ya kuchagua aidha afanye mabaya au mazuri

Na akateua miongoni mwa binadamu na majini kuwapelekea ujumbe wenzao kuwa mkifanya maovu Kuna moto na mkifanya mazuri Kuna pepo na haya maisha ya Dunia ni ya kupitia tu ila Kuna maisha ya milele Baada ya haya maisha ya Dunia

Akili aliyepewa binadamu inauwezo wa kumuongoza akaenda anapotaka kama ni motoni au peponi

Siku ilipotungwa mimba yako ulikuwa maiti alafu ukapewa uhai na kuanza maisha tumboni mwa mama yako na hatimaye hapa Duniani

Ipo siku utakuwa tena maiti

Na ipo siku utakuwa hai tena na huo ndio utakuwa uhai wa milele

Mwenyezi Mungu ni nani?

Quran 2:255
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.
 
Back
Top Bottom