Kwa nini huyo Mungu atoe option ya kuchagua mazuri au mabaya ilhali yeye hapendi mabaya?
Kama huyo Mungu hapendi mabaya, Kwa nini hakuweka option ya kutenda mazuri tu?
Kama huyo Mungu hapendi mabaya, kwa nini aweke option ya kuweza kutenda mabaya?
Kulikuwa na haja gani kuumba maisha ya kupita, ilhali kuna maisha ya milele?
Kulikuwa na haja gani kuumba viumbe na binadamu vije viteseke kwanza duniani, Halafu eti baadae ndio tuje tupate raha huko mbinguni?
Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Kama una amini akili yako tu ndio inakuongoza na ndio ina uwezo, Kwa nini unahangaika kusali na kumuomba huyo Mungu?
Ninyi si ndio mna amini maisha yenu yote ni God's plan?
Kama una amini maisha yako yote ni God's plan, Kwa nini unasema tunaongozwa na akili zetu?
Mimba ikitungwa sio maiti. Acha upotoshaji.
Inaonekana hata Biology hukusoma.
Hizi ni hadithi na hekaya za vitabuni tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
Kutumia Quran kama uthibitisho wa uwepo wa Mungu ni sawa na kutumia Comic book kusema ndio uthibitisho wa uwepo wa Harry Potter.
1) wewe hauna mabaya ya kufanyia Mungu
Unaweza kufanya Mabaya kuifanyia
binadamu mwenzako
Au utafanya mabaya kuifanyia nafsi yako Kwa mfano unapopinga uwepo wa Mungu hapo unafanya mabaya lakini unaifanyia nafsi yako maana nafsi yako ndio itakayoadhibiwa Kwa hilo
2) Pia nimesha kuambia Mungu uwezo wa kuumba viumba wasiotenda mabaya anao na viumbe hao ni malaika
3) Option uliyopewa
Yani hayo unayosema na kuamini kuwa Mungu hakuna hiyo ndio inaitwa option ambayo wewe umepewa na malaika hawakupewa
4) Akili uliyopewa unaweza kuitumia vizuri ikakupeleka peponi na unaweza kuitumia vibaya ikakupeleka motoni ndio hiyo option
Mungu anasema ndani ya Quran mtu anayeitumia vizuri akili yake akiamka asubuhi akiona jua linavyochomoza na kuzama jioni anajua kuwa Mungu yupo
Sasa kama wewe Kila siku unaliona jua linachoma jioni linazama haujui Wala haufikilii kuhusu hilo basi akili yako umeshindwa kuitumia vizuri
5) Tafuta kwanza definition ya Maiti
Kwa kukusaidia mimba inaputunga unakuwa maiti Hadi siku ambayo moyo wako unaanza kudunda ndio unakuwa hai na kuanza movement za hapa na pale
Na siku moyo wako ukiacha kudunda unakuwa umerudi kuwa maiti
6) Quran ndio kitabu pekee Kwa Sasa kilichopo hapa Duniani ndio kinatoa definition ya kwali kuhusu Mungu
Na hata nyinyi ambao mnasema hakuna Mungu ni Kwa sababu hamjapata bahati ya kufundishwa kujumjua Mungu kupitia Quran it's means nyinyi chimbuko lenu ni Ugalatia
Hata siku Moja hautamkuta mtu aliyekulia katika uislam akasema hakuna Mungu hata kama atatoka katika uislam atapinga tu baadhi ya mambo lakini hata siku Moja hawezi kusema hakuna Mungu
Jiandae bro Jahanamu inakusubiri
Yani Mungu atengeneze Jua ashindwe kutengeneza Jahanamu?