Kuna watu wajinga hawaamini kuwa Mungu yupo na ndiye anshikilia uhai wa mtu na ndiye mtu mwenyewe.
Mtu anapofanyiwa ubaya na kumwachia Mungu onategemea na tafsiri yako. Kwani wewe ukifanyiwa jambo ukaichia mahakama iamue unakuwa mjinga? Ukiiachia mahakama, je hautaipa ushirikiano wa kutoa ushahidi? Tatizo haumjui Mungu unadhani kanisa na msikiti ndio Mungu au ndio makazi ya Mungu. Punguza ujinga, ukitumia akili yako japo kwa 1% utajua Mungu yupo, na yupo ndani ya Moyo wako. Keenye dini ni Mungu na Shetani, kwenye jamii ni Mema na Mabaya, kwenye sayansi ni Chanya na Hasi. Ni elimu ndevu inahitajika kuvunja ngome ya mawazo uliyo nayo umeijenga miaka nenda rudi.
Uelewa wako ni mdogo sana kukuhusu wewe na Mungu na shetani, dini na wafu. Kinachozikwa ni mwili wako lakini sio wewe unaeishi katika mwili. Vile mmeaminishwa ujinga mnaamini mtu ni mwili unaokufa na kuzikwa. Zinduka, kuna sayansi na historia uchwara iliyoletwa kushikilia mateka mawazo yenu, sawa na dini tu uhalisia hauhubiriwi.
Mwanadamu kushindwa kuutambua ukweli haimannishi kuwa Mungu na shetani hawapo. Mungu yupo, na shetani hana hadhi ya ulinganifu na Mingu bali ni kiumbe aliyeasi na kusambaza uongo wa uasi wa wanadamu kama wewe. Ili wasimwamini Mungu kwa elimu uchwara inayojaribu kumchunguza Mungu aliye asili ya kila kitu. Yaani mawazo ya kiumbe yaanze kuchunguza akili ya Muumbaji. Sub set ianze kuichunguza set wakati imebebwa (hosted) na set. Huu utakuwa wendawazimu