Mungu wangu!
Mdakuzi umeona sasa?
Nilisema mimi,zisipofanyika jitihada za haraka na dhati tutampoteza huyu.
Hivi kwa hali aliyofikia anaachiwa wa nini huyu jamani?
Si afungiwe ndani tu?
Sasa huko anakoshinda na mateja akizidiwa si wanajisevia watakavyo?
Jamani naumia hadi machozi yananitoka.
Ray C lifestyle uliyojichagulia inagharimu maisha yako sasa!
Nilikwambia huyu mtu ni mbishi sana, sio msikivu. Wakati wote anaamini yuko sahihi, na anaamini anaweza kuficha mabaya anayofanya, hataki kufikiria kama sasa nchi nzima inamtazama yeye kwa kuwa alianza kupata tiba kwa msaada wa Rais akimsaidia kwa hali na mali.
Kusema kweli ukiyasikia yote ya Ray C yanaumiza sana, tena yanaumiza kupita kiasi. Ukikaa naye mkazungumza atasema mikwamo yake iliyosababishwa na Ruge hadi atakulilia kupita kiasi, mama yake akisafiri nje anafikia wakati anakuwa hana hata nauli ya kufikia kituoni kunywa dawa.
Rais alikuwa tayari kumsaidia masomo ya uigizaji wa filamu Marekani baada ya kumaliza tiba, kama Ray C alivyoomba, lakini Ruge akamuahidi mbele ya Rais kuwa amtasaidia kumfanya arudi juu kimuziki, na kumfanya Ray C aamue kurudi tena kwenye muziki ambao alishaukatia tamaa.
Akapoteza nafasi aliyopewa na Rais, na baada ya muda Ruge naye akamtosa, akamkatalia kulipia video ya wimbo wake kwa sababu amenenepa sana, kwa hiyo anamtaka apungue ndio atoe hela ya kurekodi video. Na Ray C alinenepa kwa sababu ya dawa za uteja anazokunywa, ni ngumu kupungua.
Kwa kauli hiyo akaamini ameshatoswa, ndio maana alishawahi kutangaza kutafuta mtu wa kumsimamia kimuziki kwani tayari ana nyimbo nane amesharekodi, lakini hazina video. Alishatoa hadi namba zake za simu kwa anayetaka kumsaidia awasiliane naye, ila hakupata.
Sasa kwa akili ndogo za Ray C akashindwa kukabiliana na hiyo hali kwa kutafuta namna ya kutoka hapo, kwani hata Jide alipitia hali kama hiyo kwa Ruge, lakini akapambana akasonga.
Yeye kwa akili zake haba akarudi kutumia dawa za kulevya akidhani anaweza kutuficha tusijue.
Sasa jana kulifanywa mpango akakutanisha na Seven anayemsimamia Alikiba na Jide, na wakafanya mazungumzo kwa ajili ya kumsaidia kimuziki, sasa kama unavyoona matokeo yake leo unakuja kusikia amezima baada ya kupitiliza matumizi ya dawa za kulevya, sasa kama ni kweli nadhani ni ngumu kumuokoa.
Ova