Kuna habari humu kwamba Rais Jakaya Kikwete Kamsaidia RAY C kupata tiba baada ya kuathiriwa na utumiaji wa madawa ya kulevya, nimeshindwa kuzifuatilia taarifa hizi kwa usahihi na undani hasa baada ya kugundua watu wengi wanachukulia kitendo hiki kama cha kiungwana.
Naomba kukumbusha kwamba, wakati Rais Jakaya kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 dada huyu hakuwa mtumiaji wa dawa za kulevya (niko tayari kusahihishwa katika hili) na ni mtu huyu huyu aliyesimama ndani ya bunge letu na kudai ana majina ya wauzaji wa dawa za kulevya na akawapa muda waache kujihusisha na biashara hizo, toka hapo mtu huyu hakurudi kutueleza ombi lake limefanyiwa kazi kwa kiwango gani japo huku uraiani toka kipindi hicho utumiaji wa dawa za kulevya umeongezeka mara dufu, vijana wengi sana wakike na kiume wanaathirika vibaya sana na utumiaji wa dawa hizi, wafanyabiashara wa madawa haya sasa wanafanya biashara hiyo bila woga wala kificho, athari ni kubwa katika kila familia nchi nzima, mpaka vijijini watu wanatumia dawa za kulevya, sio bangi tu, mpaka cocaine.
Mara ya mwisho kumsikia akizungumzia tatizo hilo, ni pale alipodai kwamba mpaka viongozi wa dini wanahusika na usambazaji wa dawa za kulevya, kisha akapotea.
Leo, kama ni kweli, zinaibuka taarifa kwamba kamsaidia msanii wa muziki kujitibia maradhi yanayotokana na athari za madawa ya kulevya, inaonekana haelewi namna ya kutekeleza majukumu yake ya Urais au hayaelewi kabisa, au anafaidika na biashara hii, kama sio yeye binafsi basi wanafamilia yake, au chama chake, au maswahiba wake, sina namna ingine ya kutafsiri uzaifu huu.
Naomba kuwasilisha ombi kwa Rais na Chama Chake cha CCM kuacha usanii, washughulikie tatizo la dawa za kulevya kwa vitendo.