Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

CONGRATURATION: Mr. President, But i think you need to put more effort because u've only 2 out 10 yrs to help others.
 
kuna mtoto yupo pale Kariakoo mbele ya kituo cha Polisi cha Msimbazi.
Ana tatizo la kuvimba kichwa, yaani ukimuona tu utaingia na roho ya huruma papo hapo, na ni wazi kuwa wazazi wake hawana uwezo wa kumpeleka nje kwenda kufanyiwa uchunguzi na hata kupata matibabu.

Dah leo hii Mkuu unakwenda kulitibia jitu zima na akili zake kwa tatizo la kununua.
Mkuu nakuchukia sana, lakini kwa hili chuki yangu imezidi maradufu.

Wasalaam...
Gang Chomba..,
 
Aiseee ! kumbe inawezekana , sasa ngoja kesho niandikishe majina ya mateja wa pale kwa manyanya kisha niwakusanye niwapeleke Ikulu ili nao wapate tiba kama ya Rehema. Ebo! kumbe teja anaweza pona na kuanza kujirusha
 
basi ray c alikua haumwi. Alikua ana tekeleza mpango wake kabambe wa kurudi juu.
REHAB ya mwezi!!!!!!!! Sijawahi kuona aise.
Ili igizo linaweza kumtoa


Nilidhani kuwa niko peke yangu ninayejiuliza hili! Asante Mkuu. Binafsi hapa naona kama kuna Usanii Fulani. Huyu Bidada ni mawiki machache tu yaliyopita tumeanza kusikia kelele za kutaka achangiwe kwa sababu alikuwa ameathirika na madawa! Wiki zisizozidi NNe tu baadaye tunaambiwa ameishapata nafuu na ameweza hata kumuona Raisi wa Nchi ili Kumpa asante kwa Mchango wake!
Hivi Jamani tunajua kweli maana ya Kuathirika na Madawa ya Kulevya?? Hivi kweli aliyeathirika kweli inamchukua wiki MbiliTatu tu Kupona kiasi cha kwenda kuona Raisi Kumshukuru??
Tuache Mizaha.
Je wale wengine wote waliomchangia kupitia FaceBook baada ya Tangazo la Mheshimiwa mmoja mwanamuziki Mkongwe la kutaka Tumchangie, atawapitia wote Kuwashukuru??
Nini Kinafuata baada ya Hapa?
Je Raisi baada ya kushuhudia madhara ya mihadarati, atachukua hatua ya kuwataja na kuwachukulia hatua zinazostahili wale wanaosemekana kujihusisha na biashara hii haramu, kwa kuanzia na wale atakaotajiwa na RAY C??
Kuna Mengi jamani tunapaswa kujiuliza badala ya kushangilia kitendo hichi ambacho kinaweza kikawa si zaidi ya mtu kutafuta Cheap Popuralty!

 
Mwimbaji mashuhuri hapa Tanzania, Ray C, ametangaza kupona na matatizo ya yaliyokuwa yakimsumbua. Ametangaza hayo akiwa Ikulu baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa Mh. Rais Kikwete.

attachment.php

RAY C AKIMSHUKURU RAIS KIKWETE

attachment.php


RAY C, MAMA YAKE NA DADA YAKE WAKIMSHUKURU RAIS KIKWETE

huyu mchizi baada ya kusakamwa na zile suti za lile zungu kaamua kutafuta fundi mpemba, hizi suti maarufu sana kule pemba, mfukoni hakosi CHARM.
 
haya msaada kapata je hata rudia tena? au ndo changa la macho, 2kiachana na yote hayo ashukuriwe mwenye nchi kwa kumuokoa binti ye2 naamini atakuwa amepata funzo.
 
Huyu ray c si mwanamke wa boss wa clouds entertaiment
hakumsaidia?
Mimi nasikia huyo boss anawabebesha ngada hawa wasanii zile safari za nje wanarudi na mzigo
na laana ya ngada lazima na wewe ubwie au kizazi chako
mhhhh hii ndo dar si lamu
 
Kikwete kweli hana kazi ya kumsumbua kichwa, unaweza kweli kuwa na time ya kukutana na wasanii au msanii wa fani yeyeto instead ya kushughulikia majukumu ya nchi yetu, jamaa ni mtu wa showoff 2much
 
Jamani. Kweli kila mtu na bahati yake. Yule mama alooza mguu hadi sam mahela kampigia debe kwa watz hakusaidiwa. Yule dada mwathirika wa mabomu tena kwa uzembe wa serikali. Hatujasikia serikali kusema lolote
 
Ni vizuri kwa Rais Jakaya Kikwete amemsaidia Rehema Chalamila “Ray C” matibabu kutokana na addiction za madawa ya kulevya iwe kwa moyo au publicity. Nampenda Rehema ni dada mzuri, alikua ana tu intertain n.k.

Maoni yangu binafsi;

Tanzania kuna wagonjwa wengi ambao wapo mahospitalini na wengine wanavilema vya kuto kujitakia wanahitaji msaada. Raisi JK anajua hili na amewaona watu wanao hitaji misaada mahospitalini wengi ambao ni INNOCENT ila magonjwa tu yamewapa afya mbaya bila kujitakia. Hawana vyandarua, hawana vitanda, hawana madawa.

Ray C ni mtu mwenye akili timamu, alijiingiza kwenye madawa ya kulevya kwa hiari yake, iwe kwa influence ya marafiki, frustrations, au whatever. Nakubali ni celebrity na ni kioo cha jamii, ameshindwa kuwa kioo cha jamii at the first place ataweza kuwa kioo cha jamii sasa? Anasaidiwa sasa tuna uhakika gani hii tabia haita jirudia?
Binafsi, naona Raisi Jakaya Kikwete amecommit unethical act kwa wale wanao hitaji msaada kabla ya Ray C, wapo mahospitalini bila KUJITAKIA. Sioni sababu ya kusaidiwa yeye kabla ya watu wanao hitaji misaada mahospitalini. Sioni sababu ya kusaidiwa Ray C na kuweka kwenye vyombo vya habari kabla ya kutatua mgogoro wa madaktari ambao wanainfluence afya ya mtanzania na wagonjwa ambao wapo hospitalini kabla ya Ray C.

Muongozo:

Wamarecan wanafanya hivi; kama una hitaji organ transplant, unawekwa kwenye waiting list. Sasa basi, kama wewe uli haribu organs zako kwa ajili ya anasa, madawa, pombe na sigara, hawakuweki hata kwenye waiting list. Wanakuacha unakufa tu kwa kuwapa kipaumbele wale ambao hawakuabuse pombe, sigara n.k. Wanasema hivi tukimpa organ mpya “ATAENDA KUIHARIBU TENA” kwa hiyo inabidi awe wa mwisho kufikiriwa.

Kilicho fanyika:

Kama Tanzania tunge kuwa tuna organ waiting list, watu wanahitaji liver, heart, kidney, lungs n.k. Lets say kuna watu 1000 wanasubiri. Harafu Ray C analetwa na JK na anawekwa namba moja mbele ya watu 1000. Ingekuwa ni haki au ethical kwa sababu ni CELEBRITY? HILI NDILO LIMEFANYIKA HAPA KWA MTAZAMO WANGU. Na ni risk kumsaidia huyu mtu kwani anaweza kwenda ku BLOW organ hiyo tena.

Mwisho;

Ni mtazamo wangu na naamini wewe pia una wako. Tanzania imefika wakati tufanye mambo ki ethical na sio political.

GREAT THINKERS, LETS THINK ETHICAL-

Rehema Chalamila "Ray C" nakutakia afya njemba
 
kuna mtoto yupo pale Kariakoo mbele ya kituo cha Polisi cha Msimbazi.
Ana tatizo la kuvimba kichwa, yaani ukimuona tu utaingia na roho ya huruma papo hapo, na ni wazi kuwa wazazi wake hawana uwezo wa kumpeleka nje kwenda kufanyiwa uchunguzi na hata kupata matibabu.

Dah leo hii Mkuu unakwenda kulitibia jitu zima na akili zake kwa tatizo la kununua.
Mkuu nakuchukia sana, lakini kwa hili chuki yangu imezidi maradufu.

Wasalaam...
Gang Chomba..,

Umeongea ukweli... Najiuliza maswali mengi sana kwakweli.. Hivi kuna watoto yatima wangapi wanamahitaji?? Na niwangapi alisaidia wakataka kwenda ikulu kumshukuru japo kwa mkate alowapa wakanyimwa appoimtment eti!!! Mkuu yuko buzy?.. Inatufundisha nini kwenye hili?? Kamsaidia Mtumia madawa ya kulevya mmoja kati ya wangapi au kakemea nini kwenye hili.??? Anyway kuna viongozi hawana kazi wala washauri wazuri!! Alichokifanya mh. Rais wetu sio sawa....
 
[h=3]RAY C SASA AFYA TELE,AIBUKA IKULU NA MAMA YAKE KUMSHUKURU JK KWA MSAADA WA MATIBABU.[/h]
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu, alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa pili kulia), Mama yake mzazi Ray C, Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais
.

 
Ray C hajapona huwezi kupona utumiaji wa madawa ya kulevya kwa mwezi mmoja au miwili kwani huu sio ugojwa wa malaria ambao unatumia dawa na kupona. Watumiaji wa madawa ya kulevya wanahitaji watalaamu wa kuangalia akili na atahitaji uangalizi wa muda mrefu kwani kama ulevi bado atakuwa na hamu ya kutumia madawa kwa muda mrefu na akirudi huko anaweza asipone tena. Inabidi atulie na atafute mtu wa karibu kama boyfriend ambaye yuko tofauti na anamtakia mema, kijana serious na wazazi wawe karibu. Kama ataendelea kujirusha na ma rapper n.k atarudi kulekule!
 
Mwimbaji mashuhuri hapa Tanzania, Ray C, ametangaza kupona na matatizo ya yaliyokuwa yakimsumbua. Ametangaza hayo akiwa Ikulu baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa Mh. Rais Kikwete.

attachment.php

RAY C AKIMSHUKURU RAIS KIKWETE

attachment.php


RAY C, MAMA YAKE NA DADA YAKE WAKIMSHUKURU RAIS KIKWETE

udini huu utaliponza taifa..ray c ni kwasabu ya uislam wake ndo maana kasaidiwa
 
pole Ray c, shukrani kwako rais, wakumbuke na vijana wengine wenye matatizo kama hayo walioko mitaani japo hawana majina makubwa zaidi ya Utanzania wao.
 
Rais anabagua watu kwa jinsi hadhi zao anakuwa si Rais bali rahisi!
Wenye matatiza kama ama zaidi ya ray c wapo wengi ni wangapi ikulu imesaidia?
Kumbuka maisha hayana uwakilishi?
KWANINI RAIS WANGU USIANZE MFIKO MAALUM UKAWASAIDIA KWA WINGI WAO?
 
Nchi hii imekumbwa na tatizo la utumiaji wa Madawa ya Kulevya kwa vijana wetu wengi kilichopo hapa nchini zimeundwa Taasisi nyingi zinazoshughulikia watu(Vijana) walioathirika na utumiaji huo wa Madawa ya Kulevya akiwemo mwanamziki Ray C ambaye matibabu yake yamegharamiwa na Mh. Raisi, Napenda kuuliza swali hili hii ndiyo utatuzi wa tatizo hili? mi kwa mtazamo wangu hapa serikali ilitakiwa wakati ikitoa matibabu haya basi upande wa pili hawa waathirka walitakiwa wawe washitakiwa na ni watu muhimu sana ambao watasaidia kupatikana kwa wauzaji wa madawa haya tunapotoa matibabu tu huku hawa jamaa wakiendelea na biashara yao hili sio suruhisho serikali iliangalie hili ili tuweze kudeal na mizizi na shina sio kudeal na majani yaliyoanguka kwenye mti huku mti na mizizi ikiendelea kustawi.
Yangu ni hayo tu wajameni!
 
Back
Top Bottom