JK KUMSAIDIA RAY C NI VIZURI, BUT UNETHICAL
Ni vizuri kwa Rais Jakaya Kikwete amemsaidia Rehema Chalamila Ray C matibabu kutokana na addiction za madawa ya kulevya iwe kwa moyo au publicity. Nampenda Rehema ni dada mzuri, alikua ana tu intertain n.k.
Maoni yangu binafsi;
Tanzania kuna wagonjwa wengi ambao wapo mahospitalini na wengine wanavilema vya kuto kujitakia wanahitaji msaada. Raisi JK anajua hili na amewaona watu wanao hitaji misaada mahospitalini wengi ambao ni INNOCENT ila magonjwa tu yamewapa afya mbaya bila kujitakia. Hawana vyandarua, hawana vitanda, hawana madawa.
Ray C ni mtu mwenye akili timamu, alijiingiza kwenye madawa ya kulevya kwa hiari yake, iwe kwa influence ya marafiki, frustrations, au whatever. Nakubali ni celebrity na ni kioo cha jamii, ameshindwa kuwa kioo cha jamii at the first place ataweza kuwa kioo cha jamii sasa? Anasaidiwa sasa tuna uhakika gani hii tabia haita jirudia?
Binafsi, naona Raisi Jakaya Kikwete amecommit unethical act kwa wale wanao hitaji msaada kabla ya Ray C, wapo mahospitalini bila KUJITAKIA. Sioni sababu ya kusaidiwa yeye kabla ya watu wanao hitaji misaada mahospitalini. Sioni sababu ya kusaidiwa Ray C na kuweka kwenye vyombo vya habari kabla ya kutatua mgogoro wa madaktari ambao wanainfluence afya ya mtanzania na wagonjwa ambao wapo hospitalini kabla ya Ray C.
Muongozo:
Wamarecan wanafanya hivi; kama una hitaji organ transplant, unawekwa kwenye waiting list. Sasa basi, kama wewe uli haribu organs zako kwa ajili ya anasa, madawa, pombe na sigara, hawakuweki hata kwenye waiting list. Wanakuacha unakufa tu kwa kuwapa kipaumbele wale ambao hawakuabuse pombe, sigara n.k. Wanasema hivi tukimpa organ mpya ATAENDA KUIHARIBU TENA kwa hiyo inabidi awe wa mwisho kufikiriwa.
Kilicho fanyika:
Kama Tanzania tunge kuwa tuna organ waiting list, watu wanahitaji liver, heart, kidney, lungs n.k. Lets say kuna watu 1000 wanasubiri. Harafu Ray C analetwa na JK na anawekwa namba moja mbele ya watu 1000. Ingekuwa ni haki au ethical kwa sababu ni CELEBRITY? HILI NDILO LIMEFANYIKA HAPA KWA MTAZAMO WANGU. Na ni risk kumsaidia huyu mtu kwani anaweza kwenda ku BLOW organ hiyo tena.
Mwisho;
Ni mtazamo wangu na naamini wewe pia una wako. Tanzania imefika wakati tufanye mambo ki ethical na sio political.
GREAT THINKERS, LETS THINK ETHICAL-
Rehema Chalamila "Ray C" nakutakia afya njemba