Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Kama una taarifa zozote juu ya wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya zipeleke tume ya kupambana na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya. Pale watazifanyia kazi kwa kuwafungulia mashtaka hao unawaongelea.
Hicho unachokiongea kinawezekana lakini Hoja yangu inasimama kwenye njia rahisi ya kupambana na suala hili kwani ukianzia na mtumiaji atakutajia muuzaji mdogo na muuzaji mdogo atakutajia muuzaji Mkubwa na mwisho wa siku tutafanikiwa kung'oa shina na mizizi yake nafikiri unanipata R.Sweety
 
Marehemu Amina Chifupa alisema anawafahamu wauzaji wa madawa ya kulevya! Pia kuna wakati JK alisema anawafahamu wauzaji akawaonya viongozi wa Dini wanaojihusisha waache la sivyo atawataja! lakini pia swala la kuhoji wale vijana wanaokamatwa katika viwanja vya ndege huwa hawawataji mabosi wao!? Usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama wanashindwa kuwabaini hao wauzaji!? mimi nataka niseme hawa wauzaji wakubwa wakubwa ni mtandao mpana unaowajumuisha wakubwa wa serikali pia! Ndio maana ni ndoto kuwadhibiti
 
Habari hizi nimezisoma kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Rehema Chalamila ‘Ray C', juzi ametinga Ikulu kufikisha shukurani zake kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na kumpatia msaada wa matibabu.
Ray C aliyefuatana na mama yake mzazi, Margareth Mtweve, na dada yake, Sarah Mtweve, alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake waliomkosa kwa muda sasa.
Kwa apande wake, mama mzazi wa Ray C, alisema anamshukuru Rais kwa kuokoa maisha ya mwanaye kwani hali ilikuwa ya kusikitisha wakati alipokuwa akiumwa.
Aidha mama Ray C amesikitishwa na baadhi ya watu kutumia fursa ya matatizo ya mwanaye kuwa chanzo cha kujipatia fedha kwa kukusanya michango eti kwa ajili ya matibabu.
Mama Ray C aliongeza kwa kuwataka baadhi ya watu ambao wanafanya vitendo hivyo kuacha mara moja kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais. " Hoja yangu, pamoja na kwamba sina uhakika kuwa Mh Rais alitumia mshahara wake kulipa matibabu ya Rayc, bado nashawishika kuwa alitumia fungu lililoko kwenye bajeti ya Rais ambazo ni kodi zetu kumsaidia msanii huyo jambo ambalo kwa hakika ni jema sana. Sasa kwa vile tumekuwa na matukio ya magonjwa ya ajabu ajabu hasa kwa watoto, matukio kama vidonda vikubwa vya ajabu, kuvimba, kuzaliwa na kasoro za kimaumbile za ajabu, au kama yule mama wa Siza aliyevimba mguu ambaye Mwandishi Sam Maela( kama sikosei) amekuwa akimpigia debe kwa wasamalia wema, badala ya kusubiri michango midogomidogo ya watu binafsi, jambo ambalo laweza gharimu maisha, kwa nini serikali isiwe na utaratibu wa kushughulikia matatizo ambayo si magonjwa ya kawaida na ambayo yanahitaji utaalamu zaidi? Naomba niwe specific, case kama hizi si za mara kwa mara na zinapotokea kila mtu anashangaa. Mfano mtoto anazaliwa hana sehemu ya haja kubwa, halafu eti mpaka aende vituo vya TV kujitangaza aombe msaada? No inauma sana, kwanini wizara HUSIKA isimalize hilo tatizo maana kwa kufanya hivyo Watanzania wote tuaolipa kodi tutakuwa tumeshiriki. Kama Rais ameweza kwa RAY C wakuu wa mikoa , wakuu, wa wilaya na kadhalika waliochini ya mfumo wa serikali wanaweza pia kuwasaidia ndugu zetu. Halafu tunaweza kuwa na utaratibu wa kuchangia mfuko huu wa magonjwa ya ajabuajabu ambako sasa ndio michango hii ingekuwa inakwenda kutunisha mfuko. Hebu tujadili

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Ray C amshukuru Kikwete

na Shehe Semtawa

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif

[/TD]
 
Uko sawa.
Rais asiangalie haiba au urembo au uzuri wa sura ya mhitaji.
 
Kila kitu kina malengo yake, umejaliwa kumuona huyo dada mtu wa RayC? sijui kama mkulu hajakamua au hatakamua.
 
.Hapana mdau, mimi nadhani hapa kuna faida kubwa ya kumsaidia dada huyu ambaye kwa kweli ni kioo cha jamii.Alichofanya Mkuu wa Kaya naamini kinalenga kumfanya mwanadada huyu kuwa balozi mzuri wa kuelezea madhara ya wazi yanayotokana na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa yeye mwenyewe amekumbana nayo,na jamii inajua hivyo.Na kwa kuzingatia kipaji cha hali juu cha uimbaji alichonacho mwanamama,itakuwa ni rahisi sana kwake kutumia jukwaa la sanaa ya muziki katika kupiga vita utumiaji wa unga na hivyo vijana wengi ambo ni wadau wakubwa wa athari hizo na ambao pia ni wadau wakubwa sana wa muziki,kupata elimu na ujumbe huo kirahisi zaidi.
Sote tunafahamu namna muziki ulivyo na nguvu katika kusambaza ujumbe kwa jamii.Hivyo basi,ninachokitegemea kutoka kwa mdada huyu ni kutunga tungo na kutumia majukwaa yake ya muziki kupiga vita utumiaji wa kilevi hiki hatari ili vijana wengi wapate kupona kwenye janga hili. Hivyo, nashawishika kuamini kuwa hilo bila shaka ndio lililokuwa kusudio la Mkuu wa Nchi katika kumsaidia binti huyu.

Unamkumbuka LANGA wa wakilisha?
 
Siku mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila, maarufu kama RAY C, alipomtembela Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 10, 2012 Ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliyompatia wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake sasa imeimarika na kwamba muda si mrefu ujao atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.

Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
 
hivi kwanza alikuwa anaumwa nini hadi raisi akaingilia kumsaidia matibabu??
je wasanii wangapi ambao rais huwa anawasaidia kimatibabu ila hawajaonyesha moyo wa shukurani??
 
hivi kwanza alikuwa anaumwa nini hadi raisi akaingilia kumsaidia matibabu??
je wasanii wangapi ambao rais huwa anawasaidia kimatibabu ila hawajaonyesha moyo wa shukurani??

we mamito hebu achana na haya makitu juzi nilitoka povu humu!kama sina akili nzuri!
mi nachoka sana na haya mambo we acha tu!tukajilie zetu tu mbuzi wa foilini pale uhuru park basi!ah
 
hahahahahah alikuwa tejaaaaa! eti anasema raisi baba yake kamponya ,this is absurd kwani kikwete ni MUNGU hadi amponye??? unafki tu...mr.dhaifu@work
we mamito hebu achana na haya makitu juzi nilitoka povu humu!kama sina akili nzuri!
mi nachoka sana na haya mambo we acha tu!tukajilie zetu tu mbuzi wa foilini pale uhuru park basi!ah
 
Tanzania concept ya fairness haipo, at least kwa rais wetu.

Marekani ukiwa na watoto wako wawili, mmoja ana miaka minne na mwingine sita, ukimfanyia kitu mmoja bila kumfanyia mwingine lazima mmoja atalia "That's not fair".

But I guess Tanzania is Tanzania and the U.S.A is the U.S.A.

The question is, is this ethos of fairness something we should emulate?

Should President Kikwete be concerned about issues of favoritism before parading himself with the Ray Cs of Tanzania (who apparently had other avenues and a whole fan base to garner the requisite funds, as opposed to countless other Tanzanians who shall remain unknown and uncared for).

Why is Ray C so special?

Kuna Watanzania wangapi wanaohitaji msaada kama huu ambao hawana uwezo kabisa? Kigezo gani kimetumika kumchagua Ray C?
 
Kiranga kabla hatujafikiria concepts of fairness and favoritism hebu kwanza nieleweshe Ray C alikuwa anaumwa nini?? seriously sijui.
 
we mamito hebu achana na haya makitu juzi nilitoka povu humu!kama sina akili nzuri!
mi nachoka sana na haya mambo we acha tu!tukajilie zetu tu mbuzi wa foilini pale uhuru park basi!ah
kwani mai dia ishu ilikuwaje?? binafsi sijui lolote sijui nimezeeka ama??
 
"...Nashukuru rais ameniponyesha..." Halafu presidaa akawa ana tabasamu, I am speech less.
 
hahahahahah alikuwa tejaaaaa! eti anasema raisi baba yake kamponya ,this is absurd kwani kikwete ni MUNGU hadi amponye??? unafki tu...mr.dhaifu@work
don't tell! Ray c aaalikuwa teja?? so raisi wetu akamsaidia pesa za matibabu sio, ni jambo jema sana tena lapaswa kuigwa. but naomba mnijuze jambo hapa hivi anayejeruhika katikati ya starehe na anayejeruhika katikati ya kazi who needs sympathy??
 
kwani mai dia ishu ilikuwaje?? binafsi sijui lolote sijui nimezeeka ama??
alikuwa teja bana!
zikatolewa picha humuu kuwa anahotaji msaada nakumbuka shosti yetu mutoto ya fisadi alisema watanzania tumchangi sijui!weell kwake yeye na wengine ilieleweka!
si ndo chighafula hapa(wapi dada mkubwa FP )tunakutana namipicha na taarifa za habari oh rais kamtibu ray c na rayc,mama yale na dada yake wameenda ikulu kumpongeza basi ITV walitoa habari,TBC ,CHANNEL 10 mradi tu mambo mzomzo!
nilijiuliza maswali mengi sana mwenzio!na mpaka sas sijapata jibu ndo mana nakwambia tukajilipue tu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom