.Hapana mdau, mimi nadhani hapa kuna faida kubwa ya kumsaidia dada huyu ambaye kwa kweli ni kioo cha jamii.Alichofanya Mkuu wa Kaya naamini kinalenga kumfanya mwanadada huyu kuwa balozi mzuri wa kuelezea madhara ya wazi yanayotokana na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa yeye mwenyewe amekumbana nayo,na jamii inajua hivyo.Na kwa kuzingatia kipaji cha hali juu cha uimbaji alichonacho mwanamama,itakuwa ni rahisi sana kwake kutumia jukwaa la sanaa ya muziki katika kupiga vita utumiaji wa unga na hivyo vijana wengi ambo ni wadau wakubwa wa athari hizo na ambao pia ni wadau wakubwa sana wa muziki,kupata elimu na ujumbe huo kirahisi zaidi.
Sote tunafahamu namna muziki ulivyo na nguvu katika kusambaza ujumbe kwa jamii.Hivyo basi,ninachokitegemea kutoka kwa mdada huyu ni kutunga tungo na kutumia majukwaa yake ya muziki kupiga vita utumiaji wa kilevi hiki hatari ili vijana wengi wapate kupona kwenye janga hili. Hivyo, nashawishika kuamini kuwa hilo bila shaka ndio lililokuwa kusudio la Mkuu wa Nchi katika kumsaidia binti huyu.