Msanii Kajala Masanja ameibuka na kuitaka serikali iwachukulie hatua Hamisa Mobetto na Rayvanny kwa kumnywesha pombe binti yake aitwaye Paula na kisha kumrekodi video kuashiria yupo katika mahaba na Rayvanny. Awali zilivuja mtandaoni video zilizoonesha Rayvanny na Paula wakiwa katika penzi zito.
Kajala amedai siku ya tukio Hamisa alimuomba Kajala atoke na Paula wakatembee kumbe alikuwa na ajenda ya siri, alimchukua Paula na kwenda naye kwa Rayvanny ambapo walimnywesha pombe na Kisha kumrekodi kipande cha video chenye maudhui ya mapenzi mazito.
Punde baada ya kipande hicho cha video kuachiwa mtandaoni Rayvanny aliachia kipande cha wimbo kilichotafsiriwa Kama wimbo kwa ajili ya Paula.
Kitendo hicho kimetafsiriwa na wataalamu wa mambo Kama kiki ili tu Rayvanny naye apate kutrend hasa ikizingatiwa kuwa mama yake na Paula yaani Kajala anatoka na Harmonize.
Lakini je nini hatima ya sokomoko hili endapo mamlaka za serikali zikiingilia kati kuitikia wito wa Kajala anayedai binti aliyenyweshwa pombe ni mwanafunzi na mwenye umri mdogo?
Je hili halitamtia Rayvanny matatani kumnywesha pombe binti wa miaka 17 tena mwanafunzi na kumrekodi?
View attachment 1702362View attachment 1702363