Nimeona habari na video mitandaoni zikisema Rayvanny ana mahusiano ya kimapenzi na Paula mtoto wa kajala. Nijuavyo ni kuwa Paula alifeli form four wazazi wake wakamrudisha shule akawa anarisiti huku anasoma five na six, hivyo habari hizi za rayvanny zimenishtua kidogo. Vipi Paula ameacha shule? Na Kama bado anasoma kudate wanafunzi ni kosa linaloweza kumpeleka mtu jela miaka 30.
Na hata Kama ameacha shule bila shaka atakuwa underage huyo Paula ambapo pia ni statutory rape chini ya sheria kutembea na msichana chini ya miaka 18.
NB: Mamlaka zilifuatilie hili swala na ikibainika Kuna jinai zichukue hatua stahiki, yaani sheria ifuate mkondo wake wasanii ni vioo vya jamii hivyo wanapaswa kuwa wa mfano wa kuigwa, watoto waachwe wasome kwanza.