Mnhhh hili ni swala letu lote,je wote tukianzisha mahusiano tukiwa na miaka 19 tutajenga jamii ya aina gani??
Kama unaitegemea jamii ya sasa hivi isiyo mjua Mungu,isiyofuata maadili unakosea dada yangu.Jamii hii ya inayo funzwa na social networks ,blogs,website za ngono ambapo kumejaa uchafu wa kila aina,jamii ambayo wanakuambia "EMBE MBICHI NITALIA NA CHUMVI........" jamii hii inayo promoti KWENDA KWA MPALANGE KULIKO CHUMVINI,jamii hii ya MTOTO WA MWENZIO NI MKUBWA MWENZIO RUKA NAE unakosea sana,kwani jamii yetu haina HOFU na wala HAMUOGOPI MUNGU.
Kitu cha kwanza timiza wajibu wako kama mzazi mfundishe mwanao baya na zuri,muongoze ktk njia azipendazo Mungu na usisaha kumweleza yeye ni nani anatakiwa afanye kitu gani kwa wakati huu,muepushe na hizi simu hasa smartphone kwa wakati wa u-teenager wake,hizo ndizo zitakuwa ni silaha za kupambana na jamii tulio kuwa nayo hivi sasa.
Vinginevyo kama usipotimiza wajibu wako kama mzazi,basi atakutana na walimwengu na walimwengu wengi wao ni wabaya bora akutane nao wazuri wa kusadie kumrekebisha.
Siku hizi jamii hiyo unayo izungumzia ww hamna,zamani jirani kama akikuona unakosea ana uwezo wa kukuadhibu na mzazi akaelewa,ila jamii ya sasa hivi umuone mtoto wa jirani yako anakosea alafu ukamwadhibu,utajenga uadui mkubwa na huyo mzazi anaweza kukupeleka mpaka kwenye vyombo vya sheria.
Jamiii ile ya wazee wetu ya mtoto wa jirani ni mtoto wako ishapotea,kama ipo basi haivuki 3%,ndio maana watoto wa siku hizi wana tabia za ajab ajabu.