RC Chalamila: Mkiendelea kuchanganya Dini na Siasa huko mbele patatokea mtawala atakayeamua kufunga makanisa yote na hamtamfanya chochote!

Kwanini wao wanachanganya serikali na ccm na huku wanajua kiongozi wa serikali kachaguliwa na watu wote wenye vyama na wasio na vyama.Wanaona ni sahihi kiongozi wa serikali kufanya kazi za serikaki akiwa amevaa manguo ya vyama.
 
Hivi alifikaje kwenye hilo Kanisa? Hivi kuna mtu anaalika hili jamaa kwenye shughuli ya Dini?
Tatizo makanisa yanajikomba Sana kwa Wana siasa. Jumapili iliyopita alikuwa kwenye kanisa la sloam.
 
Kanisa lisiwe kama vyama vya Siasa ambavyo baada ya kuruhusiwa Kufanya Mikutano badala ya kuhubiri Sera Zao wao wanaporomosha Matusi

Eti baada ya kuruhusiwa...

Hawa jamaa sijui huwa wanajipata kina nani...
 
Thubutu!
 
Mbona unakwepa ukweli?. Acha kupotosha. Yeye kadai Wana uwezo wa kufungia makanisa.
 
HOTUBA YA CHALAMILA

15 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Kongamano hilo lilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwakutanisha Wachungaji wa Kanisa hilo kutoka mikoa ya Dar es Salaan na Pwani, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ndiye aliyekuwa mgeni rasmi


View: https://m.youtube.com/watch?v=rfl9ynf-Tg8

TOKA MAKTABA
Nyerere akihutubia kanisa na ukombozi dhidi ya dhulma na unyonyaji pia dhima ya kuleta usawa kupitia liberation theology kutoka latino Amerika katika mapinduzi ya kuleta maendeleo ya watu na kupinga ukandamizaji

JULIUS NYERERE Former President of Tanzania Speech in Nicaragua in 1988


15 September 2023

HOTUBA YA ASKOFU MKUU TAG, DK. MTOKAMBALI KWA MKUU WA MKOA WA DSM, KWENYE KONGAMANO LA WACHUNGAJI DAR



View: https://m.youtube.com/watch?v=1RcXWCJM2qw
Askofu Dkt. Mtokambali kanisa la TAG tumepanga kuibua viongozi wapya 35,000 na makanisa mapya ya TAG 30,000 katika maeneo 40,000 tuliyoaanisha ndani ya mpango kazi wetu .... pia nchi yenye uchumi wa kati chini hatuwezi kukaa bila kuwa na mkakati wa maendeleo ya watu ambao wengi ni masikini katika nchi yetu ....
 
Haijawahi kutokea na haitatokea kwa kanisa kukaa kimya huku likiamini raia wa kawaida wanakandamizwa. Miaka yote kanisa ni sauti ya wasio na sauti. Ni sauti ya unabii na kazi ya nabii ni kuonya na hata kukaripia ikibidi. Asome Biblia kwa makini ataona wafalme walivyokuwa wakikaripiwa na manabii pale wanapocheza fyongo kwa watu wa Mungu. Kwa kuwa Chalamila anafaidika na kinachoendelea, hatushangai kusikia kauli kama hizi kutoka kwake!
 
ati hamtafanya chochote, huyu jamaa akili yake sijui nifananishe na nini? anaamini wananchi hawatafanya chochote? akili au matope haya?
 
Mbona mfano wako ni irrelevant na context iliyopo kuhusu dini na siasa?
 
Huyo mtawala si anawekwa madarakani na kura za watu kwa ajili ya watu? Hivi hii tabia ya kutisha watu waliokuweka madarakani kupitia uteuzi wa Rais inatoka wapi? 😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…