RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara

Chanzo: ITV habari

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipaka kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
 
RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Chanzo: ITV habari!
 
Kuna machinga wamejenga mabanda yaani utadhani maduka ya nguo baadhi ya maeneo, leo hapo ubungo darajani upande wa msikiti nimekuta ugomvi jioni hii mtembea kwa miguu amekanyaga Nyanya daah nimeacha timbwili hapo.....wamepanga service road yote.
 
Back
Top Bottom